Habari kwa simu

Idhaa ya Kiswahili ya BBC sasa inatoa huduma ya wavuti maalum kwa ajili ya simu za mkononi (Swahili mobile news site).

Huduma hii mpya inawewezesha watumiaji wa simu za mkononi kusoma taarifa za kila siku moja kwa moja katika simu zao badala ya kutumia kompyuta.

Hata hivyo ieleweke kuwa baadhi ya simu haziwezi kupata huduma hiyo kwa kuwa hazikuundwa maalum kuchukua mawasiliano ya tovuti.

Pia utatakiwa kuwa na uwezo wa kuingia katika internet kadri kampuni yako ya simu inavyokuruhusu, ingawa kuna uwezekano ukatakiwa kulipa gharama kwa matumizi yako.

Toleo la wavuti ya BBC Swahili mobile linapatikana kupitia simu za mkononi, PDA na vifaa vingine vya mawasiliano ya mkononi. Kutakuwa na taarifa za matukio na vile vile soka.

Anzisha browser kwenye simu yako kasha andika:

http://www.bbcswahili.com/mobile

Ukitaka kuweka kumbukumbu ya kiunganishi cha soka andika

http://www.bbcswahili.com/mobile/football

Kisha unaweza kuhifadhi ukurasa huu ili uweze kuupata tena kwa urahisi. Endapo huna uhakika kama unaweza kutumia tovuti kupitia simu yako, wasiliana na kampuni yako ya simu.

Gharama

Kulingana na aina ya mkataba ulionao, baadhi ya gharama za kutumia tovuti kwenye simu yako, unaweza ukatozwa gharama ambazo hujulikana kama “data charges”.

Endapo huna uhakika wa uwezekano wa kukatwa fedha kwa kutumia tovuti kwenye simu yako, tafadhali wasiliana na kampuni inayokupa huduma ya simu.

Huenda ikawa baadhi ya gharama zimejumlishwa katika malipo yako, au kwamba unaweza kujiunga na mpango wa matumizi ya tovuti ‘data package’ au ‘data packet’ unaolipia kila mwezi kupunguza gharama za kutumia tovuti.

BBC haitozi fedha kwa wanaotumia huduma ya wavuti kupitia simu za mkononi.