Tangazo: Matangazo ya Dira ya Dunia

Tunaomba radhi kwa wasikilizaji wanaofuatilia matangazo yetu kwa njia ya tovuti, kwamba kwa kipindi chote cha mashindano ya Kombe la Dunia hatutaweza kuwaletea matangazo ya Dira ya Dunia.

Sababu ya kufanya hivyo ni utekelezaji wa makubaliano ya hakimiliki za kutangaza michezo ya Kombe la Dunia kwa mujibu wa FIFA.

Idhaa ya Kiswahili ya BBC, inaruhusiwa kutangaza mpira wa Kombe la Dunia moja kwa moja kupitia redio, lakini hairuhusiwi kuweka matangazo hayo katika tovuti.

Kwa maana hiyo, matangazo yatakayokuwa yanasikika kwenye tovuti ni AMKA na BBC na Taarifa za Habari za kila saa.

Mara baada ya kumalizika kwa mashindano ya Kombe la Dunia, tarehe 12 Julai 2010, tutarejesha tena matangazo ya Dira ya Dunia.

Utawala BBC Idhaa ya Kiswahili