Shindano la BBC la vijana wabunifu

Global Creative Challenge

Idhaa ya dunia ya BBC imejiunga na mtandao wa vijana wabunifu (YCN) kuzindua shindano na kimataifa la “Global Creative Challenge” au shindano la kimataifa la ubunifu.

Shindano hili linalenga kupata vijana walio na vipaji na talanta kote duniani na kusikia mawazo yao kuhusu wanavyoweza kuleta mabadiliko makubwa katika idhaa ya dunia ya BBC ili kuimarisha uhusiano wao na BBC.

Tunakualika kijana uliye kati ya umri wa miaka 18-34 kutoka kokote duniani, kubuni tangazo la kibiashara ambalo litawalenga vijana kusikiliza zaidi matangazo ya BBC idhaa ya dunia.

Mshindi wa shindano hilo atapa pauni elfu tatu huku watakaoshikilia nafasi ya pili na ya tatu wakipata pauni elfu moja kila mmoja.

Bonyeza hapa kushiriki

Kumbuka:

Wakaazi wa Uingereza hawawezi kushiriki tangazo hili. Majibu yako lazima yawe katika lugha ya kiingereza au ikiwa utafanya kwa lugha ya mama lazima yaambatane na tafsiri kwa kiingireza.

Kwa masharti ya shindano hili tafadhali bonyeza hapa: http://ycn.org/bbccreativechallenge

Shindano litaanza: Tarehe 17 Oktoba 2013

Na kumalizika: Tarehe 2 Desemba, 2013