Pokea taarifa kutoka BBCSwahili kwa simu

Haki miliki ya picha BBC World Service

Ikiwa unataka kupata habari za hivi punde kwenye simu yako ya mkononi ni rahisi sana.

Jisajili na huduma ya ‘BBC Text’ kupata taarifa na video fupi.

Huduma hii inapatikana kwa wateja wa Vodacom, Airtel na Zantel mahali popote Tanzania.

Bonyeza *149*34# kisha uchague BBC halafu uchague Habari au Michezo.

Pata habari za kila wakati kupitia idhaa ya Kiswahili ya BBC.

Huduma hii inafuatia ile ya awali ambapo Idhaa ya Kiswahili ya BBC ilizindua huduma ya wavuti maalum kwa ajili ya simu za mkononi .

Huduma hii mpya inawewezesha watumiaji wa simu za mkononi kusoma taarifa za kila siku moja kwa moja katika simu zao badala ya kutumia kompyuta.

Hata hivyo ieleweke kuwa baadhi ya simu haziwezi kupata huduma hiyo kwa kuwa hazikuundwa maalum kuchukua mawasiliano ya tovuti.

Pia utatakiwa kuwa na uwezo wa kuingia katika internet kadri kampuni yako ya simu inavyokuruhusu, ingawa kuna uwezekano ukatakiwa kulipa gharama kwa matumizi yako.

BBC haitozi fedha kwa wanaotumia huduma ya wavuti kupitia simu za mkononi.

Toleo la wavuti ya BBC Swahili mobile linapatikana kupitia simu za mkononi, PDA na vifaa vingine vya mawasiliano ya mkononi.

Kutakuwa na taarifa za matukio na vile vile soka.

Anzisha browser kwenye simu yako kisha andika:

bbcswahili.com/mobile

Au bonyeza hapa

Ukitaka kuweka kumbukumbu ya kiunganishi cha soka andika

bbcswahili.com/mobile/football

Au bonyeza hapa

Kisha unaweza kuhifadhi ukurasa huu ili uweze kuupata tena kwa urahisi. Endapo huna uhakika kama unaweza kutumia tovuti kupitia simu yako, wasiliana na kampuni yako ya simu.