Amnesty International

 1. Amnesty yamkosoa rais wa Gambia kwa ukandamizaji wa vyombo vya habari

  Adama Barrow aliahidi kuibadilisha nchi wakati anaingia madarakani mnamo 2017

  Shirika la kutetea haki la Amnesty International limemtuhumu Rais wa Gambia Adama Barrow

  ya kushindwa kufuta sheria kandamizi zinazodhibiti uhuru wa vyombo vya habari nchini.

  Shirika hilo linasema limesema nchi hiyo imeredi zaidi ya mashambulio 15 kwa waandishi wa habari katika miaka minne iliyopita, kulingana na ripoti yake iliyotolewa Jumatano.

  Rais Barrow aliingia madarakani mnamo 2017 kwa ahadi ya kampeni ya kurekebisha makosa ya mtangulizi wake, Yahya Jammeh.

  Lakini Amnesty inasema sheria hzi kandamizi zinazodhibiti haki za binadamu, pamoja na uhuru wa kujieleza na kukusanyika kwa amani hazijarekebishwa.

  Baadhi ya taasisi za serikali pamoja na vyombo vya usalama vya kitaifa vinaweza kufuatilia, kukatiza na kuhifadhi mawasiliano kwa madhumuni ya ufuatiliaji bila amri ya mahakama.

  Katika uamuzi wa mwaka 2018, Mahakama ya Haki ya Jumuiya ya Kiuchumi ya Mataifa ya Afrika Magharibi ECOWAS iliamuru mamlaka za Gambia kufanyia marekebisho sheria ya kashfa, fitna na habari za uwongo kulingana na majukumu ya nchi hiyo chini ya sheria za kimataifa za haki za binadamu.

  Hilo halijafanyika kwa sababu bunge la sasa linaelekea kumaliza kipindi chake kuelekea uchaguzi mkuu wa mwezi Disemba.

  Fatou Jallow: Malkia wa urembo anadai 'alibakwa' na rais wa zamani wa Gambia Yahya Jammeh

 2. Amnesty International: Tanzania itoe ushahidi ama imuachie huru Mbowe

  Munira Hussein

  BBC Africa

  Mbowe

  Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty international limesema kuwa serikali ya Tanzania inapaswa kutoa ushahidi wa kesi dhidi ya kiongozi wa chama kikuu cha upinzani Tanzania Freeman Mbowe ama wakishindwa wamuachie huru.

  Taarifa ya Amnesty inakuja huku Mbowe akitarajiwa kupandishwa mahakami mapema kesho siku ya alhamisi.

  Amnesty imesema kuwa ‘’uongozi wa rais Samia Suluhu Hassan umeleta matumaini ya uhuru wa kujieleza, lakini vitendo vya hivi karibuni vya kukamatwa kwa wanachama wa vyama vya upinzani vinatia wasiwasi kama uhuru huu utaendelea ama hali itarudi kama ilivyokua awali’’.

  Polisi nchini Tanzania imesisitiza kuwa Mbowe amefanya makosa na ushahidi upo.

  ‘’Wafuasi wa CHADEMA wanadhani Mbowe ameonewa na kuwa yeye ni malaika hawezi kufanya makosa, lakini kesi hii iko mahakami hivyo tuachie mahakama ifanye kazi yake na ukweli utajulikana’’ alisema IGP Simon Sirro mkuu wa polisi Tanzania.

  Mbowe alikamatwa wiki mbili zilizopita na baadae kusomewa mashtaka ikiwemo ugaidi.

  Freeman Mbowe: LHRC, Amnesty International wataka Mbowe aachiwe na uhuru wa kisiasa uheshemiwe Tanzania

 3. Anyongwa kwa uhalifu alioufanya utotoni

  Mustafa al-Darwish alikamatwa mnamo 2015 na kushtakiwa kwa kujaribu kutekeleza uasi
  Image caption: Mustafa al-Darwish alikamatwa mnamo 2015 na kushtakiwa kwa kujaribu kutekeleza uasi

  Saudi Arabia imemnyonga mwanamume mmoja kwa uhalifu ambao makundi ya kutete haki yanasema alifanya akiwa na miaka 17,licha ya hakikisho la ufalme kwamba umekomesha adhabu ya kifo kwa watoto.

  Mustafa Hashem al-Darwish alikamatwa mnamo mwaka 2015 kwa makosa yanayohusiana na maandamano.

  Mamlaka nchini Saudia zinasema alishtakiwa kwa kuunda seli ya kigaidi na kujaribu kufanya uasi kwa kutumia silaha.

  Lakini makundi ya kutetea haki yalikuwa yametoa wito wa kutotekelezwa kwa adhabu ya kifo dhidi yake, yakisema kesi yake haikuwa ya haki.

  Mashirika ya kutetea haki ya Amnesty International na Reprieve, ambayo yanapinga adhabu ya kifo, yanasema al -Darwish ambaye alikuwa na umri wa miaka 26, alikukiri makosa ambayo baada ya kudai wa kuteswa. Mamlaka ya Saudi Arabia haijatoa tamko lolote hadharani juu ya tuhuma hizo.

  Kulingana na shiririka la habari la Reuters, mashataka dhidi ya al-Darwish yalijumuisha "kutaka kuvuruga usalama kupitia maandamano" na "kuzua ugomvi".

  Ushahidi dhidi yake ulijumuisha picha "ya kukera kwa vikosi vya usalama", na ushiriki wake katika mikusanyiko zaidi ya 10 ya "ghasia" mnamo mwaka 2011 na 2012.

 4. Rais wa Msumbiji awafuta kazi wakuu wa majeshi

  Rais Filipe Nyusi hakutoa sababu ya kuwafuta kazi
  Image caption: Rais Filipe Nyusi hakutoa sababu ya kuwafuta kazi

  Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi amewafukuza kazi wakuu wa jeshi la ardhini na angani wakati nchi inapokabiliana na wanamgambo wa Islamic States kaskazini mwa nchi hiyo na uasi wa wanamgambo wanaohusishwa na chama kikuu cha upinzani.

  Katika taarifa iliyotolewa usiku Alhamisi, rais hakutoa sababu ya kumfuta kazi Ezequiel Isac Muianga, mkuu wa jeshi la ardhini, na Messias André Niposso, mkuu wa jeshi la anga.

  Rais pia amemfukuza kazi kamanda na naibu kamanda wa chuo cha mafunzo ya kijeshi cha Marechal Samora Macheya.

  Naibu kamanda wa Taasisi ya mafunzo ya juu ya masuala ya ulinzi pia alifukuzwa kazi.

  Msumbuji imekuwa ikipambana na uasi katika mkoa wenye utajiri wa madini wa Cabo Delgado tangu Oktoba 2017.

  Watu nusu milioni wamekimbia makazi yao mwaka jana pekee.

  Kundi la al-Ansar al-Sunna, ambalo linajulikana na wenyeji kama al-Shabab, limehusika na makumi ya mashambulio ya kigaidi ambayo yanakaidiriwa kuuwa mamia ya watu.

  Shirika la kutete haki la Amnesty International mwezi huu lilichapisha ripoti inayolaumu majeshi ya Msumbiji wajenzi wa majeshi wa kibinafsi na waasi wanaohudumu katika mkoa wa Cabo Delgado kwa kutekeleza uhalifu wa kivita.

  Soma zaidi: