Afrika Magharibi

 1. Wanajeshi nchini Guinea wamzuia kwa muda waziri wa zamani

  Wanajeshi walichukua madaraka nchini Guinea mnamo 5 Septemba
  Image caption: Wanajeshi walichukua madaraka nchini Guinea mnamo 5 Septemba

  Utawala mpya wa kijeshi nchini Guineaumemkamata waziri wa zamani siku ya Jumapili na kupekua nyumba yake kabla ya kumuachia saa kadhaa baadye.

  Wanaume waliokuwa wamevalia sara walivamia nyumba ya Tibou Kamara katika mji mkuu wa Conakry wakati wa asubuhi, kumkamata na kumpeleka mahali pasipojulikana. Aliachiliwa huru mwendo wa mchana.

  Vitu kadhaa ikiwemo simu zilichukuliwakutoka kwake.

  Kukamatwa kwake kunaashiria kulithibitishwa na Kamati ya kitaifa ya maridhiano na (CNRD) Pamoja na timu yake.

  Viongozi wa mapinduzi wanamtuhumu kwa kukiuka ahadi ya kutokua na upande wowote katika usimamizi wa jeshi.

  Bw. Kamara alikuwa waziri wa viwanda na mshauri war ais wa zamani Alpha Condé, ambaye alifurushwa madarakani mapema mwezi huu.

  Maelezo zaidi:

  Mapinduzi Guinea:Mfahamu Kanali Mamady Doumbouya, kiongozi wa mapinduzi nchini Guinea

  Je mapinduzi ya kijeshi yanaongezeka Afrika?

 2. Chuo cha kupambana na ugaidi chafunguliwa Ivory Coast

  Wanajeshi

  Chuo cha kimataifa cha kupambana na ugaidi kimefunguliwa karibu na mji wa Abidjan huko Ivory Coast.

  Chuo hicho kinachofahamika kama AILCT, kilifadhiliwa na Ufaransa na Muungano wa Ulaya ,EU, na nchini zingine kinalenga kusaidia eneo hilo kukabiliana na wanamgambo wa kijihadi.

  Hafla ya ufunguzi wake iliongozwa na Waziri Mkuu wa Ivory Coast, Waziri wa Ulinzi wa nchi hiyo na Waziri wa Mambo ya nje wa Ufaransa.

  Chuo hicho ambacho kimejengwa eneo lenye minazi mingi karibu kilo mita 80 kutoka mjini Abidjan, kitatumika kutoa mafunzo ya kijeshi.

  Wanajeshi

  Tayari dola milioni 27 sawa na (euro milioni 20) zimewekezwa katika mradi huo lakini fedha zaidi zinahitajika kuukamilisha ndani ya miaka miwili ijayo.

  Malengo matatu muhimu ni:

  • Kufundisha vikosi maalum vya majeshi katika mkoa huo.
  • Kuwapa mafunzo dhidi ya ugaidi maafisa, kama mahakimu, maafisa wa forodha na wahasibu.AILCT inataka kuunda mitandao ya wataalamu wanaojuana na kufanya kazi pamoja katika mipaka.
  • Kuunda kituo cha kimkakati cha kusoma.
  Tayari dola milioni 27 sawa na (euro milioni 20) zimewekezwa katika mradi huo
  Image caption: Tayari dola milioni 27 sawa na (euro milioni 20) zimewekezwa katika mradi huo

  Uzinduzi wake unakuja siku chache baada ya Ufaransa kutangaza kwamba inakamilisha Operesheni ya Barkhane katika eneo la Sahel, ambalo linakabiliwa ukame kusini mwa Jangwa la Sahara.

  Eneo hilo linajumuisha Mali, Chad, Niger, Burkina Faso na Mauritania.

 3. Mwanamke ajifungua watoto tisa Mali

  Watoto

  Mwanamke mmoja nchini Mali amejifungua watoto tisa katika hali ambayo sio ya kawaida.

  Halima Cisse, 25, alijifungua watoto wa kike watano na wavulana wanne katika hospitali ya Morocco siku ya Jumanne ambako alikuwa amelazwa, Waziri wa Mali Fanta Siby alisema katika taarifa. Alijifungua kupitia njia ya upasuaji.

  Bi Cisse amekuwa akitarajia kijifungua watoto saba kulingana na uchunguzi wa skani ya tumbo aliyofanyiwa nchini Mali na Morocco lakini skani hiyo haikugundua amebeba watoto wengine wawili.

  Siku ya Jumanne, Dkt Siby alisema watoto hao na mama yao “wanaendelea vyema”. Wanatarajiwa kurejea nyumbani wiki chache zijazo.

  Aliwapongeza madaktari waliomhudumia Mali na Morocco, “ambao ujuzi wao ni chanzo cha matokeo mema ya ujauzito huu".

  Mimba ya Bi Cisse imeshangaza taifa hilo la Afrika Magharibi na imewavutia baadhi ya wakuu wa nchi hiyo – huku baadhi yao wakisafiri had Morocco alipohitaji utunzi wa kitaalamu, shirika la habari la Reuters liliripoti.

  Msemaji wa wizara ya afya ya Morocco, Rachid Koudhari, ameliambia shirika la habari ya AFP kwamba hakujua uzazi wa aina hiyo hutokea nchini humo.