Ulaya

 1. Alexandre Lacazette

  Mchezaji wa Arsenal Alexandre Lacazette amesema kuwa mawakala wake wanafikiria wapi atakwenda huku kandarasi ya mshambuliaji huyo Mfaransa mwenye umri wa miaka 30 ikikamilika msimu wa joto. (Telefoot via Athletic)

  Soma Zaidi
  next
 2. Erling Braut Haaland iwapo ataondoka Borussia Dortmund

  Klabu anayotaka kuhamia mshambuliaji wa Norway Erling Braut Haaland iwapo ataondoka Borussia Dortmund mwaka ujao Real Madrid, inagawa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 bado hajafanya maamuzi kuhusu hali yake ya baadaye . (Goal)

  Soma Zaidi
  next
 3. Aina mpya ya kirusi cha Corona yatua Ulaya

  Kisa cha kwanza cha maambukizi charipotiwa Ubelgiji
  Image caption: Kisa cha kwanza cha maambukizi charipotiwa Ubelgiji

  Ubelgiji imeripoti kisa cha kwanza cha aina mpya ya kirusi cha Corona barani Ulaya ambacho kwanza kigunduliwa nchini Afrika Kusini - huku Shirika la Afya Duniani likifanya mkutano maalum kuangazia umuhimu wake.

  Wataalamu mjini Geneva wataamua ikiwa kirusi hicho kinahitaji kutambuliwa kama ni hatari.

  WHO inasema itatoa mwongozo mpya baada ya mazungumzo lakini imeonya kwamba itachukua wiki kadhaa kubaini ikiwe kirusi hicho kivyoweza kuambukizwa na ikiwa chanjo itasalia kuwa na ufanisi dhidi yake.

  Rais wa Tume ya Ulaya, Ursula von der Leyen,iliwakumbusha watengenezaji kwamba kandarasi zao na EU inamaanisha lazima wabadili chanjo zao mara moja kwa kuzingatia kirusi hiki kipya.

  Pia alisema kuwa safari zote za anga kwenda nchi zilizo na kirusi kipya cha corona zinapaswa kusitishwa.

  Soma zaidi:

  B.1.1.529 : Fahamu aina mpya ya kirusi hatari cha corona kilichogunduliwa