Facebook

 1. Biashara za Afrika zinahesabu hasara baada ya kukatika kwa huduma za Facebook

  After the outage took place, people turned to other social media platforms like Twitter to connect

  Wamiliki wa biashara wa Afrika wanaotegemea mitandao ya kijamii kuendesha mauzo yao wanakadiria hasara waliyopata baada ya huduma za mitandao ya kijamii ya Facebook, WhatsApp, na Instagram kupotea kwa saa sita.

  Wataalamu wanasema huduma za biashara za kimtandao, ambazo zimepata ukuaji mkubwa barani Afrika wakati wa janga la corona ziliathiriwa vibaya.

  "Walioathiriwa zaidi ni wale wanaojitegemea na wenye biashara ndogo, ikilinganishwa na wale wenye bishara kubwa ambazo zina tovuti," Mtaalamu wa mauzo ya kidijitali Karen Wambugu aliambia BBC.

  Aliongeza: "Wakati mitandao mikubwa ya kijamii kama vile Facebook na Instagram hazifanyi kazi, wenye biashara ndogo ndogo hawawezi kuendesha mauzo yao kwa sababu hawana njia nyingine mbadala.”

  Mama mfanyabishara wa Ghana ambaye anaendesha biashara yake ya chakula mtandaoni na pia kuuza vyakula vyake katika hoteli iliyopo mji mkuu wa Accra anasema huduma hizo zilikatika wakati wa shughuli nyingi za chakula cha mchana.

  "Asilimia 80 ya mauzo yetu hutokana na wateja wanaoagiza vyakula kupitia mtandaoni. Ni wateja wachache wanaoweza kufika hotelini wakati kuna msongamano wa magari kuja kula " Kafui Adza aliambia BBC.

  Huduma za Facebook, Whatsapp na Instagram zarejea baada ya kukatika

  Fahamu simu na Kompyuta zitakazoathirika na kuzimwa kwa mtandao duniani

 2. Facebook yabuni mbinu mpya ya usalama kwa watumiaji wa Afghanistan

  Wanawake na watoto wa kikeAfghanistan

  Facebook imefanya iwe vigumu kutafuta akaunti ya Wafhanistan miongoni mwa vipengee vingine vya usalama, huku kukiwa na hofu kwamba Taliban wanatumia mitandao ya kijamii kufuatilia wapinzani wao.

  Nathaniel Gleicher, mkuu wa sera ya usalama wa kampuni hiyo kubwa ya teknolojia, aliandika ujumbe kwenye Twitter kusema kuwa Facebook pia "ilizindua kifaa kimoja cha kubofya kwa watu nchini Afghanistan kufunga akaunti zao haraka".

  "Wakati wasifu wao umefungwa, watu ambao sio marafiki zao hawawezi kupakua au kushirikisha picha ya wasifu wao, au kuona machapisho yao mtandaoni."

  Katika mtandao wa Instagram, ambao unamilikiwa na Facebook, kampuni hiyo "kutoa arifu za pop-up nchini Afghanistan na hatua maalum ya jinsi ya kulinda akaunti yako".

 3. Facebook yathibitisha kupiga marufuku maudhui yenye kujihusisha na Taliban

  Kampuni zinazoendeleza teknolojia zakabiliwa na changamoto ya namna ya kushughulikia maudhui ya Taliban
  Image caption: Kampuni zinazoendeleza teknolojia zakabiliwa na changamoto ya namna ya kushughulikia maudhui ya Taliban

  Mtandao wa kijamii wa Facebook inachukulia Taliban kama kundi la kigaidi na hivyobasi, inapiga marufuku maudhui yote yanayounga mkono Taliban katika majukwaa yao.

  Kampuni ya Facebook imesema timu ya wataalam wa Afghan inafuatilia na kuondoa maudhui yote yenye kufungamana na kundi hilo.

  Facebook imegusia kwamba sera hiyo inatumika kwa majukwaa mengine yote ya mitandao yao ikiwemo Instagram and WhatsApp.

  Hata hivyo, kuna taarifa kwamba Taliban inatumia jukwaa la mawasiliano la Whatsapp kuwasiliana.

  Facebook imeiambia BBC kwamba itachukua hatua ikiwa itabaini akaunti kwenye programu za simu yenye kijihusisha na kundi hilo.

  Majukwaa pinzani ya mitandao ya kijamii kama vile Twitter na Youtube pia nayo yameanza kufuatilia kwa karibu namna ya kushughulikia maudhui ya kundi la Taliban.

 4. Trump aunga mkono hatua ya Nigeria kuifungia Twitter

  Bw. Trump alifungiwa na Twitter na Facebook mwezi Januari
  Image caption: Bw. Trump alifungiwa na Twitter na Facebook mwezi Januari

  Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump amepingeza hatu ya Nigeria kuipiga marufuku Twitter - na kutoa wito nchi zingine zifuate mkondo huo.

  "Pongezi kwa nchi ya Nigeria, kwa kuifungia Twitter kwasababu ya kumpiga marufuki Rais wao," alisema katika taarifa.

  Rais huyo wa zamani ametoa wito kwa nchi zingine kufuata mkondo na kuzifungia Facebook na Twitter " kwa kudhibiti uhuru wa kujieleza".

  Bw. Trump alipigwa marufuku na katika mitandao ya kijamii ya Twitter na Facebook mwezi Januari kwa tuhuma za kuchapisha ujumbe wa kuchochea uvamizi wa bunge la Marekani. Watu watano walifariki kutokana na kisa hicho.

  Twitter

  Katika taarifa yake siku ya Jumatatu, alijita kwanini hakuzifungia Facebook na Twitter wakati wa Urais wake.

  "Wao ni nani kuamua kizuri na kibaya ikiwa wao wenyewe ni wabaya? Nadhani ningeliwapiga marufuku nilipokuwa Rais. Lakini [Mwanzilishi wa Facebook Mark] Zuckerberg aliendelea kunipigia simu na kuja Ikulu ya White House kwa chakula cha jioni akiniambia jinsi nilivyokua mzuri," alisema.

  Wiki iliyopita Nigeria ilifunga akaunti za Twitter nchini humo kwa madai kwamba "shughuli za mtandao huo zinahujumu uwepo wa Nigeria kama taifa lililoundwa shirikisho".

  Hatua hiyo ilichukuliwa siku kadhaa baada ya ujumbe wa Rais Muhammadu Buhari kuondolewa kwa kukiuka kanuni za mtandao wa huo wa kijamii.

  Ilizua ghadhabu miongoni mwa Wanaigeria na mataifa ya magharibi ambayo yalisema hatua hiyo inaminya uhuru wa kidemokrasi.

  Pande zote mbili zimesema zinajadiliana kuhusu namna ya kusuluhishi

  Soma zaidi:

 5. Facebook yazindua huduma ya uchangiaji damu nchini Tanzania

  Facebook

  Mtandao wa kijamii wa Facebook kwa ushirikianao na Huduma ya Kitaifa ya uchangiaji wa Damu nchini Tanzania (NBTS), imezindua huduma ya uchangiaji damu.

  Kulingana na Gazeti la The Citizen, mpango huo utasaidia kuinganisha NBTS na vituo saba vya uchangiaji damu nchini Tanzania.

  Katika taarifa iliyotolewa na kampuni hiyo siku ya Jumanne, na meneja wa mawasiliano wa kanda ya Afrika Mashariki Janet Kemboi mpango huo utawawezesha watu kuwashirikisha marafiki na jamaa zao kujisajili ili wapate taarifa kuhusu utoaji damu.

  Tangu ilipozinduliwa mwaka 2004, NBTS imeondokana na mfumo wa kutegemea utoaji damu kupitia familia na kugeukia mfumo ambao unahamasisha watu kutoa damu kwa hiari.

  Soma zaidi:

 6. Facebook kuilipa News Corp kwa kushirikisha habari zake Australia

  Shirika la Habari la Rupert Murdoch kulipwa Facebook huko Australia
  Image caption: Shirika la Habari la Rupert Murdoch kulipwa Facebook huko Australia

  Facebook imekubali kulilipa shirika la habari la News Corp linalomilikiwa na Rupert Murdoch nchini Australia kwa kutumia taarifa zake.

  Mkataba huo umefikiwa wiki kadhaa baada ya Australia kupitisha sheria tata inayolenga kuzishurutisha kampuni za teknolojia kulipia maudhui ya habari.

  News Corp haijasema thamani ya mkataba huo wa miaka mitatu nchini Australia. Mwezi uliopita , ilifikia mkataba na kampuni ya Google.

  Himaya ya Bw.Murdoch ya uwasilishaji habari ilianza na uchapishaji wa magazeti nchini Australia. Mkataba huo unajumuisha maudhui yote ya habari kutoka News Corp nchini humo – ambao unakadiriwa kugharimu kiasi kikubwa cha fedha.

  News Corp inashikilia karibu asilimia 70 ya usambazaji wa magazeti nchini Australia ikiwa na machapisho yake katika magazeti ya The Daily Telegraph na The Herald Sun miongoni mwa zingine. Pia inamiliki tovutu ya news.com.au.