Haki za Kibinadamu

 1. Msako mkali dhidi ya jamii ya Tigray unaendelea Ethiopia- UN

  Demonstrators have been marching around the world to highlight the plight of Tigrayans

  Ripoti ya shirika la Umoja wa Mataifa la kutetea haki za binadamu imesema takriban watu 1,000, wengi wao wakiwa kutoka kabila la Tigray, wamekamatwa tangu serikali ilipotangaza hali ya hatari tarehe 2 Novemba.

  Chini ya hali hiyo ya dharura ya miezi sita, serikali ina mamlaka makubwa ya kuwakamata watu, kuwaweka kizuizini washukiwa bila kuwafungulia mashtaka, na kufanya upekuzi nyumbani bila vibali.

  Kamishna Mkuu wa Haki za Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa alisema "takriban watu 1,000 wanaaminika kuzuiliwa kwa muda wa wiki moja au zaidi - huku ripoti zingine zikiweka idadi hiyo juu zaidi".

  Taarifa hiyo ilisema mazingira wanayozuiliwa ni mbaya na wafungwa wengi wanashikiliwa katika vituo vya polisi vilivyo na watu wengi.

  Wafanyakazi kumi wa ndani wa Umoja wa Mataifa ambao walikamatwa tarehe 9 Novemba bado wanazuiliwa.

  "Wengi wa wale wanaozuiliwa wanaripotiwa kuwa watu wa asili ya Tigray, wanaokamatwa mara kwa mara kwa tuhuma za kuhusishwa au kuunga mkono Tigray People's Liberation Front (TPLF)," UN ilisema.

  Katika siku za nyuma, polisi walisema kukamatwa huko hakukuwa na msukumo wa kikabila bali kulilenga wafuasi wa TPLF, ambayo imekuwa ikipambana na serikali kuu tangu mwaka uliopita na sasa wanatishia kuelekea mji mkuu.

  Mzozo wa Tigray, Ethiopia: Kwa nini ulimwengu mzima una wasiwasi na mzozo huu?

  Vita vya Ethiopia mwaka mmoja baadaye: Jinsi ya kumaliza mahangaiko

 2. Jeshi la Nigeria 'liliwapiga risasi na kuwaua waandamanaji wa #EndSars': ripoti

  Nchi ilitikiswa na maandamano ya kupinga ukatili wa polisi kwa wiki mbili Oktoba iliyopita
  Image caption: Nchi ilitikiswa na maandamano ya kupinga ukatili wa polisi kwa wiki mbili Oktoba iliyopita

  Jopo la uchunguzi, lililoundwa na mamlaka nchini Nigeria kuchunguza tukio la waandamanaji kupigwa risasi mjini Lagos mnamo Oktoba 2020, limewasilisha ripoti juu ya kile kilichokea usiku huo.

  Toleo lililovuja la ripoti hiyo, iliyokabidhiwa kwa gavana wa jimbo hilo leo, inadai kuwa wanajeshi wa Nigeria waliwapiga risasi kimakusudi waandamanaji waliokuwa wakipinga ukatili wa polisi kwenye barabara ya Lekki Tollgate, kisha wakajaribu kuificha.

  Waandamanaji hao walikuwa wakiendesha kampeni dhidi ya ukatili wa polisi.

  Pia ilibaini kuwa baada ya jeshi hilo kurudi nyuma, askari polisi waliendelea na vurugu na kujaribu kufanya usafi katika eneo la tukio na kuweka miili kwenye lori na kutoa risasi.

  Baadhi ya matokeo yanalingana na ripoti za awali za Amnesty International, pamoja na vyombo vya habari vya ndani na kimataifa.

  Gavana wa Jimbo la Lagos Babajide Sanwo-Olu, ambaye alianzisha jopo hilo, ameahidi "kutilia maanani" matokeo yake.

 3. Video content

  Video caption: Tutawahi kupata haki?-Raia wa Gambia

  Ni miaka minne sasa tangu Yahya Jammeh ,kiongozi aliyetawala Gambia kwa miaka 22 kukimbia nchi yake.

 4. Mashambulio ya angani yagonga mji mkuu wa Tigray - waasi na mashahidi

  Mashambulio ya angani yamefanywa dhidi ya mji mkuu wa jimbo la Tigray, Mekelle, kaskazini mwa Ethiopia, waasi na wakazi wameambia BBC.

  Vikosi vya muungano vimekua vikipikabiliana na wapiganaji wa Tigray People's Liberation Front (TPLF) kaskazini mwa nchi kwa karibu mwaka mmoja.

  Kindeya Geberehiwot, mwanachama wakamati kuu ya TPLF, ameambia BBC Tigrinya kwamba mashambulio ya Jumatatu asubuhi yalilenga sehemu mbili za mji huo.

  Shambulio la kwanza, lilitokea viungani mwa mji wa Mekelle, karibu saa 09:30 (06:30 GMT) ambapo raia watatu waliuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa, Bw. Kindeya alisema.

  Shambulio la pili lilitokea katika soko lenye shughuli nyingi ambapo makumi ya watu walijeruhiwa, aliongeza kusuma.

  Wakazi pia wameambia BBC kuhusu mashambulio hayo huku watumiaji wa mitandao ya kijamii wakishirikisha picha zinazoonesha uharibifu uliosababishwa.

  Ushahidi unaoonesha jinsi jeshi la Ethiopia lilivyofanya mauaji Tigray

  Je janga la njaa la Tigray ni msiba wa kujitakia?

  Uchumi wa Ethiopia waathiriwa na mzozo wa Tigray