Unyanyasaji wa Watoto

 1. Video content

  Video caption: Hatari ya mafundisho potofu kuhusu mahusino ya ngono mitandaoni

  Mafundisho kuhusu mahusiano na ngono shuleni huibua mjadala ,lakini daktari mmoja huko Wales Uingereza anasema Watoto kupitia video za ponografia wakupotoshwa kuhusu ngono.

 2. Zaidi ya watoto 6000 walikabiliwa na unyanyasaji Tanzania katika kipindi cha miezi tisa mwaka huu

  N

  Naibu waziri wa mambo ya ndani wa nchini Tanzania Khamis Chilo amelifahamisha Bunge la nchi hiyo kwamba jumla ya watoto 6,168 wa Tanzania walikabiliwa na aina tofauti za unyanyasaji kati ya Januari na Septemba mwaka 2021.

  Bw. Chiko alikuwa akijibu swali la Mbunge wa viti maalum Bi Esther Matiko siku ya Ijumaa ambaye alitaka kujua idadi ya watoto na waathirika wa ghasia nchini Tanzania katika kipindi hicho.

  Katika jibu lake, Bw Chilo alisema kati ya 6168 walioathirika wanawake walikuwa 5287 na wanaume wakiwa 881 akiongezea kwamba 3524 kati yao walibakwa huku 637 wakilawitiwa

  Bw. Chiko alisema karibu washukiwa 3,800 wamekamatwa na kesi 2,368 zinaendelea katika mahakama tofauti nchini na hukumu za kesi 88 zimetolewa.

 3. Video content

  Video caption: Familia yauza mtoto kwa dola 500 kuepuka njaa

  Afghanistan inakabiliwa na mzozo mkubwa zaidi wa kibinadamu duniani, huku nchi hiyo ikishuhudia kuzorota kwa kasi kwa hali nchini humo tangu wapiganaji wa Taliban wachukue mamlaka

 4. Anne Ngugi

  BBC Swahili

  Cecilia

  Kubakwa ni tukio ambalo Mchungaji Cecilia Muthoni Ssewagaba, hatawahi kulisahau maishani mwake. Lakini tukio hili ambalo alilipitia utotoni yameachia kofu moyoni mwake, lakini bila shaka halikumkatisha tamaa ya kusonga mbele na maisha na kuwasaidia wengine waliopitia masaibu kama yake.

  Soma Zaidi
  next
 5. R. Kelly: Uteuzi wa wanasheria wa kusikiliza kesi ya dhulma za kingono dhidi ya msanii R.Kelly waanza

  R.Kelly

  Msanii wa R&B R. Kelly amefika mahakamani mjini New York,huku uteuzi wa wanasheria katika kesi ya dhulma za kingono dhidi yake ukianza.

  Inajiri zaidi ya miaka miwili baada ya msanii huyo kushtakiwa kwa unyanyasaji wa wanawake na wasichana wadogo kwa karibu miongo miwili.

  Mwimbaji huyo aliyeshinda Tuzo ya Grammy anakabiliwa na mashtaka ya unyanasaji wa kingono dhidi ya watoto, ujambazi na rushwa. Amekanusha mashtaka

  Wanasheria wanaotarajiwa kuongoza kesi hiyo wanahojiwa ikiwa wanaweza kuwa na mawazo huru katika kesi hiyo.

  Baada ya majaji kuteuliwa, kesi inatarajiwa kuanza Agost18 na huenda ikaendelea kwa wiki kadhaa.Msanii huyo mwenye umri wa miaka 54 akipatikana na hatia huenda akafungwa jela kwa miongo kadhaa.

  Kesi dhidi yake pia imewasilishwa katika mahakama ya Illinois na Minnesota.

  R Kelly
  Image caption: R. Kelly (anayeonekana hapa mwaka 2019) ianakabiliwa na mashataka ya kuwanyanyasa watoto kingono na rushwa

  Alipoulizwa jinsi anavyojihisi,wakili wa Kelly,Deveraux Cannick aliliambia shirika la Habari la AFP: "Ni sawa na Jumatatu nyingine."

  Kelly, mmoja wa wasanii nyota wa miondoko ya R&B miaka ya1990, amekuwa akizuiliwa tangu Julai mwaka 2019.

  Kesi ya New Yorki inamtuhumu mwimbaji huyo–ambaye jina lake halisi ni Robert Kelly –kwa kuongoza kundi la mameneja , walinzi wa kibinafsi na wengine ambao waliwaanda wanawake na wasichana kwa ajili ya kufanya ngono.

  Waendesha mashtaka wanasema wahasiriwa waliteuliwa katika matamasha na maeneo mengine.

  Soma zaidi:

 6. Data inaashiria wasichana ndio walio katika hatari zaidi ya kunyanyaswa

  Unyanyasaji dhidi ya mtoto unachukuliwa kuwa matendo mabaya au nia ya kumdhuru mtoto ama kisaikolojia, kihisia, kingono au kimwili ama kutelekezwa na anayemtunza hadi kufikia miaka anayochukuliwa kuwa mtu mzima kwa nchi nyingi ikiwa ni miaka 18.

  Soma Zaidi
  next