Usafiri wa Ndege

 1. An aeroplane lands in a beautiful sunset

  Mtu mmoja huko kusini mwa Uingereza , hivi karibuni alimwagikiwa na vinyesi vilivyodondoka kwenye ndege iliyokuwa inapia karibu juu yake ikielekea kutua. Je hili ni hatari? Na je hiii ni hatari kiasi gani, na kuna uwezekano gani wa anayefuata kudondokewa na kinyesi akawa wewe?

  Soma Zaidi
  next
 2. Ndege yamwagia mtu majitaka akiwa kwenye bustani yake

  Ndege ilidondosha maji taka ya kibinadamu kote kwa mtu wakati alikuwa katika bustani

  Mwanamume mmoja na mfanyakazi wake walimwagiliwa maji taka kutoka kwa ndege, jopo la uchunguzi lafahamishwa nchini Uingereza.

  Akizungumza katika baraza la Royal Borough ya Windsor na shurika la ndege la Maidenhead, kansela Karen Davies alisema "amegutushwa" kusikia kisa hicho.

  Alielezea jinsi "yeye’’ na bustani lote "lilivyofunikwa" kwa uchafu huo.

  Kisa hicho kilitokea mjini Windsor kati kati ya -Julai.

  Vyoo vya ndege huhifadhi maji taka katika sehemu maalum, lakini yaliyomo kawaida hutupwa mara tu ndege inapotua.

  Diwani wa Clewer Mashariki aliambia kikao hicho kuwa alifahamishwa kuhusu kisa hicho cha "kuogofya" na mkazi wa eneo bunge lake, kulingana na Huduma ya Kuripoti Demokrasia ya Mitaa.

  Diwani wa parokia ya Whitfield, Geoff Paxton, ambaye amefanya kazi katika viwanja vya ndege kwa miaka 40, alitaja tukio hilo kuwa "nadra sana" na ambalo halijawahi kutokea kwa muda mrefu.

  BBC imewasiliana na Mamlaka ya Usafiri wa Angani ili kupata tamko lake.

 3. 铁臂阿童木机器人 2018年东京世界机器人峰会上以卡通人物阿童木为原型的机器人

  Utafiti unaoendelea unaonyesha kuwa hata maafisa wa polisi waliopewa mafunzo huwa wanajaribu kumuelewa muongo kupitia lugha yake ya mwili na muonekano wa uso wake, na wanasema mara nyingi kuelewa mafanikio ya njia hii huwa ni bahati.

  Soma Zaidi
  next
 4. RwandaAir yasitisha kwa muda safari zake Uganda -kunani?

  Dinah Gahamanyi

  BBC Swahili

  RwandaAir

  Shirika la ndege la Rwanda, RwandAir imetangaza kuwa imesitisha kwa muda safari zake za ndege za kwenda na kutoka kwenye uwanja wa kimataifa wa ndege wa Uganda wa Entebbe mara moja.

  “Kutokana na kuongezeka kwa visa vya Covid-19 nchini Uganda, RwandAir inatangaza kusitishwa kwa safari zake za ndege za kuelekea na kutoka Entebbe kuanzia tarehe 10 Juni 2021, hadi tangazo lingine litakapotolewa,” Taarifa ya shirika hilo la ndege ya Rwanda lilisema.

  View more on twitter

  Liliongeza kuwa : “RwandAir inaomba radhi kwa usumbufu uliosababishwa na hatua hiyo.”

  Shirika hilo lilisema kuwa wateja waliothiriwa ‘’wanaweza kupanga upya safari na kusafiri baadaye, pale safari hizo zitakaporejeshwa tena–au waombe kurejeshewa pesa zao za nauli.”

  Uganda imeshuhudia ongezeko la idadi ya watu walioambukizwa virusi vya corona, jambo lililowalazimisha maafisa kuweka sheria inayowataka watu kupunguza shughuli na matembezi yasiyo ya lazima kwa muda wawiki sita.