Somalia

 1. Marekani yafanya shambulio la kwanza la angani chini ya Biden Somalia

  Biden

  Marekani imefanya shambulio la kwanza la angani dhidi ya wanamgambo wa al-Shabab mjini Galkayo, kaskazini mwa Somalia, Jumanne.

  Hili ni shambulio la kwanza la angani tangu Rais Joe Biden kuingia madarakani.

  Msemaji wa wizara ya ulinzi ya Marekani Cindi Kingal amesema Marekani ilikuwa ikiyasaidia majeshi ya Somalia ambayo yalikuwa yakivamiwa na wanamgambo.

  Ripoti za awali zinasema kuwa raia walijeruhiwa.

  Rais Biden alidhibiti mashambulio ya angani kwa kutumia ndege zisizo na rubani nje ya Marekani.

  Mtangulizi wake Donald Trump aliongeza mashambulio ya angani nchini Somalia wakati wa utawala wake.

  Kabla tu ya kuondoka ofisini, aliamuru vikosi maalum vya wanajeshi 700 vilivyopelekwa Somalia viondolewe.

  Somalia imekuwa ikikabiliwa na ukosefu wa usalama kutokana na mashambulio yanayofanywa na wanamgambo wa al-Shabab.

 2. Mlipuko wa Somalia waua zaidi ya wanajeshi 10

  Wanawake wanalia

  Zaidi ya wanajeshi 10 wameuawa baada ya mlipuaji wa kujitoa mhanga kujilipua katika kambi moja ya kijeshi iliyopo mji mkuu wa Somalia, Mogadishu, ripoti zinasema.

  Mwanahabari aliyekua katika eneo la tukio amesema mlipuaji huyo alijidai kuwa mwanajeshi, na kuingia katika kambi ya jeshi ya Wadajir na kuanza kulipua vilipuzi alivyokuwa amejifunga kiunoni, wakati wa mafunzo ya asubuhi.

  Watu wengine 10 pia wamejeruhiwa.

 3. Ripoti ya UN imesema wanajeshi wa Somalia walipigana Tigray huku Ethiopia ikishtumiwa kwa mauaji ya kiholela

  Mamilioni ya watu waliathiriwa katika mzozo wa Tigray
  Image caption: Mamilioni ya watu waliathiriwa katika mzozo wa Tigray

  Ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa inadai kwamba wanajeshi kutoka Somalia walipigana kwa ushirikiano na Waeritrea katika eneo linalokumbwa na mzozo la Ethiopia-Tigray.

  Ripoti ya Mwakilishi Maalum wa Umoja wa mataifa Mohamed Abdelsalan Babiker ilisema wanajeshi wa Somalia walipigana katika mstari wa mbele huko Tigray.

  "Mbali na ripoti za kuhusika kwa wanajeshi wa Eritrea katika mzozo wa Tigray, mwakilishi huyo Maalum pia alipokea habari na ripoti kwamba wanajeshi wa Somalia walihamishwa kutoka kambi za mafunzo ya kijeshi huko Eritrea hadi mstari wa mbele huko Tigray, ambapo waliandamana na wanajeshi wa Eritrea wakati wakivuka mpaka wa Ethiopia, "inabainisha ripoti hiyo.

  Ilisema kwamba wapiganaji wa Somalia waliripotiwa kuwapo katika mji mtakatifu wa Ethiopia wa Aksum. Serikali ya Somalia imekanusha kuhusika katika mzozo wa Tigray.

  Eritrea haikushirikiana katika uchunguzi wa UN ambao ulizingatia zaidi hali ya haki za binadamu huko Eritrea.

  Mwakilishi wa wa UN alisema ripoti yake ilitokana na uchunguzi na habari kutoka vyanzo tofauti.

  Mnamo Februari, Shirika la Amnesty International lilishtumu wanajeshi wa Eritrea huko Aksum kwa kuua mamia ya watu haswa zaidi ya siku mbili mnamo Novemba ambayo inaweza kuwa ni uhalifu dhidi ya binadamu – madai ambayo mamlaka ya Eritrea ilitupilia mbali.

  Mzozo wa Tigray uliibuka mnamo Novemba mwaka jana wakati serikali ya Ethiopia ilipoanzisha shambulio la kukiondoa chama tawala cha jimbo hilo TPLF madarakani baada ya wapiganaji wake kuteka kambi za jeshi za serikali huko Tigray.

  Tangu mzozo ulipoibuka mwaka jana, maelfu ya watu wanafikiriwa kuuawa na mamilioni wanahitaji msaada wa kibinadamu.

  wakati huo huo Serikali ya Ethiopia imeshutumiwa kwa kutekeleza mauaji ya kiholela ya kijana mmoja - katika ripoti mpya ya Human Rights Watch. Amanuel Wondimu Kebede mwenye umri wa miaka 17 aliuawa katika mkoa wa Oromia wa Ethiopia mnamo Mei mwaka jana- ni mmoja wa raia wengi waliokufa tangu mapigano yalipoanza katika eneo hilo miaka 3 iliyopita. Imesababisha wito wa uwajibikaji zaidi kwa vikosi vya usalama nchini humo.

  Video iliyochapishwa kwenye mitandao ya kijamii ilionyesha dakika za mwisho za Amanuel Wondimu Kebede .. Mikono yake ilikuwa imefungwa nyuma yake. Bunduki ilikuwa imetundikwa shingoni mwake ... uso wake ulikuwa na damu wakati alikuwa akizungumza na kamera.

  Human Rights Watch inadai kwamba - dakika chache tu baadaye - vikosi vya usalama vya Ethiopia viliamuru kijana huyo ageuze kichwa chake… kabla ya kumpiga risasi mara mbili mbele ya mashahidi wasiopungua wanne.

  Wakati huo, ilidaiwa kuwa Amanuel alikuwa amempiga risasi na kumjeruhi mtu mwingine - na vile vile alikuwa akihusishwa na mauaji ya mwandishi wa habari wa huko.

  Hili pia limepingwa - na mashahidi wakisema alikuwa mwanafunzi mzuri ambaye alifanya kazi katika kanisa la eneo hilo.

  Mzozo wa miaka mitatu kati ya serikali na Jeshi la Ukombozi la Oromo umewaacha raia wengi wamekufa. Mashirika ya kutetea haki za binadamu yanadai udhalilishaji unaofanywa na vikosi vya usalama, pamoja na kuzima kwa mawasiliano na mauaji ya kiholela.

  Maelezo zaidi:

 4. Somalia yatangaza kurejesha uhusiano wa kidiplomasia na Kenya

  Caro Robi

  BBC Swahili

  Rais wa Farmajo na mwenzake Uhuru wa Kenya

  Somalia imetengaza kuwa inarejesha mahusiano ya kidiplomasia na nchi jirani ya Kenya baada ya kusitisha mahusiano hayo mwezi Desemba mwaka jana ikiishutumuj Kenya kwa kuingilia siasa zao za ndani.

  Naibu waziri wa habari wa Somalia Abdirahman Yusuf amesema sasa mahusiano ya kati ya nchi hizo mbili yamefufuliwa akiongeza Qatar ndiyo iliyoasaidia mchakato wa upatanisho.

  Serikali ya Kenya haijatoa tamko kuhusiana na tangazo hilo la Somalia ila Ikulu ya Rais ya Nairobi iliandika katika ukurasa wa Twitter leo kuwa Rais Uhuru Kenyatta amekutana na Mfalme wa Qatar Sheikh Tamim bin Hamad Al Thani na kupokea kile kilichotajwa ujumbe maalum.

 5. Kenya kufunga kambi za Kakuma, Dadaab kufikia Juni 2022

  kambi

  Kenya imethibitisha kuwasiliana rasmi na Shirika la Wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR na kutaarifu kuwa itafunga kambi za wakimbizi ya Dadaab na Kakuma ifikapo Juni 30, 2022.

  Waziri wa mambo ya nje wa nchini Kenya bwana Fred Matiangí ametangaza hayo baada ya kufanya mkutano na Filippo Grandi, mjumbe wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia wakimbizi.

  Dkt. Matiangí amesema kuwa timu ya maafisa wa serikali ya Kenya na Shirika la wakimbizi la Umoja wa Mataifa watafuatilia mchakato huo uliopangiwa kuanza Mei, 5, 2022.

  Mchakato wa sasa hivi unajumuisha kurejea katika nchi zao kwa hiari au kutoa kibali cha kufanyakazi au cha makazi bila malipo kwa wakimbizi kutoka jamii ya Afrika Mashariki.

  Wakati huo huo, Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limefurahishwa na mpango wa kupitiwa tena kwa mpango wa kufunga kambi hizo za wakimbizi.

  ‘’Sio kambi za kudumu za wakimbizi au kufungwa kwa haraka kwa kambi hizo au kukiuka kanuni ya kimataifa inayokataza nchi inayopokea wakimbizi kuwarejesha nchini mwao ambako wanaweza kuwa katika hatari ni suluhisho ya hili’’, UN imesema.

  Katika taarifa iliyotolewa na shirika hilo, imesema kuwa inaamini serikali ya Kenya na shirika la wakimbizi la Umoja wa Mataifa katika kubaini machaguo mengine ya kuwahifadhi au kurejea kwa hiari kwa wanaotaka kwa namna heshima.

  Mnamo mwezi Machi, serikali ya Kenya ilikuwa imeipatia UN makataa ya mwisho ya kutafuta njia kwasababu inataka kufunga kambi hizo mbili ambazo ni makazi kwa wakimbizi 400,000.

  Muda mfupi baadae, Shirika la Amnesty International likajibu kwa kusema kuwa hatua ya kufungwa kwa kambi za Dadaab na Kakuma bila mpangilio unaoheshimu haki za wakimbizi, kutasababisha janga la kibinadamu wakati tayari dunia inakumbana na janga la virusi vya corona.

  Kenya imekuwa ikitoa makazi kwa wakambizi kwa zaidi ya miaka 30 na sasa hivi serikali inasema uwezo wake kuendelea kuwatunza hata kwa kuzingatia viwango vya chini kabisa vya kibinadamu vinavyokubalika imekuwa changamoto kwa nchi hiyo kuvifikia.

  Katibu Mkuu nchini Kenya Karanja Kibicho, aliongeza kuwa uamuzi wake wa kufunga kambi za Dadaab na Kakuma kufikia Juni 30, 2022 ‘ni kwa maslahi ya raia wa nchi yake’.

 6. Na Mohammed AbdulRahman

  Mchambuzi

  Rais Mohammed Abdullahi Farmajo wa Somalia

  Umezuka wasiwasi katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu baada ya mapigano makali ya risasi Jumapili na Jumatatu ya wiki hii, Kati ya majeshi yanayomuunga mkono Rais Mohamed Abdullahi Mohamed maarufu kwa jina la "Farmaajo", na makundi ya wanamgambo yanayowaunga mkono wapinzani wake

  Soma Zaidi
  next
 7. Mohamed Hagi (R), Somaliland's Taiwan representative, bumps elbows while posing with Taiwan's Foreign Minister Joseph Wu during the opening ceremony of the Somaliland representative office in Taipei on September 9, 2020

  Taiwan na Somaliland ni maeneo mawili ambayo yote yanajitegemea kikamilifu ambayo yalijitangazia uhuru wake lakini hakuna ambalo linatambuliwa kimataifa na sasa hivi inasemekana kuwa yanaendelea kuwa na uhusiano wa karibu.

  Soma Zaidi
  next
 8. Farmajo aongezewa miaka miwili kuongoza Somalia

  Rais wa Somalia Mohamed Abdullahi Mohamed 'Farmaajo'
  Image caption: Bw. Farmajo amekuwa akishinikizwa na vyama vya upinzani na serikali za majimbo kuondoka madarakani

  Bunge la Somalia limepiga kura siku ya Jumatatu ili kurefusha muhula wa rais kwa miaka miwili zaidi kuliongoza taifa hilo la upembe wa Afrika ili kuliruhusu kujiandaa kufanya uchagzuzi wa moja kwa moja.

  Spika wa bunge hilo Mohamed Mursal Sheikh amesema wabunge 149 walipiga kura kuidhinisha pendekezo hilo,mmoja akalipinga ilhali watatu hawakupiga kura.

  Rais wa sasa Mohamed Abdullahi Mohamed 'Farmaajo' ambaye amekuwa ofisini tangu 16 Februari 2017 amekuwa akishinikizwa na vyama vya upinzani na serikali za majimbo kuondoka madarakani baada ya kukamilika kwa muda wake wa kuhudumu .

  Utata huo kati yake na viongozi wa majimbo hayo umesababisha wasi wasi ya uwezekano wa taifa hilo kutumbukia katika mgogoro Zaidi wa kiasa na kiusalama baada ya mapigano ya muda mrefu ya wenyewe kwa wneyewe na mashambulizi ya kigaidi kutoka kwa kundi la Al shabaab kuhujumu jitihada za jamii ya kimataifa kuleta uthabiti nchini humo.

  Maelezo zaidi: