Muhammadu Buhari

 1. Kiongozi wa vuguvugu la kujitenga Nigeria kufikishwa mahakamani leo

  Mwanachama wa kundi la Indigenous People of Biafra (Ipob),

  Kesi dhidi ya kiongozi wa vuguvugu la kujitenga nchini Nigeria Nnamdi Kanu inarejelewa leo mjini Abuja

  Bwana Kanu ni kiongozi wa kundi la Indigenous People of Biafra (Ipob), kundi linalotaka kujitenga kwa jimbo la kusini -mashariki mwa Nigeria, ambalo serikali imeharamisha. Anakabiliwa na mashataka ya "ugaidi na uhaini.

  Akipatikana na hatia huenda akafungwa maisha. Nnamdi Kanu amekua akizuiliwa na polisi wa kisiri kulingana na mawakili wake.

  Wiki iliyopita serikali ya Nigeria imefanyia marekebisho mashataka dhidi yake na kuongeza kuwa anaendesha kampuni haramu na kuchapisha taarifa za kuchafua sifa.

  Hali ya taharuki ilipanda mwezi Julai wakati amamlaka ilipokosa kumfikisha mahakamani kumfungulia mashataka.

  Mawakili wake wanataka serikali kuhakikisha anafikishwa mahakamani leo.

  Wanachama wa kundil lake linalotaka kujitenga kwa eneo la Biafra, have been agitating for a breakaway state for the southeast region of the country.

  Kanu alikamatwa mara ya kwanza Oktoba 2015, lakini akatoroka Nigeria 2017 baada ya jeshi kuvamia nyumbani kwake.

  Alikamatwa mwezi Juni mwaka huu. Mawakili wake walishutumu serikali kwa kukiuka sheria za kimataifa na kukiuka haki zake.

  Rais Buhari apongeza kukamatwa kwa Nnamdi Kanu

  Kukamatwa kwa Nnamdi Kanu kunawaacha wafuasi wa kujitenga wa Ipob wa Nigeria wakiwa katika hali mbaya

 2. Rais Buhari ahimiza utulivu baada ya shambulio lililowaua watu zaidi ya 40 Nigeria

  Ramani

  Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari ametuma risala za rambi rambi kwa familia za watu waliouawa katika shambulio kwenye soko la kijiji katika jimbo la kaskazini magharibi la Sokoto.

  Serikali ya jimbo la Sokoto ilisema watu 43 walifariki katika shambulio la Jumapili jioni baada ya watu wenye silaha kuvamia soko la wazi katika mji wa Goronyo.

  Katika taarifa yake, Rais Buhari anatoa wito kwa Wanigeria "wasikate tamaa" lakini "waendelee kuwa na subira" kwani mamlaka "zimeazimia zaidi kuliko hapo awali kuwalinda Wanigeria".

  Serikali yake imekosolewa vikali kwa kushindwa kukabiliana na ukosefu wa usalama ulioenea nchini, na mauaji na utekaji nyara unaotekelezwa na vikundi vyenye silaha vinaongezeka.

  Mashambulio yameendelea licha ya kupelekwa kwa maelfu ya maafisa wa vikosi vya usalama na pia kuzuiwa kwa mtandao na huduma za simu za rununu katika sehemu nyingi za kaskazini magharibi mwa nchi hiyo.

  Africa Eye: Watoto wa Nigeria wanaotekwa nyara

  Mzozo wa utekaji nyara Nigeria: Barua zilivyochukua nafasi ya simu

 3. Kano yajiandaa kwa 'harusi ya mwaka'

  Maharusi

  Mamia ya watu wamekusanyika nje ya kasri la Emir wa mji wa Bichi katika jimbo la Kano nchini Nigeria wakiwa na matumaini ya kujionea sherehe ya harusi ya mwana wa kiume wa Rais Muhammadu Buhari, Yusuf.

  Hatua yake ya kumuoa Zahra Bayero, binti wa Emir wa Bichi imewavutia wengi tangu tangazo lilipotolewa mwezi Juni kwamba kamati ya wanachama 145- itafanya maandalizi ya sherehe hizo.

  Sherehe ya Ijumaa inajulikana kama fatiha, ambayo hafla ya wanaume peke ambapo ibada za kitamaduni zinafanywa kulingana na dini ya Kiislamu, na inahuduriwa na viongozi wakuu wa serikali ya Nigeria akiwemo, Makamu wa Rais Yemi Osinbajo.

  Utamaduni Nigeria

  Sherehe ya harusi na dhifa ya chakula cha jioni imepangwa kufanyika siku ya Jumamosi.

  Usalama katika mji huo umeimarishwa kabla ya Rais Buhari kuwasili.

  Miongoni wa wageni wanaotarajiwa kuhudhuria harusi hiyo ni viongozi wa kisiasa wa Nigeria pamoja na wanasiasa kadhaa wa upinzani akiwemo makamu wa rais wa zamani Atiku Abubakar.

  Wakazi wa mji huo pia wamevalia mavazi ya kupendeza kwa ajili ya hafla hiyo kuu.

  Harusi
  Harusi
 4. Nigeria yataka wenye mitandao ya kijamii kupata vibali vya ndani

  Nigerian authorities suspended Twitter five days ago

  Kampuni za mitandao ya kijamii ambazo zinataka kuendesha shughuli zao nchini Nigeria sasa zitahitajika kujisajili nchini humo na kupewa leseni na tume ya utangazaji.

  Waziri wa mawasiliano,Lai Mohammed, ametoa tangazo hilo kufuatia hatua ya serikali kupiga Twitter marufuki siku tano iliyopita.

  Mtandao huo wa kijamii ulifuta ujumbe wa Rais Muhammadu Buhari kwa kukiuka sheria zake lakini ofisi ya rais imepinga madai kwamba marufuku hiyo ilikuwa hatua ya kilipiza kisasi.

  Baadhi ya vyombo vya habari vya kibinafsi nchini Nigeria vimepuuza amri ya kufunga akaunti zao za Twitter na kuamua kufikia mtandao huo kupitia mtandao wa VPN.

 5. Trump aunga mkono hatua ya Nigeria kuifungia Twitter

  Bw. Trump alifungiwa na Twitter na Facebook mwezi Januari
  Image caption: Bw. Trump alifungiwa na Twitter na Facebook mwezi Januari

  Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump amepingeza hatu ya Nigeria kuipiga marufuku Twitter - na kutoa wito nchi zingine zifuate mkondo huo.

  "Pongezi kwa nchi ya Nigeria, kwa kuifungia Twitter kwasababu ya kumpiga marufuki Rais wao," alisema katika taarifa.

  Rais huyo wa zamani ametoa wito kwa nchi zingine kufuata mkondo na kuzifungia Facebook na Twitter " kwa kudhibiti uhuru wa kujieleza".

  Bw. Trump alipigwa marufuku na katika mitandao ya kijamii ya Twitter na Facebook mwezi Januari kwa tuhuma za kuchapisha ujumbe wa kuchochea uvamizi wa bunge la Marekani. Watu watano walifariki kutokana na kisa hicho.

  Twitter

  Katika taarifa yake siku ya Jumatatu, alijita kwanini hakuzifungia Facebook na Twitter wakati wa Urais wake.

  "Wao ni nani kuamua kizuri na kibaya ikiwa wao wenyewe ni wabaya? Nadhani ningeliwapiga marufuku nilipokuwa Rais. Lakini [Mwanzilishi wa Facebook Mark] Zuckerberg aliendelea kunipigia simu na kuja Ikulu ya White House kwa chakula cha jioni akiniambia jinsi nilivyokua mzuri," alisema.

  Wiki iliyopita Nigeria ilifunga akaunti za Twitter nchini humo kwa madai kwamba "shughuli za mtandao huo zinahujumu uwepo wa Nigeria kama taifa lililoundwa shirikisho".

  Hatua hiyo ilichukuliwa siku kadhaa baada ya ujumbe wa Rais Muhammadu Buhari kuondolewa kwa kukiuka kanuni za mtandao wa huo wa kijamii.

  Ilizua ghadhabu miongoni mwa Wanaigeria na mataifa ya magharibi ambayo yalisema hatua hiyo inaminya uhuru wa kidemokrasi.

  Pande zote mbili zimesema zinajadiliana kuhusu namna ya kusuluhishi

  Soma zaidi:

 6. Rais wa Nigeria aelekea Uingereza kwa ukaguzi wa kimatibabu

  Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari

  Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari, anasafiri London leo katika kile ofisi yake inasema ni "uchunguzi wa mara kwa mara wa kimatibabu".

  Anatarajiwa kurejea nyumbani wiki ya pili ya mwezi Aprili, kulingana na taarifa kutoka kwa msemaji wa rais, Femi Adesina.

  Taarifa hiyo haikutoa maelezo yoyote kuhusu hali ya afya ya Bw. Buhari.

  "Rais atakutana na wakuu wa usalama, kabla ya kuanza safari yake,” Bw. Adesina alisema.

  Tangu alipokua rais karibu miaka sita iliyopita, Bw. Buhari amesafiri mara kadhaa nchini Uingereza kupata huduma za kimatibabu.

  Rais huyo ambaye ana umri wa miaka 78, alikaa zaidi ya miezi mitatu nje ya nchi mwaka 2017.

  Mwaka mmoja baadae alirejea London kwa siku nne – ziara ambayo wahudumu wake walidai "ilikuwa ya kumuona daktari wake".

  Hofu imekuwa ikiongezeka kuhusu hali ya afya ya rais. Tangu uchaguzi wa mwaka 2019, shughuli zake na kuonekana kwake hadharani zimekuwa nadra sana.