Alshabab

 1. Kenyatta afuta uwezekano wa Marekani kushambulia al-Shabab kutoka Kenya

  rAIS Uhuru Kenyatta (Kulia) akiwa na mwenyeji wake Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron

  Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amekiambia kituo cha habari cha France 24 kwamba hataidhinisha mashambulizi ya kutumia ndege zisizokuwa na rubani dhidi ya wanamgambo wa al-Shabab katika ardhi ya Kenya.

  Rais Kenyatta ambaye yuko nchini Ufaransa kwa ziara rasmi ya kikazi amesema hajapokea ombi lolote kama hilo.

  Mwezi uliyopita gazeti la New York Times lilinukuu vyanzo vya serikali ya Marekani ikisema majeshi ya nchi hiyo yanatafuta idhini ya kushambulia ngome za al-Shabab kutoka mashariki mwa Kenya.

  Ripoti hiyo ilitolewa siku kadhaa kabla ya mahakama ya kijeshi nchini Somalia kumhukumu mwanamgambo mmoja wa Kislam kifungo cha maisha gerezani kwa kuhusika na shambulio dhidi ya kambi ya jeshi la Marekani nchini Kenya.

  Shambulio hilo lilikuwa la kwanza kutekelezwa na wanamgambo wa al-Shabab dhidi ya vikosi vya Marekani nchini Kenya.

 2. Kenya yazuia mali ya 'wafadhili' wa Al Shabab

  Al Shabab

  Kenya imezuilia mali ya watu tisa wanaotuhumiwa kufadhili kundi la wanamgambo wa Al Shabab nchini Somalia.

  Wizara ya mambo ya ndani imesemahatua hiyo ni sehemu yajuhudi mpya za kukabiliana na ugaidina kudibiti ‘’ ugaidi nyumbani’’

  Katika taarifa yake waziri wa usalama wa kitaifa Fred Matiangi amesemakuzuiliwa kwamali ya Wakenya hao tisakutahakikishahawawezi tena kufadhili kundi la Al Shabab ‘’ ndani ya mipaka yetu’’.

  Pia ameonya kuwa kundi hilo lilikuwa likiwasajili ,kuwapa mafuzo na kuwawekamiongoni mwa raia‘’ ili waendeleze ajenda yao ya misimamo mikali na ugaidi.''

  Tangazo hilo linajiri wakati ambapo Rais Uhuru Kenyatta amewaambia viongozi wa kimataifa kwamba janga la Covid 19 limechangia vitendo vya kigaidi, kuzidisha mzozo wa wakimbizi na kuongezeka kwa silaha ndogo ndogo katika eneo la Pembe ya Afrika.

  Kenya imekabiliwa na mashambulio kadhaa kutoka kwa Al Shabab tangu ilipowapeleka wanajeshi wake Somalia 2011 kukabiliana na kundi hilo

  Rais Kenyatta ailikuwa akizungumza katika mkutano wa Aqaba kuhusu Covi-19 uliandaliwa kupitia mfumo wa kidijitali na Mfalme Abdullah wa pili wa Jordan ambao pia ulihudhuriwa na Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau, Rais Rodrigo Duterte wa Ufilipino na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guteress kujadili jannga la corona na usalama wa kimataifa.

 3. Mohamed Moalimu

  Mwandishi wa zamani wa BBC Mohamed Moalimu aliponea shambulio la Jumapili dhidi ya hoteli mji mkuu wa Somalia, Mogadishu - kwa mara ya nne amejipata katikati ya mashambulizi ya kundi la al-Shabab katika kipindi cha miaka saba.

  Soma Zaidi
  next