Equatorial Guinea

 1. Idadi ya vifo katika mlipuko Equatorial Guinea yaongezeka hadi 98

  Mamia ya watu bado wako hospitalini
  Image caption: Mamia ya watu bado wako hospitalini

  Idadi ya waliofariki kutokana na mlipuko mkubwa nchini Equatorial Guinea siku ya Jumapili imeongezeka hadi 98, maafisa wanasema

  Mlipuko huo ulitokea katika kambi ya jeshi mjini Bata.

  Maafisa wanasema mlipuko huo ulitokana na silaha ambazo zilihifadhiwa vibaya ambayo ilichomeka baada ya moto uliowashwa na wakulima katika shamba lililokuwa karibu.

  Idadi ya waliofariki iliongezeka baada ya wadumu wa kujitolea kuchukua karibi siku nzima kutafuta miili katika vifusi. Awali ilikadiriwa ni watu 31 pekee ndio waliofariki kutokana na mkasa huo.

  Mamia ya watu bado wako hospitalini

  Watoto wadogo watatu walipatikana wakiwa hai na kupelekwa hospitali.

  Karibu mijengo yote na nyumba za makazi katika mji huo ''ziliharibiwa vibaya'' na mlipuko huo, Rais Teodoro Obiang Nguema alisema.

  Katika taarifa, Rais Obiang Nguema alisema mlipuko huo ulisababishwa na "uzembe" uliohusishwa na hifadhi ya baruti kali katika kambi ya kijeshi ya Nkoantoma.

  Mambo matano muhimu kuhusu EquatorialGuinea:

  1. Ni nchi pekee barani Afrika inayozungumza Kihispania na ilipata uhuru wake kutoka kwa Uhispania 1968
  2. Imegawanywa katika sehemu ya bara na kisiwani, uliopo mji mkuu wa Malabo
  3. Rais Obiang Nguema, amekuwa madarakani tangu mwaka 1979, na amelaumiwa kwa ukiukwaji wa haki za binadamu.
  4. Maafisa wa nchi za Ulaya na mashirika yasiokuwa ya kiserikali yamemlaumu rais na familia yake kwa kujihusisha na ufisadi.
  5. Licha ya kuwa na utajiri wa mafuta na gesi asilimia 76, watu milioni 1.5 wanaishi katika hali ya umasikini, kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa na Benki ya Dunia.
 2. Chanjo ya Ebola yawasili Guinea

  Chango ya Ebola

  Ndege maalum iliyobeba shehena ya chanjo ya Ebola imewasili nchini Guinea usiku wa Jumatatu.

  Dhoruba ya vumbi iliyokumba eneo la Sahara siku ya Jumapili ililazimisha ndege hiyo kuelekezwa Senegal, hali iliyochelewesha kutolewa kwa chanjo kwa siku moja.

  Shughuli ya kutoa chanjo itaanza kufanyika katika mji mkuu wa Guinea, Conakry, hivi leo.

  Shehena ya Chanjo ya Ebola

  Dozi 11,000 ya chanjo hiyo zitapelekwa mji wa Nzérékoré kusini mashariki mwa nchi hiyo.

  Watu watano wamefariki hivi karibuni kutokana na Ebola.

  Huu ni mlipuko wa kwanza wa ugonjwa huo hatari Afrika Magharibi tangu mwaka 2016.

  Maelezo zaidi: