Swaziland

 1. Jeshi lapelekwa katika shule Eswatini

  Wanajeshi walisambazwa katika maeneo ya mijini wakati wa ghasia mwezi wa Julai
  Image caption: Wanajeshi walisambazwa katika maeneo ya mijini wakati wa ghasia mwezi wa Julai

  Wanajeshi na polisi wamepelekwa katika shule zote katika Eswatini ambako wanafunzi wamekuwa wakifanya maandamano kwa muda wa wiki moja kudai mageuzi ya kisiasa.

  Shule za msingi na sekondari katika nchi hiyo pekee ya Kiafrika inayotawaliwa Kifalme zamani ikifahamika kama Swaziland, wamekuwa wakisusia kuingia madarasani na kufanya mgomo baridi kwa mwezi mzima uliopita.

  Hapo nyuma, maandamano ya wanaounga mkono demokrasia yalikuwa yakifanyika katika maeneo ya mijini, lakini katika kipindi cha mwaka hivi -maandamano hayo yamekuwa yakionekana miongoni mwa jamii za vijijini-ambako kwa kawaida wamekuwa walimuunga mkono Mfalme.

  Maafisa wa usalama wamekuwa wakionekana katika miji mikuu ya Eswatini-Mbabane na Manzini.

  Maafisa wanasema wamepelekwa kusaidia kuimarisha amani lakini wanafunzi waandamanaji wanaamini ni kuwatisha.

  Maandamano ya wanafunzi ya wiki hii ni ya hivi karibuni katika miezi ya hivi karibuni ya ghasia katika ufalme huo mdogo.

  Wanatoa wito wa hali bora za kusoma na elimu ya bure. Wanasema gharama ya elimu katika shule za taifa haipatikani kwa wengi-katika nchi ambazo karibu 25% ya watu wazima hawana ajira.

  Waandamanaji, ambao wamekuwa wakikusanywa na makundi ya wanafunzi, pia wanadai kuachiliwa kwa wabunge wawili waliokamatwa wakati wa maandamano ya kudai demokrasia mapema mwaka huu.

  Mfalme Mswati III aliwahi kuwashutumiwa na wanaharakati kwa kutumia ghasia kuwanyamazisha wapinzani wake wa kisiasa-baadhi wanaona kusambazwa kwa wanajeshi kama sehemu ya kutekeleza nia hiyo.

  Ufalme wa Eswatini ni mojawapo ya nchi masikini zaidi barani Afrika-wakosoaji wake wanamshutumu kwa kuishi maisha ya anasa huku watu wake wakikabiliwa na njaa kila siku.

  Wachambuzi wa siasa wanasema maandamano ya mara kwa mara ya upinzani ni ishara ya kutaka mabadiliko nchini-kwamba watu wanaendelea kutofurahia utawala uliopo sasa madarakani.

 2. Mwanamke mwenye ukimwi anayewasaidia wengine 'kufa kifo kizuri'

  Thembi Nkambule

  Thembi Nkambule amekuwa akiwahudumia mamia ya watu wanaofariki kutokana na Ukimwi Eswatini - nchi ambayo mtu mmoja kati ya wanne ana HIV. Haya ndio mambo aliyojifunza juu ya maana ya "kifo kizuri".

  Soma zaidi