Jamuhuri ya Afrika ya Kati

 1. Rwanda yawapeleka wanajeshi wake kulinda amani C.A.R

  Wanajeshi wa Rwanda hulinda amani katika nchi kadhaa Afrika
  Image caption: Wanajeshi wa Rwanda wanlinda amani katika nchi kadhaa Afrika

  Kikosi cha Ulinzi cha Rwanda (RDF) kimeanza shughuli ya kuwapeleka wanajeshi 750 wa kujiunga na ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati (MINUSCA), kulingana na taarifa kutoka kwa jeshi.

  Kundi la kwanza la walinda amani 300 wakiongozwa na Luteni Kanali Patrick Rugomboka kiliondoka uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kigali kuelekea Bangui, Jumanne.

  Walipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Bangui, walinda amani wa Rwanda walikaribishwa na Kamanda wa Kikosi cha MINUSCA, Luteni Jenerali SADIKI Traoré akifuatana na Mkuu wa Wafanyikazi wa Kikosi cha Wanajeshi wa Jamuhuri ya Afrika ya Kati, Jenerali Zephlin Mamadou.

  Kamanda wa Kikosi alitoa shukrani zake kwa walinda amani wa Rwanda kwa kujitolea kwao bila kutetereka kulinda raia na kudumisha amani na usalama huko CAR.

  Kulingana na RDF, kikosi hicho kitapewa jukumu ulinzi katika njia kuu ya usambazaji (MSR1) inayounganisha Bangui na mpaka na Cameroon.

  Kufuatia hatua hii Rwanda sasa itakuwa na vikosi vitatu pamoja na Hospitali ya kiwango cha pili iliyowekwa chini ya MINUSCA.

 2. Police had locked the hut but items used in rituals can be seen through a crack in the door

  Visa kama hivyo vimetokea katika nchi za DRC, Liberia na hata Sudan Kusini . Hata hivyo kunavyo visa vya kuogofya ambavyo watu walipatikana na hatia ya kula nyama ya binadamu nchini Afrika kusini ,na kuzua hofu nchini humo miaka minne iliyopita .

  Soma Zaidi
  next
 3. UN yaingia tumbo joto kwa makundi binafsi ya kijeshi Jamhuri ya Afrika ya Kati

  Umoja wa Mataifa imeonesha wasiwasi juu ya ukiukaji wa haki za binadamu na makampuni binafsi ya jeshi

  Umoja wa Mataifa imeonesha wasiwasi wake juu ya kuongezeka kwa usajili na utumiaji wa vikosi binafsi vya jeshi kutoka nchi za nje na makampuni ya usalama na serikali katika nchi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati.

  Pia imeonesha wasiwasi wake juu ya uhusiano wa karibu ambao kampuni hizo na wafanyakazi wake wanauendeleza na walinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini humo.

  Nchi hiyo imeghubikwa na mapigano kati ya muungano wa waasi unaoongozwa na aliyekuwa rais François Bozizé na jeshi la kawaida linaloungwa mkono ma ujumbe wa UN huko (Minusca) na kampuni binafsi ya kijeshi ya Urusi.

  Katika taarifa iliotolewa Jumatano, kundi la wataalam wa UN limesema limepokea taarifa za ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu na sheria ya kimataifa ya misaada ya kibinadamu kwa kampuni binafsi za kijeshi zinazoendesha shughuli zake kwa pamoja na jeshi la nchi ya Jamhuri ya Afrika Kati na katika baadhi ya matukio ikijumuisha vikosi vya kulinda amani vya UN.

  Ukiukaji unajumuisha mauaji ya halaiki, kukamatwa kwa watu kiholela, mateso wakati wa kuhojiwa na watu kutojulikana walipo.

  Pia inaangazia wakazi kulazimishwa kuhama makazi yao na ubaguzi unaolenga vituo ya raia na watoa wa misaada ya kibinadamu.

  Kundi linalofanya kazi linashutumu ukosefu wa uchunguzi pamoja na ukosefu wa maamuzi ya kutambua wanaotekeleza manyanyaso hayo.

  Wataalam wametoa wito kwa serikali ya Jamhuri ya Kati na "washirika wake kimataifa" kufuata majukumu yao chini ya sheria ya kimataifa na hasa kuhakikisha wanaokiuka haki za binadamu na kutekeleza unyanyasaji wanakabiliwa na mkono wa sheria.

 4. Jean-Bedel Bokassa

  Mwezi Septemba 1979, aliyekuwa mfalme wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Jean-Bedel Bokassa, aling'atuliwa madarakani na nchi hiyo ikarejea katika utawala wa kiraia miaka kadhaa baada ya kushikwa mateka na mwanaume ambaye jina lake linatambulika na wengi kwenye simulizi nyingi za kushangaza.

  Soma Zaidi
  next
 5. Video content

  Video caption: Upasuaji huo hatari ulichukua takriban saa 18

  Mapacha wa miaka miwili wailioshikamana kichwani watenganishwa katika 'upasuaji wa kwanza wa kipekee'