Burudani

 1. Baa na klabu za burudani Kenya kufungwa saa tano usiku

  Eneo la burudani

  Baa na klabu zote za burudani zitafungwa mwendo wa saa tano nchini Kenya. Haya ni kwa mujibu wa Waziri wa Afya nchini Kenya Mutahi Kagwe.

  Kagwe hatahivo amesema kwamba baa na klabu za burudani zilizo na leseni ya kuhudumu hadi alfajiri zitaruhusiwa kuwa wazi.

  Hapo jana Rais Uhuru Kenyatta aliondoa kafyu ya kutotoka nje kuanzia saa nne usiku hadi saa kumi alfajiri lakini hakugusia suala la kufunguliwa kwa baa na klabu za burudani.

  Hatua hiyo ilishinikiza idara ya polisi kuingilia kati na kuelezea umma kwamba baa zote zitafungwa mwendo wa saa moja kama ilivyokuwa.

  Hatahivyo akihutubia taifa kuhusu hali ya maambukizi ya ugonjwa wa corona, Waziri kagwe alisema kwamba muda wa kufungwa kwa baa zote sasa utakuwa mwendo wa saa tano usiku.

  Katika hotuba yake ya kila siku, Kagwe hatahivyo amewataka Wakenya zaidi kujitokeza ili kupata chanjo ya Corona.

  Katika ujumbe wa Twitter polisi walikua wamesisitiza kuwa baa zifungwe kufikia saa moja usiku licha ya Rais Uhuru Kenyatta kuondoa amri ya kutotoka nje usiku iliyodumu kwa miezi 18.

 2. Kanye West abadilisha jina lake kuwa Ye

  Jina lake la awali- Kanye Omari West - halitatumika tena.
  Image caption: Jina lake la awali- Kanye Omari West - halitatumika tena.

  Msanii wa Marekani aliyekua akijulikana kama Kanye West sasa itajulikana rasmi kama wewe tu.

  Jaji wa Los Angeles aliridhia ombi la rappa huyo kubadilisha jina, afisa mawasiliano katika Mahakama Kuu ya Los Angeles alithibitisha.

  Nyota huyo wa miaka 44-aliwasilisha ombi hilo mwezi Agosti, akitoa "sababu za kibinafsi."

  Rapa huyo, anayejulikana sana kwa vibao kama vile Gold Digger na Stronger, alikua akitumia Ye kama jina la utani na mnamo 2018 alilitumia kama jina la albamu.

  Muda mfupi baada ya kutolewa kwa albamu hiyo, alitweet: "Kujulikana rasmi kama Kanye West. Mimi ni YE."

  Sasa amelifanya rasmi na jina lake la awali- Kanye Omari West - halitatumika tena.

  Ijapokua jina la Ye tayari lilikua likitumia kwenye Twitter, akaunti yake ya Instagram na wavuti yake bado inatumia jina lake la zamani kufikia Jumanne.

  "Ninaamini 'Ye' ni neno linalotumiwa sana katika Biblia, na katika Biblia linamaanisha wewe. Kwa hivyo mimi ni wewe, mimi ni nyinyi, yaani ni sisi," alisema katika mahojiano ya 2018 na mtangazaji wa redio Big Boy.

  Wasnii wengine waliobadilisha jina ni Prince, Snoop Dogg na Sean Love Combs, wengine wao mara kadhaa.

  Kim Kardashian West azungumzia matatizo ya akili ya Kanye West

  Je Umma unapaswa kumhukumu Kanye west kwa afya yake ya akili?

 3. Mwanamuziki wa Zambia ajitoa kuwania tuzo baada ya mashabiki kumpinga mtandaoni

  Slapdee

  Mwanamuziki maarufu wa Zambia Slapdee amejiondoa kuwania tuzo baada ya mashabiki kumkosoa kwa kufanya maonesho ya muziki kwa chama kilichokuwa madarakani.

  Chama hicho cha Patriotic Front kilishindwa uchaguzi na hivyo kundoka madarakani mwezi Agosti.

  Slapde, ambaye jina lake halisi ni Mwila Musonda, awali alitetea maamuzi yake ya kufanya maonesho kwa ajili ya maofisa kama biashara lakini inaoneka iliathiri muziki wake.

  Kufuatiwa kuchaguliwa Afrimma kushiriki kuwania tuzo, Wazambia walihamasisha watu watu mtandaoni kumpigia kura mwanamuziki wa Afrika Kusini Cassper Nyovest katika kipengele alichokuwa anawania cha mwanamuziki bora wa kiume kusini mwa Afrika ambapo kulikuwa na mshiriki wa Zimbabwe Jah Prayzah naTha Dogg kutoka Namibia na wengine.

  Kampeni za kumpinga Slapdee na kumuunga mkono Cassper Nyovest zilizua gumzo mtandaoni.

  Mwanamuziki wa Afrika kusini aliandika kwenye twitter "kwanini anazungumziwa Zambia?" alafu akasema "Ni sawa Zambia, hii ni biashara tu"

 4. Nyota wa Nigeria washirikisha simulizi za unyanyasaji wanazopitia

  N

  Nyota wa Nigeria wameanzisha kampeni katika mtandao wa Instagram na kueleza simulizi za maisha ya unyanyasaji walioupitia na ubaguzi waliokutana nao kwa kuweka #NobodyLikeWoman.

  Kampeni hiyo ilianzishwa na mwanamuziki na mcheza filamu wa Nigeria, Simi – ambaye akiwafanya wanawake wengi kushirikisha maoni ya maisha yao yenye machungu mengi kuhusu ndoa, ajira na muonekano.

  Nyota wa Nollywood Adesua Etomi-Wellington aliandika kwenye mtandao na kuhoji : “Je bado mjamzito?”

  View more on instagram

  Muigizaji na mwanamitindo Efe Irelealiweka picha ambapo alieleza mambo mabaya aliyopitia katika kazi yake : “Tunapiga picha usiku wote leo. Hawajali kuwa una watoto na mume wanakusubiri.”

  View more on instagram
 5. Video content

  Video caption: Tuzo ya Nobel: Joto la jua au kukumbatiwa ni tiba ya maumivu

  Sasa Wanasayansi ambao waligundua jinsi miili yetu inahisi joto la jua au kukumbatiwa kwa mpendwa wameshinda Tuzo ya Nobel.