Ujasiriamali

 1. Video content

  Video caption: Ubunifu: Mkaanga chips anayetumia mkaa wa aina yake kupikia

  Mjasiriamali Yazidu Yassin wa jijini Dar es salaam ameamua kutumia takataka kujitengenezea mkaa ambao anautumia kwenye biashara yake ya chipsi.

 2. Fahamu siri inayoendelea kumtajirisha bilionea nambari moja duniania duniani

  Jeff Bezos

  Jeff Bezos tajiri mkubwa duniani anayesimamia kampuni ya kimataifa ya Amazon inayofanya vizuri.

  Kampuni yake inakadiriwa kuwa na thamani ya takribani dola bilioni $171 sawa na (£137bn), na pia ameweza kutengeneza mabilioni ya pesa wakati wa janga la Covid-19 .

  Lakini je, anazingatia nini katika kuhakikisha anaendelea kufanikiwa?

  Fahamu siri inayomfanyatajiri mkubwa duniani kuendelea kutajirika

  1. kila tatizo linaweza kutatuliwa kwa kufikiria na uwepo wa ukweli.

  2. Kila wakati mteja ni mfalme.

  3. Fikiria anachotaka mteja na namna ya kutimiza hitaji lake.

  4. Kila siku chukulia kana kwamba ni siku ya kwanza ya biashara yako. Kuwa na hamu ya kutaka kuona unavumbua kitu cha kipekee hadi mafanikio yake.

  5. Kuwa na moyo wa kutaka kujaribu kitu hata kama kutakuwa na hatari ya kupoteza.

  6. Na hata usipofaulu, hautakuwa sawa na ambaye hajajaribu. Hivyobasi, pendelea kuwa mtu wa kudhubutu.

  7. Hutawahi kujuta kwa kujaribu kitu fulani.

  “Unapofikiria vitu ambavyo hujafanya ukiwa umetimiza miaka 80, mara nyingi ni vile ambavyo hukujaribu kabisa. Ni nadra sana kujuta kwasababu ya jambo ambalo ulijaribu kufanya lakini halikufanikiwa.”

  8. Zungumza unachodhani ni sahihi.

  9. Usiogope ushindani.

  10. Angalia malengo ya muda mrefu.

  Inasemekana kuwa tajiri huyu wa dunia Bezos, “yuko tayari kuchukua miaka 10 kufanya kitu kitakachomwezesha kupata peza miaka ijayo” na kusalia na lengo lake mradi linaonesha dalili ya kupiga hatua.

  Soma zaidi kuhusu tajiri mkubwa duniani

  Jeff Bezos: Mtu tajiri zaidi duniani ni mtu wa aina gani?

 3. Video content

  Video caption: Britney Spears anyimwa haki ya kumiliki mali yake.

  Mwanamuziki maarufu nchini Marekani amenyimwa haki ya kumiliki mali yake na mahakama moja nchini humo.

 4. Saniniu Kuryan Laizer akionyesha mawe ya Tanzanite ya awali yaliyompatia hadhi ya Ubilionea

  Mtanzania Saniniu Kuryan Laizer ambaye hivi karibuni aligeuka kuwa bilionea baada ya kupate mawe ya madini ya Tanzanite yenye thamani ya shiling bilioni 7.8, ameagundua jiwe lingine la Tanzanite lenye thamani ya mabilioni kwa shilingi za Kitanzania.

  Soma Zaidi
  next
 5. Je unataka kufaulu katika jitihada zako za kujitafutia maisha ?

  Video content

  Video caption: Ni masuala gani muhimu ya kuyazingatia ili kufanikiwa katika malengo yako?

  Tazama mambo 3 ambayo unayohitaji kutekeleza iliufanikiwe maishani

 6. Mo Dewji afunguka kuhusu siku 9 akiwa mikononi mwa mateka

  Bilionea kijana Afrika na mmiliki wa mojawapo ya klabu maarufu ya soka Afrika mashariki Simba SC - Mohammed Dewji akumbuka muda alipotekwa mwaka jana na namna alivyotishiwa maisha yake Tanzania.

  Soma Zaidi
  next