Mitetemeko ya Ardhi

 1. Tetemeko la ardhi latokea Mara,Tanzania

  Tetemeko la ardhi la uzani wa4.7 katika vipimo vya richa limeripotiwa kutokea Mkoa wa Mara nchini Tanzania mapema Alhamisi.

  Kwa mujibu wa shirika la Marekani la utafiti wa masuala ya jiolojia la Marekani (USGS), tetemeko hilo liligonga Kusini Magharibi mwa mji wa Tarime.

  Matetemeko madogo ya ardhi pia yaliripotiwa katika miji kadhaa ya magharibi mwa nchi jirani ya Kenya ikiwa ni pamoja na Kisumu, Homabay, Kilgoris, Siaya na Migori.

  Gazeti la Mwananchi mtandaoni linaripoti kuwa Mkuu wa mkoa huo amethibitisha tukio hilo.

  View more on twitter

  USGS linachunguza na kuripoti athari za tetemeko la ardhi na kufanya utafiti wa kubaini chanzo cha matetemeko ya ardhi.

 2. Video content

  Video caption: Tetemeko la ardhi Uturuki: Tazama Mtoto wa miaka mitatu alivyookolewa baada ya saa 65

  Mtoto huyo alikwama ndani ya kifusi cha jengo lililoporomoka kwa karibu siku tatu.

 3. Video content

  Video caption: Raia wa Kenya na Tanzania wasimulia tetemeko la ardhi lililvyotokea

  Hakuna uharibifu ulioripotiwa.