Unyanyasaji wa Nyumbani

 1. Anne Ngugi

  BBC Swahili

  Cecilia

  Kubakwa ni tukio ambalo Mchungaji Cecilia Muthoni Ssewagaba, hatawahi kulisahau maishani mwake. Lakini tukio hili ambalo alilipitia utotoni yameachia kofu moyoni mwake, lakini bila shaka halikumkatisha tamaa ya kusonga mbele na maisha na kuwasaidia wengine waliopitia masaibu kama yake.

  Soma Zaidi
  next
 2. Esmeralda Millán

  Esmeralda Millán alikuwa na miaka 23 Disemba mwaka 2018 aliposhambuliwa kwa tindikali mjini Puebla, Mexico. Mpenzi wake wa zamani na baba ya watoto wake wawili anayetuhumiwa kufanya shambulio hilo anazuiliwa kwa jaribio la mauaji.

  Soma Zaidi
  next
 3. Picha

  Unyanyasaji dhidi ya wanaume ni nadra sana kutokea na kujadiliwa na hasa unyanyasaji wa kingono dhidi ya mwanaume au unyanyasaji wa mwanaume ambaye amefanyiwa unyanyasaji na mtu wa familia yake.

  Soma Zaidi
  next
 4. Afungwa siku moja kwa kumuua mume wake Kenya

  Mahakamani

  Mahakama nchini Kenya imemhukumu kifungo cha siku moja mwanamke aliyemuua mume wake mwaka mmoja uliopita, Kwa mujibu wa gazeti la Daily Nation.

  Jaji Roselyn Aburili alimpata Truphena Ndong’a Aswani na kosa la kumuua mumewe Disemba 14, mwaka jana.

  ''Hakua na sauti. Alinyamazishwa kwa kichapo hadi akakubali kupigwa ni jambo la kawaida. Ana bahati yuko hai'', gazeti hilo lilinukuu maneno aliyotumia Jaji Aburuli.

  Mtuhumiwa alionewa huruma na Jaji kwa kuvumilia mateso na kumhukumu kifungo cha siku moja ambacho hakikujumuisha kuzuiliwa ndani.

  Aidha Jaji Aburili aliagiza idara ya mahakama kuhakikisha Bi Truphena amepewa usafiri wa kwenda hadi nyumbani kwake Ukwala katika Kaunti ya Siaya Magharibi mwa Kenya.

  Ni nini kilitokea?

  Bi Truphena aliye na umri wa miaka 49 aliifahamisha mahakama kwamba alivumilia mateso katika ndoa yake ili kumtunza mwanawe wa kiume na watoto wengine wanne walioachwa na mama zao (wake wa awali) wa Bw. James Oyengo Obochi.

  Siku ya mkasa, mahakama ilifahamishwa Bw. Obochi alirejea nyumbani usiku akiwa mlevi kama ilivyo ada akapewa chakula.

  Baada ya kula huku akiwa amelewa alianza kuzozana na mkewe akidai kupewa hati miliki ya shamba la familia.

  Alipokataa kumpatia nyaraka hizo kwa kuhofia anaweza kuzitumia kuuza shamba lao, alikimbilia chumbani na kuchukua panga kumkata mke wake.

  Lakini alimshinda nguvu katika purukushani hilo akamuua katika juhudi za kujilinda.

 5. Unyanyasaji dhidi ya wanawake waongezeka Afrika

  Wanawake

  Ripoti mpya ya Shirika la Afya Duniani (WHO) imefichua kwamba thuluthi tatu ya wanawake hukumbana na unyanyasaji wa kijinsia na kingono wakati mmoja maishani mwao.

  Ripoti hiyo ni moja ya utafiti mkubwa zaidi kufanywa kuhusu unyanyasaji dhidi ya wanawake na inajumuisha data kati ya mwaka 2000-2018.

  WHO linasema janga la corona limechangia kuongezeka kwa visa vya unyanyasaji dhidi ya wanawake. Linaripoti visa vya wanawake kushambuliwa na wenzi wao kuongezeka zaidi.

  Hali hiyo inawaathiri zaidi ya wanawake milioni 640 kote duniani.

  Asia Kusini, Kusini mwa Jangwa la Sahara, na Oceania zina viwango vya juu vya unyanyasaji wa wenzi.

  Robo ya wanawake walio na umri kati ya miaka 15 -24 tayari wamekabiliwa unyanyasaji kutoka kwa wenzi wao.