Maandamano

 1. Video content

  Video caption: Uchaguzi wa Marekani 2020: Tazama jinsi waandamanaji walivyovamia bunge Marekani

  Takriban watu wanne wamefariki nchini Marekani baada ya waandamanaji wanaomuunga mkono rais Trump kuvamia bunge na kuzuia kuidhinishwa kwa Joe Biden kuwa mshindi wa uchaguzi uliopi

 2. wafuasi wa upinzani walikabiliana na maafisa wa polisi Jijini nairobi

  Mkurugenzi wa uchunguzi wa mashtaka ya jinai nchini Kenya George Kinoti amefafanua kwana ofisi yake haina mpango wa kufufua upya kesi zilizopita za ghasia za baada ya uchaguzi wa maka 2007 kama inavyodaiwa na baadhi ya viongozo nchini humo.

  Soma Zaidi
  next
 3. Habari za hivi pundeUchaguzi wa Uganda 2021:Mwanamuziki Bobi Wine aachiwa kwa dhamana

  Mwanamuziki Bobi Wine

  Mahakama moja mashariki mwa Uganda imemshtaki mgombea urais wa chama cha upinzani Robert Kyagulanyi maarufu kama Bobi Wine, kwa makosa ya kutenda kitendo chenye uwezekano wa kusambaza ugonjwa wa kuambukiza.

  Bobi Wine alikamatwa katika mkutano wa kampeni Jumatano akishtumiwa kwa kukiuka miongozo ya kudhibiti ugonjwa wa virusi vya corona kwenye mkusanyiko wa hadhara.

  Hata hivyo Bobi Wine amepewa dhamana.

  Wakati huohuo, jeshi la Uganda limeongeza wanajeshi wake katika mji wa Kampala na miji mingine kukabiliana na maandamano yanayoendelea kuibuka.

  Hadi kufikia sasa watu 28 wamethibitishwa kufariki dunia kote nchini humo wakati wa maandamano yaliyokuwa yakidai kuachiliwa huru kwa Bobi Wine huku wengine zaidi ya 500 wakikamatwa, kulingana na jeshi la polisi.

  Maandamano hayo ya kudai kuachiliwa huru kwa Bobi Wine, yalisambaratishwa kwa kutumia vitoza machozi na wakati mwingine risasi zilitumiwa.

  Awali, naibu msemaji wa jeshi, Kanali Deo Akiiki aliviambia vyombo vya habari kuwa wanajeshi watapelekwa katika barabara zote kuu zinazoingia mjini.

  Januari 2021, Uganda itakuwa na uchaguzi mkuu wa urais lakini wiki za kwanza za kampeni tayari zimekubwa na vurugu na ghasia.

  Pia unaweza kusoma:

  Serikali kugharamia matibabu ya waliojeruhiwa katika maandamano ya Bobi Wine

  Idadi ya waliopoteza maisha katika maandamano Uganda yafikia 28

  Ofisi ya Bobi Wine yavamiwa Uganda