Chanjo

 1. Aina mpya ya kirusi cha Corona yatua Ulaya

  Kisa cha kwanza cha maambukizi charipotiwa Ubelgiji
  Image caption: Kisa cha kwanza cha maambukizi charipotiwa Ubelgiji

  Ubelgiji imeripoti kisa cha kwanza cha aina mpya ya kirusi cha Corona barani Ulaya ambacho kwanza kigunduliwa nchini Afrika Kusini - huku Shirika la Afya Duniani likifanya mkutano maalum kuangazia umuhimu wake.

  Wataalamu mjini Geneva wataamua ikiwa kirusi hicho kinahitaji kutambuliwa kama ni hatari.

  WHO inasema itatoa mwongozo mpya baada ya mazungumzo lakini imeonya kwamba itachukua wiki kadhaa kubaini ikiwe kirusi hicho kivyoweza kuambukizwa na ikiwa chanjo itasalia kuwa na ufanisi dhidi yake.

  Rais wa Tume ya Ulaya, Ursula von der Leyen,iliwakumbusha watengenezaji kwamba kandarasi zao na EU inamaanisha lazima wabadili chanjo zao mara moja kwa kuzingatia kirusi hiki kipya.

  Pia alisema kuwa safari zote za anga kwenda nchi zilizo na kirusi kipya cha corona zinapaswa kusitishwa.

  Soma zaidi:

  B.1.1.529 : Fahamu aina mpya ya kirusi hatari cha corona kilichogunduliwa

 2. Amnesty International yaomba Kenya kutowalazimisha watu kuchomwa chanjo ya Corona

  Shirika la kutetea haki za binadamu Amnesty International tawi la Kenya limetoa wito kwa serikali ya Kenya kutowalazimisha raia wake kupewa chanjo ya Covod -19.

  Katika taarifa shirika hilo lilsema: 'Kamati ya kitaifa ya kukabiliana na janga la Corona iharakishe programu za elimu zinazofaa ili kushughulikia chanjo kwa uwazi na kushughulikia taarifa potofu'.

  ''Ingawa kuna sababu halali za afya ya umma kwa watu wengi iwezekanavyo kupata chanjo, sababu hizi zisiwanyime watu haki ya kufanya kazi, kupata huduma muhimu zikiwemo elimu, afya na usalama pamoja na uhuru wao wa kutembea. Haya yote ni haki za kimsingi na uhuru wa kikatiba,'' ilisema taarifa hiyo.

  th

  Siku ya Jumapili Waziri wa afya wa Kenya Mutahi Kagwe alisema watu ambao hawajachanjwa watazuiwa kupata huduma za usafiri wa umma, ndege na treni.

  Utaratibu huo utaanza kufanya kazi Disemba 21.

  Kenya imepanga kuchanja watu milioni 10 mpaka kufikia mwishoni mwa Disemba mwaka huu .

  Mpaka sasa ni chini ya asilimia 10% ya watu wamepatiwa chanjo.

 3. Covid-19: Pfizer kuruhusu mataifa yanayoendelea kutengeneza kidonge cha matibabu

  The deal will allow local drug manufacturers to produce the treatment pill

  Kampuni ya dawa ya Marekani ya Pfizer imetia saini mkataba wa kuruhusu kidonge chake cha majaribio cha tiba ya Covid-19 kutengenezwa na kuuzwa katika mataifa 95 yanayoendelea.

  Lakini haijumuishi nchi kadhaa ambazo zimekuwa na milipuko mikubwa ya Covid-19, ikiwemo Brazil.

  Pfizer anasema kidonge hicho kinapunguza hatari ya ugonjwa mbaya kwa watu wazima walio hatarini.

  Katika taarifa yake siku ya Jumanne, Pfizer ilisema makubaliano hayo yataruhusu watengenezaji wa dawa za kienyeji kuzalisha kidonge hicho "kwa lengo la kuwezesha upatikanaji wake kwa urahisi duniani".

  Pfizer haitapokea mirabaha ya mauzo katika nchi zenye mapato ya chini na ilisema itaondoa mirahaba katika mataifa yote yaliyojumuishwa katika makubaliano hayo huku Covid ikisalia kuwa dharura ya afya ya umma iliyotambuliwa na Shirika la Afya Duniani.

  Mapema Novemba, Pfizer alisema majaribio ya kimatibabu yanaonyesha kuwa kidonge chake cha Covid-19, Paxlovid, kinapunguza kwa 89% hatari ya kulazwa hospitalini au kifo kwa wagonjwa wazima walio katika hatari kubwa.

  Mabilioni ya pesa ambayo nchi za afrika mashariki zimepewa kupambana na janga la Corona

 4. Chanjo ya HPV inapunguza saratani ya shingo ya kizazi kwa karibu 90%-Utafiti

  rwanda

  Chanjo ya human papillomavirus, au HPV, inapunguza visa vya saratani ya shingo ya kizazi kwa karibu 90%, data ya kwanza ya kweli inaonesha.

  Taasisi ya Utafiti wa Saratani Uingereza ilielezea matokeo hayo kama ya "kihistoria", na ilisema kuwa chanjo hiyo ilikuwa ikiokoa maisha.

  Takriban saratani zote za shingo ya kizazi husababishwa na virusi, na matumaini ni kwamba chanjo inaweza karibu kuondoa ugonjwa huo.

  Watafiti walisema mafanikio hayo yanamaanisha kuwa wale ambao walichanjwa wanaweza kuhitaji vipimo vichache vya uchunguzi wa mlango wa kizazi pia.

  Wasichana wanapewa chanjo hiyo kati ya umri wa miaka 11 na 13, kulingana na wapi wanaishi nchini Uingereza. Chanjo hiyo pia imetolewa kwa wavulana tangu 2019.

  Utafiti huo uliochapishwa katika jarida la Lancet, uliangalia kile kilichotokea baada ya chanjo hiyo kuanzishwa kwa wasichana nchini Uingereza mwaka 2008.

  Wanafunzi hao sasa ni watu wazima katika miaka ya 20. Utafiti huo ulionesha kupungua kwa ukuaji wa kabla ya saratani na kupungua kwa saratani ya shingo ya kizazi kwa 87%.

 5. Baa na klabu za burudani Kenya kufungwa saa tano usiku

  Eneo la burudani

  Baa na klabu zote za burudani zitafungwa mwendo wa saa tano nchini Kenya. Haya ni kwa mujibu wa Waziri wa Afya nchini Kenya Mutahi Kagwe.

  Kagwe hatahivo amesema kwamba baa na klabu za burudani zilizo na leseni ya kuhudumu hadi alfajiri zitaruhusiwa kuwa wazi.

  Hapo jana Rais Uhuru Kenyatta aliondoa kafyu ya kutotoka nje kuanzia saa nne usiku hadi saa kumi alfajiri lakini hakugusia suala la kufunguliwa kwa baa na klabu za burudani.

  Hatua hiyo ilishinikiza idara ya polisi kuingilia kati na kuelezea umma kwamba baa zote zitafungwa mwendo wa saa moja kama ilivyokuwa.

  Hatahivyo akihutubia taifa kuhusu hali ya maambukizi ya ugonjwa wa corona, Waziri kagwe alisema kwamba muda wa kufungwa kwa baa zote sasa utakuwa mwendo wa saa tano usiku.

  Katika hotuba yake ya kila siku, Kagwe hatahivyo amewataka Wakenya zaidi kujitokeza ili kupata chanjo ya Corona.

  Katika ujumbe wa Twitter polisi walikua wamesisitiza kuwa baa zifungwe kufikia saa moja usiku licha ya Rais Uhuru Kenyatta kuondoa amri ya kutotoka nje usiku iliyodumu kwa miezi 18.

 6. Misri kuwazuia wafanyikazi ambao hawajachanjwa kwenda kazini

  Egypt has administered about 30m Covid vaccine doses

  Misri itawazuia wafanyikazi wa umma ambao hawajachanjwa dhidi ya kuingia katika majengo ya serikali kutoka katikati ya mwezi ujao.

  Ilani ya baraza la mawaziri Jumapili ilisema wafanyikazi watalazimika kupewa chanjo au kufanyiwa vipimo vya Covid kila wiki ili waruhusiwe kuingia kwenye majengo ya serikali kutoka 15 Novemba.

  Baraza la mawaziri pia liliruhusu kufunguliwa kwa bafu katika misikiti kutoka Jumatano.

  Bafu zilifungwa mnamo Machi mwaka jana kama sehemu ya hatua za kuzuia kuenea kwa virusi vya Corona Serikali pia imetenga pauni bilioni Moja za Misri ($ 64m; £ 47m) kushughulikia janga hilo.

  Misri imetoa chanjo zaidi ya milioni 30 kwa raia wake dhidi ya idadi ya watu zaidi ya milioni 100, kulingana na data kutoka kwa wizara yake ya afya.

 7. Uganda yatoa agizo kwa wafanyakazi wote wa umma kupata chanjo

  chanjo

  Wakala wa serikali ya Uganda wanaosambaza chanjo ya Uviko -19 katika vituo vya afya amewaambia wafanyakazi wote na wageni kuonesha uthibitisho wa kuwa wamepata chanjo zote za corona.

  Mtu yeyote ambaye hajapata chanjo zote za corona lazima awasilishe cheti cha kuonesha kuwa hana maambukizi ya corona ,vipimo ambavyo amevifanya ndani ya saa 72 la sivyo hataruhusiwa kuingia ndani.

  Katika taarifa, maduka ya dawa yanayomilikiwa na serikali yanapaswa kuonesha mfano.

  Wale ambao wameathirika na agizo hilo ni wakurugenzi wa hospitali za umma, wauza madawa, wasambazaji wa dawa pamoja na wafadhili na wanasiasa.

  Uganda mpaka sasa imepokea dozi milioni 5.6 za chanjo za Covid-19 - na nyingine zilikuwa zimechangiwa lakini ni watu milioni 2.3 ndio wamepata chanjo na watu 580,000 ndio wamemaliza dozi kamili ya chanjo.

  Waziri wa afya Jane Ruth Aceng, siku ya Jumatano alilaumu mchakato wa utoaji chanjo kwenda taratibu.

  Taifa hilo limepanga kutoa kipaumbele kwa kutoa chanjo kwa watu milioni 4.8 la kundi la watu ambao ni pamoja na watumishi wa afya na walimu ,mpaka ifikapo mwezi Disemba mwaka huu.

  Kufunguliwa tena kwa uchumi wa nchi hiyo kunategemea chanjo.

 8. Nchi 40 za Afrika zafeli kufikia lengo la chanjo dhidi ya Corona

  Chanjo

  Shirikala Afya Duniani linasema kuwa ni mataifa 14 pekee ya Afrika yamefikia lengo la kuchanja asilimia 10 ya raia wao dhidi ya Covid-19.

  Hii ni kwa sababu mpango wa Covax, unaolenga kusaidia nchi masikini kupata chanjo haujafanikiwa kufanya hivyo baada ya nchi tajiri kununua chanjo zote.

  Kati ya nchi hizo 14 ni Ushelisheli, Mauritius na Morocco ambazo zimefanikiwa kufikia lengo la kimataifa la chanjo dhidi ya Covi-19 kufikia sasa.

  Asilimia 14 ya raia wa nchi hizo tatu wamepata chanjo kamili.

  Nchi zinine zilizofikia lengo la kamataifa la chanjo hiyo ni Tunisia, Eswatini, Cape verde, Botswana, Comoros, Zimbabwe, Equatorial Guinea, Afrika Kusini, Mauritania, Lesotho na Rwanda.

  Mpango wa chanjo wa Covax ulitarajiwa kuwasilisha dozi milioni 274 za chanjo kwa nchi za Afria kufikia mwisho wa mwezi Septemba, lakini imefanikiwa kuwasilisha zaidi ya dozi milioni tano.

  Chanjo ya Corona: Nini kitahitajika kwa bara hili kuanza kutengeneza chanjo zake?

  Virusi vya Corona: Kwanini baadhi ya nchi za Afrika hazijatumia chanjo zote walizopokea?