Uhalifu

 1. Benzema akabiliwa na kesi ya udhalilishaji wa kingono ya Ufaransa

  On the pitch Karim Benzema, 33, has scored for Real Madrid and France in the past 10 days

  Mshambuliaji wa Real Madrid Karim Benzema ameshtakiwa nchini Ufaransa kwa kuhusika na jaribio la kumlaghai mwanasoka mwenzake Mathieu Valbuena kuhusiana na viddeo ya ngono iliyopatikana katika simu yake.

  Amepuuza mashtaka dhidi yake na kukosa kufika mahakamani mjini Versailles.

  Kesi hiyo ni ya kutoka Juni 2015, wakati wanasoka hao walikua katika kambi ya mazoezi huko Ufaransa.

  Sakata hiyo iliyokumba soka ya Ufaransa ilifanya wachezaji wote wawili kupoteza nafasi zao.

  Karim Benzema, 33, hata hiyo amerejea katika timu ya Ufaransa na kufungia bao Real Madrid mjini Kyiv Jumanne katika michuano ya Ligi ya Mabingwa.

  Amefunguliwa mashataka pamoja na wanaume wengine wanne kwa kujaribu kumtapeli Bw. Valbuena, ambaye aliambia mahakama kuwa soka ni maisha yake.

  "Nilijua video hiyo ingelivujishwa maisha yangu yataathiriwa katika timu Ufaransa," alisema kulingana na waandishi wa habari.

  Kesi juu ya video hiyo ya ngono ilianza mwaka 2015 wakati Valbuena, ambaye sasa ana miaka 37, kumuomba mtu huko Marseille, Axel Angot, kupakua yaliyomo kwenye simu yake ya rununu kwa kifaa kipya.

  Tetesi za Soka Ulaya Jumatano 20.10.2021: Mount, Fati, Trippier, Adeyemi, De Ligt, Pepi, Bruce

 2. Rais Buhari ahimiza utulivu baada ya shambulio lililowaua watu zaidi ya 40 Nigeria

  Ramani

  Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari ametuma risala za rambi rambi kwa familia za watu waliouawa katika shambulio kwenye soko la kijiji katika jimbo la kaskazini magharibi la Sokoto.

  Serikali ya jimbo la Sokoto ilisema watu 43 walifariki katika shambulio la Jumapili jioni baada ya watu wenye silaha kuvamia soko la wazi katika mji wa Goronyo.

  Katika taarifa yake, Rais Buhari anatoa wito kwa Wanigeria "wasikate tamaa" lakini "waendelee kuwa na subira" kwani mamlaka "zimeazimia zaidi kuliko hapo awali kuwalinda Wanigeria".

  Serikali yake imekosolewa vikali kwa kushindwa kukabiliana na ukosefu wa usalama ulioenea nchini, na mauaji na utekaji nyara unaotekelezwa na vikundi vyenye silaha vinaongezeka.

  Mashambulio yameendelea licha ya kupelekwa kwa maelfu ya maafisa wa vikosi vya usalama na pia kuzuiwa kwa mtandao na huduma za simu za rununu katika sehemu nyingi za kaskazini magharibi mwa nchi hiyo.

  Africa Eye: Watoto wa Nigeria wanaotekwa nyara

  Mzozo wa utekaji nyara Nigeria: Barua zilivyochukua nafasi ya simu

 3. Video content

  Video caption: Africa Eye: Watoto wa Nigeria wanaotekwa nyara

  Kumeshuhudiwa jumla ya matukio tisa makubwa ya utekaji katika ajimbo matano

 4. Masten Wanjala: Mtuhumiwa wa mauaji aliyetoroka kizuizini auawa Kenya

  Bw Wanjala alikiri kutumia dawa za kulevya na kuua zaidi ya watoto 10
  Image caption: Bw Wanjala alikiri kutumia dawa za kulevya na kuua zaidi ya watoto 10

  Masten Wanjala mtuhumiwa aliyekiri kuwaua zaidi ya watoto kumi na baadaye kutoroka katika kituo cha polisi alipokua anazuiliwa ameuawa na wanakijiji wa Bungoma magharibi mwa Kenya.

  Naibu kamishena wa kaunti ya Bungoma Cornelius Nyaribai amethibitisha kifo chake katika ujumbe wa Twittter.

  Polisi wanasema Masten Wanjala alifuatwa na wanakijiji hadi nyumbani katika mji wa Bungoma na kupigwa hadi kufa.

  Mamlaka ilikuwa imeanzisha msako mkali kumtafuta mtu huyo ambaye alikiri kuwaua zaidi ya wavulana kumi katika kipindi cha miaka mitano.

  Masten Wanjala alitoweka kutoka kwa seli za polisi katika mji mkuu, Nairobi saa chache kabla ya kuitikia mashtaka ya mauaji ya wavulana 14.

  Maafisa watatu wa polisi wa Kenya waliokuwa kazini siku walifishwa mahakamani siku ya Alhamisi na kufunguliwa mashtaka ya kumsaidia mtuhumiwa huyo.

  Bwana Wanjala alikamatwa mnamo Julai na alikiri kutumia dawa za kulevya na kuwaua wavulana wadogo, na pia kunywa damu zao katika visa vingine.