Hali mbaya ya hewa

 1. Video content

  Video caption: Gambia ina jua la kutegemewa, lakini ni kwanini hailitumii kuzalisha nishati?

  Wagambia huzalisha nishati mbadala kibinafsi kwasababu hawawezi kutoshelezwa na nishati ya mifumo ya umeme ya taifa.

 2. Video content

  Video caption: Afisa usalama barabarani wa Iraq anayeongoza magari katika kiwango cha nyuzijoto 50

  Iraq ni mojawapo ya maeneo yenye hali ngumu ya hewa kwa mtu kuishi. Kushuhudia hilo BBC imefuatilia maisha ya askari wa usalama barabarani kazini katika nyuzijoto zaidi 50

 3. Mafuriko yasababisha vifo vya takriban watu 24 India

  Raia wa India

  Watu wasiopungua 24 wamefariki katika mafuriko kusini mwa India baada ya mvua kubwa kusababisha mito kufurika, kukata usafiri katika miji na vijiji.

  Watoto watano ni kati ya waliokufa.

  Kuna hofu idadi ya waliofariki inaweza kuongezeka zaidi kwani watu wengi hawajulikani waliko.

  Nyumba kadhaa zilisombwa na maji na watu walinaswa katika wilaya ya Kottayam katika jimbo la Kerala.

  Video kutoka eneo hilo ilionyesha abiria wa basi wakiokolewa baada ya gari lao kujaa maji ya mafuriko. Kottayam na Idukki ni wilaya mbili zilizoathirika zaidi katika jimbo hilo.

  Siku kadhaa za mvua kubwa pia zimesababisha maporomoko hatari ya ardhi.

 4. Mji

  Kila mtu anafikiria kuwa suluhu bora ni kujenga majengo yanayoelea majini katika sikuzijazo ili kuweza kukabiliana na kuongezeka kwa viwango vya maji ya bahari na hali mbaya ya hewa inayoendelea kusababisha maafa duniani.

  Soma Zaidi
  next
 5. Mafuriko ya Burundi: Viwango vya maji vyaongezeka Ziwa Tanganyika

  Uvuvi

  Majanga ya kiasili yamelazimisha zaidi ya watu 100,000 kutoroka makwao nchini Burundi ikatika miaka ya hivi karibuni, Shirika la watoato la Save the Children linasema.

  Baadhi yao walikua wakiishi kando ya Ziwa Tanganyika ambako viwango vya maji vimepanda kutokana na dhoruba kali, lililosababisha mafuriko na maporomoko ya ardhi.

  Watu walielezea kuamka usiku na kupata nyumba na mashamba yao yamesombwa na maji ya ziwa hilo, la pili kwa ukubwa duniani.

  Save the Children lilisema ni "mzozo uliosahaulika".

  Karibu 85% ya watu 122,500 wanaoishi katika makambi nchini Burundi wamehamishwa na majanga ya asili, badala ya mizozo, shirika hilo lilisema.

  Sababu nyingi zinachangia mafuriko, lakini hali ya joto inayosababishwa na mabadiliko ya hali ya hewa hufchangia uwezekano wa mvua nyingi.

  Viwango vya joto duniani tayarivimefikia nyuzi 1.2 tangu enzi ya viwanda ilipoanza na joto litaendelea kuongezeka endapo serikali ulimwenguni hazittadhibiti uzalishaji wa hewa ya kaboni.