Ukatoliki

 1. Wataalam wa Umoja wa Mataifa waitaka Vatican kukomesha unyanyasaji wa kingono dhidi ya watoto

  Papa

  Wataalam huru wanaofanya kazi na Umoja wa Mataifa wameyataka makao makuu ya Kanisa Katoliki Vatican kufanya juhudi zaidi kuzuia ghasia na unyanyasaji wa kingono dhidi ya watoto.

  Wataalamu hao wametoa wito huo wakielezea ‘’kuendelea kwa madai ya kuwepo kwa vizingiti na ukosefu wa ushirikiano ''kutoka kwa Kanisa Katoliki'', imesema ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa.

  Katika barua yao ya tarehe 7 Aprili ambayo ilitangazwa kwa umma Jumatatu wiki hii, wataalamu hao walielezea hitilafu katika juhudi za kanisa ikiwa ni pamoja na ''kuwalinda wakiukaji, kuficha uhalifu, kuzuia uwajibishwaji wa wanaodaiwa kutekeleza unyanyasaji, na kukwepa kulipa fidia wanazopaswa kupewa waathiriwa''.

  Kwa ujumla, wataalam wanadai baadhi wajumbe wa kanisa hilo wamekuwa wakizuia kwa makusudi juhudi katika sheria za nchi za kuwashitaki wahusika wa makosa ya unyanyasajii wa kingono wa watoto.

  Wataalam hao wameelezea kuwepo kwa harakati za kuweka ukomo wa muda ambao waathiriwa wanaweza kuripoti uhalifu waliotendewa baada ya kuwa watu wazima

  Wanasema unyanyasaji huo unadaiwa kutekelezwa zaidi ya miongo kadhaa katika nchi nyingi huku kukiwa na maelfu ya waathiriwa.

  Makao makuu ya Vatican hayajatoa tamko kwa umma kujibu barua hiyo.

  Mamlaka hiyo imekuwa ikikosolewa vikali kwa kushindwa kushighulikia unyanyasaji wa mkubwa wa waathiriwa unaofanyika katika nchi nyingi na kushindwa kuwaadhibu au kuwaondoa maaskofu, mapadre na viongozi wao wengine kuficha unyanyasaji wa kingono dhidi ya watoto.

 2. Video content

  Video caption: Kifo cha Rais Magufuli: Rastafari wa Mwanza wamfanyia ibada kiongozi huyo wa Tanzania

  Rastafari wa Mwanza wenye itikadi za kipekee wamefanya ibada maalumu ya kumuombea hayati Rais John Pombe Magufuli wakisisitiza alikuwa ni shujaa