Botswana

 1. Botswana kurejesha maelfu ya tembo Angola

  Botswana ina idadi kubwa ya ndovu duniani

  Botswana inasema inarejesha maelfu ya tembo nchini Angola.

  Nchi hiyo ya kusini mwa Afrika ina idadi kubwa ya tembo duniani inayokadiriwa kuwa 130,000.

  Lakini makumi ya maelfu ya tembo ni wakimbizi wa wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya mwaka 1975 na 2002.

  Na sasa hivi watarejeshwa nchini mwao kusini mwa Angola.

  Mbunge wa upinzani wa Botswana na mwanamazingira Kgoborego Nkawana amekiambia kipindi cha BBC Newsday kuwa tembo wana makazi katika sehemu kubwa Afrika kuanzia Zimbabwe, Zambia, Namibia hadi Angola.

  "Daima wamekuwa wakiishi katika maeneo hayo, lakini lazima waondolewe Angola kwasababu ya vita. Najua Angola imekuwa ikishirikiana na Umoja wa Ulaya kujaribu kuondoa mabomu ya ardhini katika baadhi ya sehemu," amesema.

  "Unachohitajika kujua ni kuwa tembo hukumbuka yaliyotokea nyuma na kila wakati hujaribu kuepuka maeneo yenye hatari..." aliongeza.

 2. Jiwe kubwa la almasi lagunduliwa Botswana

  Almasi

  Moja kati ya mawe makubwa ya almasilimechimbwa nchini Botswana na mchimbaji mdogowa Canada, ambaye ameendelea kugundua mawe makubwa.

  Kampuni ya Lucara Diamond Corp. imesema imebaini almasi nyeupe ya karati 998, na kufanya kuwa miongoni mwa mawe makubwa matano kuwahi kugunduliwa. Lucara amesema almasi hiyo itahitajika kuigawa vipande kabla ya kuisafisha.

  Mgodi wa Karowe umekuwa maarufu kwa kugundua mawe makubwa. Mwaka 2015, kampuni iligundua jiwe la karati 1,109 Lesedi La Rona , lililouzwa kwa dola milioni 53, na pia jiwe la karati 813 lililoweka rekodi ya kuuzwa kwa dola za Marekani milioni 63.

  Kwa mujibu wa gazeti la Bloomberg , Jiwe kubwa kabisa la almasi kuwahi kugunduliwa ni la karati 3,106 Cullinan, lililogunduliwa Nchini Afrika Kusini mwaka 1905.

  Kwa mujibu wa Forbes Lucara, ambayo iliuza mawe yake mawili mwakubwa kwaLouis Vuitton , imesema inafanya tathimini hatua zinazofuata na mshirika wake wa shughuli za kukata na kusafisha HB Antwerp.

 3. Video content

  Video caption: Nembo ya mchoro wa jicho kuwaokoa wafugaji

  Kwa kipindi cha miaka minne, wanasayansi na wafugaji kutoka Botswana na Australia wamekuwa wakiwachora ng'ombe katika makalio ili kuzuia wasivamiwe na simba.

 4. Video content

  Video caption: Je, chimbuko la binadamu wote ni Bostwana?

  Wanasayansi wamesema makao ya binadamu wote walio hai yako kusini mwa mto Zambezi huko Bostwana.