Italia

 1. Balozi wa Italia aliyeuawa DRC azikwa

  Luca Attanasio was shot dead apparently in a botched kidnapping attempt
  Image caption: Luca Attanasio alipigwa risasi na kuuawa katika jaribio lau utekaji nyara uliotibuka

  Mazishi ya kitaifa ya balozi wa Italia aliyeuawa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo yamefanyika mjini Rome.

  Luca Attanasio, mlinzi wake polisi wa Italia, Vittorio Iacovacci na derva raia wa DR Congo, Mustapha Milambo, waliuawa Jumatatu baada ya msafara wa magari ya Umoja wa Mataifa uliokuwa ukisafiri Mashariki mwa nchi hiyo DRC.

  Waziri Mkuu Italia, Mario Draghi, alikuwa miongoni mwa waombolezaji waliohudhuria ibada ya mazishi iliyofanyika katika kanisa la Santa Maria Degli Angeli.

  Serikali ya Congo imelaumu kundi la waasi wa Rwanda, FDLR. Waasi hao wamepinga madai hayo.

  Maelezo zaidi:

 2. Mwili wa balozi wa Italia umesafirishwa Roma kutoka DR Congo

  Jeneza lililobeba mwaili wa balozi wa Italia

  Mwili wa balozi wa Italia aliyeuawa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika jaribio la utekaji nyara uliotibuka siku ya Jumatatu, umesafirishwa mjini Rome.

  Luca Attanasio, mlinzi wake Vittorio Lacovacci, na dereva wake raia wa DR Congo Moustapha Milambo, waliuawa katika shambulio lililofanywa dhidi ya msafara wa magari ya chakula ya Umoja wa Mataifa, Mashariki mwa nchi hiyo.

  Ndege ya kijeshi ya Italia iliyokuwa imebeba majeneza mawili yaliyokuwa yamefunikwa bendera ya kitaifa ilitua katika uwanja wa ndege wa Ciampino mjini Rome na kupokelewa na Waziri Mkuu, Mario Draghi.

  Mamlaka nchini DR Congo zimelaumu kundi la waasi wa Rwanda la FDLR kwa mauaji.

  Kundi hilo limekanusha kuhusika na shambulio hilo.

  Maelezo zaidi:

 3. Mwili wa balozi wa Italia waagwa DRC

  Gavana wa Kivu Kaskazini Carly Nzanzu na mshauri mkuu wa Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wameongoza maafisa wengine kutoa heshima zao za mwisho kwa mwili wa balozi wa Italia nchini DRC, Luca Attanasio na mlinzi wake.

  Mwili wa marehemu unasafirishwa leo nchini Italia kutoka uwanja wa ndege wa Goma mashariki mwa DRC.

  Viongozi wa matabaka mbali mabili nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wakitoa heshima zao za mwisho kwa mwili wa marehemu balozi wa Italia na wahasiriwa wengine.
  Image caption: Gavana wa Kivu Kaskazini Carly Nzanzu kasivita akiongoza shughuli ya kuaga mwili wa balozi Luca

  Viongozi wa DRC na maafisa wa Italia wakishauriana kabla ya kuuaga mwili wa balozi wa Italia ambao unasafirishwa nyumbani leo.

  Viongozi wa DRC na maafisa wa Italia wakishauriana baada ya mwili wa balozi wa Italia kusafirishwa kutoka Goma mashariki mwa nchi hiyo.
  Image caption: Viongozi wa DRC na maafisa wa Italia wakishauriana

  Bw Luca Attanasio na mlinzi wake waliuawa baada ya msafara wa magari ya Umoja wa Mataifa kushambuiliwa siku ya Jumatatu mashariki mwa nchi hiyo.

  Ndege ilipowasili kutoka Goma
  Image caption: Ndege itakayosafirisha mwili wa balozi wa Italia kutoka DRC
 4. Waasi DRC wajitenga na mauaji ya mwanadiplomasia wa Italia

  Walinda usalama wa Umoja wa Mataifa

  Kundi la waasi la wa Rwanda (FDLR), limekanusha kuhusika na mauaji ya siku ya Jumatatu ya balozi wa Italia nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

  Luca Attanasio, 43, alifariki hospitalini kutokana na majeraha aliopata baada ya msafara wa magari ya Umoja wa mataifa kushambuliwa karibu na mji wa Goma mashariki mwa nchi hiyo.

  Afisa wa kijeshi alikuwa katika msafara huo pia aliuawa.

  Wizara ya mambo ya ndani ya DR Congo imelaumu kundi la waasi la FDLR kuhusika na mashambulio hayo.

  Lakini msemaji wa kundi hilo amekanusha madai hayo.

  “Zaidi ya makundi 100 yaliyojihami yanahudumu eneo hili, hatujui kwa nini wanatuhusisha na mauaji hayo. Hatukuhusika kwa njia yoyote na mashambulio hayo,” Cure Ngoma aliambia BBC.

  Pia unaweza kusoma:

 5. Ofisi ya Rais DRC yajiunga na uchunguzi wa mauaji ya balozi wa Italia

  Walinda amani wa Umoja wa Mataifa wamepelekwa katika eneo lililoshambuliwa
  Image caption: Walinda amani wa Umoja wa Mataifa wamepelekwa katika eneo lililoshambuliwa

  Maafisa kutoka ofisi ya rais nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wanatarajiwa kupelekwa mjini Goma kusaidia katika uchunguzi wa mauaji ya balozi wa Italia nchini humo.

  Maafisa hao wataondoka leo kuelekea Goma na watakuwa wakiwasilisha ripoti kwa za mara kwa mara kwa rais.

  "Mjumbe wa rais wa DRC atazuru [Italia] Jumanne ya leo Februari 23 kuwasilisha barua ya kibinafsi kwa rais wa baraza la Italia," Kulingana na ripoti kutoka kwa idara ya Idara ya habari ya rais.

  Katika ujumbe uliyochapishwa katika mtandao wa Twitter, Rais Félix Tshisekedi alisema alisikitishwana taarifa za kufuatia kuuawa kwa mwanadiplomasia wa Italia, Luca Attanasio.

  Alilaani shambulio la kigaidi lililolenga msafara wa magari ya Umoja wa Mataifa.

  Balozi Luca Attanasio alikuwa ameabiri gari la Shirika la Chakula Dunia (WFP).

  Rais amezitaka asasi husika kutoa maelezo kuhusiana shambulio hilo haraka iwezekanavyo ili waliyohusika wachukuliwe hatua za kisheria.

  Maelezo zaidi: