Afrika

 1. TB Joshua anasubiri 'sauti kutoka kwa Mungu'

  Mchungaji maarufu wa Nigeria, Temitope Balogun Joshua maarufu kama TB Joshua anasema anasubiri kusikia 'sauti ya Mungu' kabla hajafungua huduma za ibada katika jiji la biashara la Lagos.

  Follow
  next
 2. Abiria kutoka Tanzania, Afrika kusini kupimwa mara mbili virusi vya corona UAE

  Munira Hussein

  BBC Africa

  Tanzania, Afrika kusini, Nigeria, Iran na nchi nyingine zaidi ya ishirini, abiria wake wanatakiwa kupima mara mbili kipimo cha kuthibitisha kuwa hawana virusi vya corona ili waweze kuingia falme za kiarabu.

  Kwa mujibu wa gazeti la The National, utaratibu huo utaanza Agosti Mosi .

  Abiria kutoka maeneo hayo wanatakiwa kuwa na cheti cha kuonyesha kuwa hawana virusi vya corona, lakini pia watapimwa kwa mara nyingine wakifika falme za kiarabu.

  Pia watatakiwa wajitenge hadi pale majibu yatakapotoka.

  Na majibu yakija hawana virusi hivyo basi wataruhusiwa kuendelea na shughuli zao.

 3. Video content

  Video caption: Tundu Lissu azungumza na BBC baada ya kurejea nyumbani, Tanzania?

  Siku mbili baada ya kiongozi wa upinzani nchini Tanzania Tundu Lissu kuwasili nchini Mwake Tanzania akitokea Ubelgji kwa matibabu, ameielezea BBC juu ya hisia zake.