Ugiriki

 1. Kasisi akamatwa kwa kuwashambulia maaskofu kwa tindikali

  Polisi

  Kasisi mmoja amekamatwa mjini Athens baada ya kuwasahambulia maaskofu saba wa kanisa la Othodox nchini Ugiriki, polisi wanasema.

  Shambulio hilo lilitokea wakati wa kikao cha nidhamu dhidi ya kasisi huyo mwenye umri wa miaka 36 siku ya Jumatano, kulingana na polisi.

  Maaskofu hao watatu waliochomeka vibaya hasa usoni wanapokea matibabu hospitalini.

  Polisi aliyejaribu kuwasaidia pia alikimbizwa hospitali.

  Mshukiwa, kasisi ambaye anakabiliwa na hatari ya kufurushwa kutoka kwa kanisa hilo, alituhumiwa kw akuhusika na ulanguzi wa dawa za kulevya, kwa mujibu wa shirika la habari la ANA.

  Maaskofu walikuwa wanakutana kujadili mienendo yake baada ya kudaiwa kupatikana na gramu 1.8 ya dawa ya kulevya aina ya cocaine mwezi Juni 2018, kulingana na vyambo vya habari nchini Ugiriki.

  Kasisi huyo alikuwa amenunua "chupa kubwa iliyojaa tindikali" na kwenda nayo katika kikao kilichokuwa kikifanyika ukumbi wa Petraki Monastery mjini Athens, gazeti la Ta Nea liliripoti.

  Mlinzi aliyefanikiwa kumkamata kasisi huyo katika langoni, pia alichomeka kwa tindikali na kupelekwa hospitali.

 2. Video content

  Video caption: Moto wateketeza kambi kubwa ya wakimbizi Ugiriki

  Moto wateketeza kambi kubwa ya wahamiaji nchini Ugiriki, na maelfu wakusanyika katika kisiwa cha Lesbos.

 3. Video content

  Video caption: Walinzi wa mbambao wa Ugiriki walivyofyatua risasi kuwazuwia wahamiaji kuendelea na safari

  Picha za video zimepatikana za walinzi wa mwambao wa Ugiriki wakifyatua risasi ndani ya eneo la bahari karibu na mashua ya wahamiaji waliotoka Uturuki.