Silaha za Nyuklia

 1. Mwanaharakati, Dkt.Cyrilo aachiwa kwa dhamana

  Mwanaharakati wa kimtandao nchini Tanzania anayefahamika kwa jina la Dkt.Cyrilo Christopher ambaye ni Daktari wa binadamu pia mwandishi wa vitabu aliyekuwa akishikiliwa katika kituo cha polisi cha Kati Jijini Dar es salaam leo Jumatano ameachiwa kwa dhamana.

  Soma Zaidi
  next
 2. Korea Kaskazini:Aukus inaweza kuchochea 'nchi kukimbilia kujihami na zana za kinyuklia

  Kim Jong-un
  Image caption: Picha ya Kim Jong-un kutoka maktaba

  "Korea Kaskazini imekosoa mkataba mpya wa usalama kati ya Marekani, Uingereza na Australia, ikisema unaweza kusababisha "nchi kukimbilia kujihami na zana za kinyuklia."

  Afisa wa wizara ya mambo ya nje alisema makubaliano ya Aukus "yatasumbua usawa wa kimkakati katika eneo la Asia-Pasifik."

  Mkataba huo utajumuisha Marekani na Uingereza zikiipa Australia teknolojia ya kujenga nyambizi zinazotumia nyuklia.

  Inatazamwa sana kama juhudi ya kukabiliana na ushawishi wa China katika Bahari ya China Kusini inayozozaniwa.

  Mkataba wa Aukus ulitangazwa wiki iliyopita na pia utajumuisha makombora ya meli, akili ya bandia na teknolojia zingine.

  "Hivi ni vitendo visivyofaa na vya hatari ambavyo vitasumbua usawa wa kimkakati katika eneo la Asia-Pasifiki na kusababisha kila nchi kukimbilia kuwa na silaha za nyuklia," amesema afisa wa wizara ya mambo ya nje ya DPRK akirejelea makubaliano ya usalama.

  Wiki iliyopita, Korea Kaskazini ilifanya majaribio mawili makubwa ya silaha - lile la kombora la masafa marefu na kombora la balistiki.

  China pia imekosoa makubaliano hayo na msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Beijing Zhao Lijian amesema muungano huo unahatarisha "kuharibu kabisa amani ya eneo ... na kuimarisha juhudi za kujihami kwa silaha za nyuklia.

  Pyongyang ilisema ni "kawaida kabisa kwa nchi jirani [kama] China kulaani vitendo hivi kama kutowajibika kwa kuharibu amani na utulivu wa eneo hilo."

  Matarajio ya mkataba huo ni kuona Marekani ikishirikisha wengine teknolojia yake ya nyambizi kwa mara ya kwanza katika miaka 60, hapo awali ikiwa ilishirikisha Uingereza mara moja tu.

  Ni nchi gani zilizo na nyambizi?

  Nchi zilizo na nyambizi
  Image caption: Nchi zilizo na nyambizi

  Inamaanisha Australia itaweza kujenga nyambizi zenye nguvu za nyuklia ambazo ni haraka mno na ngumu kuzigundua kuliko meli za kawaida.

  Zinaweza kukaa ndani ya maji kwa miezi kadhaa na kudungua makombora ya umbali mrefu - ingawa Australia inasema haina nia ya kuweka silaha za nyuklia ndani yake.

  China haikutajwa moja kwa moja wakati wa tangazo la mpangilio wa usalama.

  Hata hivyo, viongozi wa nchi hizo tatu walitaja mara kwa mara masuala ya usalama wa kikanda ambayo "yameongezeka sana".

  Korea Kaskazini pia ilirejelea taarifa ya hapo awali iliyotolewa na Ufaransa, ambayo ilitaja makubaliano hayo kuwa "usaliti," na kusema kwamba mkataba huo umesababisha "mgogoro mkubwa" kati ya washirika.

  Ufaransa imekuwa ikikosoa mkataba wa Aukus kwasababu ilifikisha ukomo wa makubaliano yenye thamani ya $ 37bn (£ 27bn) yaliyosainiwa na Australia mnamo mwaka 2016 kwa Ufaransa kujenga nyambizi 12 za kawaida.

  Ufaransa inasema iliarifiwa juu ya makubaliano hayo saa chache kabla ya tangazo rasmi kwa umma kutolewa.