Haki za wachache na wanaotengwa

 1. Video content

  Video caption: Dontae Sharpe: 'Mapambano yangu ya miaka 26-kuthibitisha sina hatia'

  Lakini kuthibitisha kuwa hana makosa ilikuwa hatua ya kwanza kuelekea uhuru wa kweli.

 2. Marekani yasema 'mauaji ya kikabila' yalifanyika Tigray

  Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Antony Blinken, amesema watu katika jimbo la Tigray kaskazini mwa Ethiopia wanakabiliwa na kile alichotaja kuwa mauaji ya kikabila.

  Akitoa ushahidi mbele ya kamati ya bunge, alitoa wito kwa serikali ya Ethiopia komesha hali hiyo na kukomesha ukiukwaji wa haki za binadamu katika eneo hilo.

  Bw. Blinken amesema wanajeshi wa Eritrea na wanamgambo wa Ethiopia lazima waondoke Tigray. "Kama mnavyojua, tuna vikosi kutoka Eritrea katika eneo hilo na hali kadhalika vikosi vya wapiganaji kutoka jimbo jirani la Amhara. Wanahitaji kuondoka ili kikosi ambacho hakitakiuka haki za binadamu za watu wa Tigray au kutekeleza visa vyamauaji kupelekwa huko, yale tuliyoona magharibi mwa Tigray, lazima yakomeshwe," alisema.

  "Pia tunataka uwajibikaji kamili na uchunguzi huru wa kubaini ni nini hasa kilichotokea huko."

  Mapema mwezi huu alitoa wito kwa mamlaka mjini Addis Ababa kuruhusu uchunguzi ufanyike dhidi ya madai ya ukatili uliotekelezwa katika hilo.

  Serikali ya Ethiopia imepuuzilia mbali ukosoaji wa Marekani, ikisema mapigano ya Tigray ni suala la ndani.

 3. Video content

  Video caption: Changamoto kwa watu walemavu kupata mkopo nchini Tanzania

  Halmashauri zote nchini Tanzania zinapaswa kutenga asilimia mbili ya mapato yake kwa ajili ya walemavu