Unyanyasaji wa Kingono

 1. Video content

  Video caption: Hatari ya mafundisho potofu kuhusu mahusino ya ngono mitandaoni

  Mafundisho kuhusu mahusiano na ngono shuleni huibua mjadala ,lakini daktari mmoja huko Wales Uingereza anasema Watoto kupitia video za ponografia wakupotoshwa kuhusu ngono.

 2. A campaign against child sexual abuse in India

  Mahakama ya juu zaidi nchini India imebatilisha uamuzi tata wa mahakama kuu wa kufuta kosa la ukatili wa kingono mwanaume aliyetuhumiwa kumbaka ya msichana mwenye umri wa miaka 12 kwasababu "hapakuwa na mgusano wa mwili -kwa mwili'' na muathiriwa.

  Soma Zaidi
  next
 3. Zaidi ya watoto 6000 walikabiliwa na unyanyasaji Tanzania katika kipindi cha miezi tisa mwaka huu

  N

  Naibu waziri wa mambo ya ndani wa nchini Tanzania Khamis Chilo amelifahamisha Bunge la nchi hiyo kwamba jumla ya watoto 6,168 wa Tanzania walikabiliwa na aina tofauti za unyanyasaji kati ya Januari na Septemba mwaka 2021.

  Bw. Chiko alikuwa akijibu swali la Mbunge wa viti maalum Bi Esther Matiko siku ya Ijumaa ambaye alitaka kujua idadi ya watoto na waathirika wa ghasia nchini Tanzania katika kipindi hicho.

  Katika jibu lake, Bw Chilo alisema kati ya 6168 walioathirika wanawake walikuwa 5287 na wanaume wakiwa 881 akiongezea kwamba 3524 kati yao walibakwa huku 637 wakilawitiwa

  Bw. Chiko alisema karibu washukiwa 3,800 wamekamatwa na kesi 2,368 zinaendelea katika mahakama tofauti nchini na hukumu za kesi 88 zimetolewa.

 4. Video content

  Video caption: Tutawahi kupata haki?-Raia wa Gambia

  Ni miaka minne sasa tangu Yahya Jammeh ,kiongozi aliyetawala Gambia kwa miaka 22 kukimbia nchi yake.

 5. Mwanataaluma asimamishwa kazi Tanzania kwa tuhuma za rushwa ya ngono

  University of Dodoma

  Chuo Kikuu cha Dodoma(UDOM) nchini Tanzania kimetoa taarifa kwa umma kujibu tuhuma dhidi ya mwanataaluma wa chuo hicho.

  Taarifa hiyo inasema "chuo kilipokea kwa masikitiko makubwa taarifa za tuhuma dhidi ya mtumishi wake ndugu Petro Bazil Mswahili ambaye ni Mwanataaluma juu ya kujihusisha na rushwa ya ngono kinyume na maadili ya Utumishi wa Umma".

  Chuo hicho kimesema, mwalimu huyo amesimamishwa majukumu yake yote kuanzia Oktoba 25 mwaka huu hadi uchunguzi utakapokamilika.

  Tayari , Chuo kimeanzisha mchakato wa hatua za kinidhamu na maadili kulingana na sheria na kanuni za utumishi wa umma.

  Aidha, Chuo kinapenda kuutaarifu Umma kuwa kitendo hiki hakivumiliki wala kukubalika na kwamba wakati wote Chuo kitaendelea kusimamia nidhamu na maadili kwa watumishi wake wote.

  Pia, Chuo kitaendelea kuchukua hatua kali kwa mtumishi yeyote atakayebainika kujihusisha na makosa ya kinidhamu. Chuo kimesikitishwa sana kwa usumbufu uliojitokeza.

 6. Video content

  Video caption: Ipi dhana ya udhalilishaji wa kingono?

  Makala haya yanaangazia suala la unyanyasaji wa Kingono nchini Tanzania na kuonesha namna vitendo hivyo vinavyoweza kuleta athari kwa jamii kama visipoepukwa.