Uchukuzi wa Reli

 1. Nigeria yasitisha huduma ya reli baada ya shambulio

  N

  Shirika la reli la Nigeria limesitisha kwa muda huduma za reli kutoka Abuja, kuelekea kaskazini magharibi mwa Kaduna baada ya watu wenye silaha kuwavamia abiria wa treni siku ya Jumatano.

  Watu walioshuhudia walisema washambuliaji hao walimlenga dereva wa treni ingawa hakuna majeruhi alireripotiwa mpaka sasa.

  Abiria mmoja aliiambia BBC kuwa walisikia mlio mkubwa kabla ya treni haijasimama kwa saa kadhaa.

  Mbunge wa zamani nchini humo, Senata Shehu Sani, aliandika kwenda tweeter kuwa treni ya pili na hivyo kulazimika kurudi Abuja siku ya Alhamisi baada ya mlipuko ulipotokea katika reli hiyo.

  Kampuni ya reli ya Nigeria ilisema huduma hizo zitarudi baada baada ya Ijumaa baada ya ukarabati..

 2. Watu 36 wafariki katika ajali ya treni Pakistan

  At least 30 people have died in the crash, and several more are in a critical condition
  Image caption: Watu kadhaa pia wameripotiwa kuwa katika hali mahututi

  Treni mbili za abiria zimegongana kusini mwa Pakistan, na kuua watu takriban 36 na wengine kadhaa kujeruhiwa.

  Maafisa walisema kuwa gari moshi moja lililokuwa likisafiri kwenda mkoa wa Sindh lilikuwa limepoteza mkondo na kuanguka katika njia ya reli. Treni ya pili iliyokuwa na abiria kisha iligongana nayo na kupinduka.

  Timu za uokoaji ziliwapeleka majeruhi katika hospitali za karibu na inadhaniwa kuwa watu kadhaa wako katika hali mbaya.

  Pakistan imeshuhudia msururu wa ajali mbaya za treni katika miaka iliyopita.

  Kati ya 2013 na 2019, watu 150 walikufa katika ajali kama hizo, kulingana na ripoti za vyombo vya habari nchini humo.

  Afisa mwandamizi katika wilaya ya Ghokti, Usman Abdullah, aliliambia shirika la habari la Reuters kwamba ni vigumu kujua ni watu wangapi bado wamenaswa katika treni hizo.

 3. Video content

  Video caption: Mzee wa miaka 66 aokolewa na polisi

  Afisa wa polisi afanya uamuzi wa haraka wa kumuokoa mzee wa miaka 66 , kugongwa na treni

 4. Video content

  Video caption: Corona: India kutumia mabehewa 500 ya treni kama vyumba vya wagonjwa

  India kwa sasa imesema itageuza mabogi ya treni 500 kutoa nafasi ya kuweka vitanda elfu 8 vya wagonjwa wa virusi vya corona.