Uvumbuzi

 1. Wasafiri wa chombo kipya cha Shepard(Kushoto kwenda kulia): Mark Bezos, Jeff Bezos, Oliver Daemen, Wally Funk.

  Hatua kubwa imepigwa katika harakati za biashara kwenda anga za mbali siku ya Jumanne baada ya bilionea Jeff Bezos kupaa na kuvuka mpaka wa angani unaojulikana kama mstari wa Kármán kwa kutumia roketi yake mwenyewe.

  Soma Zaidi
  next
 2. Video content

  Video caption: Mbunifu wa mitindo anavyotengeza nguo kutokana taka za plastiki

  Elisha Ofori Bamfo, mbunifu wa mitindo nchini Ghana amepata suluhisho ambalo linaweza kusaidia tu

 3. Video content

  Video caption: Je umewahi kufikiri kuwa mabaki ya nywele unazonyoa yanaweza kutumika kutengeneza bidhaa?

  David Daudi na Ojung’u Jackson wameanzisha kampuni ya (Cutoff recycle) ambayo wanatumia mabaki ya nywele za binadamu kuongeza nguvu kwenye matofali.

 4. Video content

  Video caption: Wataalamu nyota wagundua mizunguko isiyo ya kawaida ya miangwi ya radio

  Kifaa kipya chenye nguvu za kuvuta picha za mbali angani kimewawezesha wataalamu wa nyota kuvumbua kitu kipya katika anga za mbali ''mizunguko isiyo ya kawaida ''

 5. Video content

  Video caption: Uzinduzi wa BBC 100 Women

  Ungana nasi mubashara katika uzinduzi wa BBC 100 Women

 6. Raia wa Ghana awa mwanamke wa kwanza Afrika kushinda tuzo ya uhandisi

  Charlette N’Guessan
  Image caption: Charlette N’Guessan

  Mfanyabiashara wa teknolojia nchini Ghana Charlette N’Guessan, ameshinda tuzo ya mwaka huu ya uhandisi Afrika.

  Charlette N’Guessan ni mwanamke wa kwanza barani Afrika kushinda tuzo hiyo na wa kwanza kutoka Ghana.

  Bi N’Guessan mwenye umri wa miaka 26 na kundi lake la wavumbuzi, Bace API, wanatumia utambuzi wa usoni na akili bandia kuthibitisha utambulisho kwa mbali, ilisema taasisi ya uhandisi ya Royal Academy.

  Inatumia picha za moja kwa moja ama video fupi zilizonaswa kwa kutumia kamera ya simu kutambua ikiwa picha hiyo ni ya mtu halisi, ama picha ya kitu kilichopo.

  Taasisi mbili za kiuchumi tayari zinatumia programu hiyo kuthibitisha utambulisho wa wateja wao.

  Bi N’Guessan alipewa zawadi ya dola 33,000 kwa kuibuka mshindi.

  Mshindi alipigiwa kura na watazamaji wa moja kwa moja wakati wa hafla ya tuzo iliyofanyika Alhamisi ambapo wahitimu wanne waliwasilisha kazi zao.