Msumbiji

 1. Mashambulizi ya kijeshi Msumbiji 'yanayokabiliwa na changamoto'

  Mwezi uliopita Rwanda ilituma wanajeshi wake 1,000 kwenda Msumbiji kupigana na wanamgambo
  Image caption: Mwezi uliopita Rwanda ilituma wanajeshi wake 1,000 kwenda Msumbiji kupigana na wanamgambo

  Mkuu wa jeshi la Msumbiji amesema shambulio linaloendelea katika mkoa wa kaskazini wa Cabo Delgado limekabiliwa na upinzani kidogo kwasababu wapiganaji walioko huko labda huenda walitupilia mbali silaha zao na kujifanya kama raia.

  "Ndiyo sababu tunaendelea kuwafuata na kufanya uchunguzi kwa yeyote anayewasili haswa wale wanaodai wanatoka Palma, ambako kwa muda mrefu hadi hivi karibuni eneo hilo lilikuwa halina watu," Brigedia Chongo Vidgal aliiambia televisheni inayomilikiwa na serikali Jumapili usiku.

  Alisema "asilimia 95 ya wanamgambo walikuwa Msumbiji.

  Mwaka jana kikundi hicho kiliteka mji wenye kuongoza kwa gesi wa Palma na mji wa bandari wa kimkakati wa Mocímboa da Praia.

  Eneo la Mocímboa da Praia lilitekwa tena wiki iliyopita baada ya kampeni iliyoongozwa na wanajeshi wa Rwanda ambao walipelekwa mkoa huo mwezi uliopita kama sehemu ya makubaliano ya nchi mbili.

  Brigedia Vidgal alisema wanajeshi wa Rwanda walikuwa na vifaa bora na kuongeza kuwa wanajeshi wa Msumbiji "wana hisia kubwa ya uzalendo" na walikuwa wakifanya kazi kwa karibu na wenzao.

  Alisema pia kwamba wanajeshi wa Rwanda walikuwa wepesi kutoa taarifa kuhusu ujumbe huo, ikiwemo kushirikishana picha za wanajeshi kwasababu walikuwa na waandishi wa habari ndani ya jeshi.

  "Sisi pia tuko tunakaribisha waandishi wa habari wa kitaifa kufuata mfano huo," alisema.

  Nchi wanachama katika kambi ya ukanda wa kusini mwa Afrika, Sadc, pia wamejiunga na juhudi za kupambana na wanamgambo wa Kiislam kaskazini mwa Msumbiji.

  Zaidi ya watu 3,000 wameuawa huku wengine 820,000 wakitoroka makazi yao tangu kuanza kwa uasi huko Cabo Delgado mnamo mwaka 2017.

 2. Rais wa zamani wa Msumbiji ahimiza mazungumzo na makundi yenye silaha

  Joaquim Chissano anasema sababu za vurugu za silaha huko Cabo Delgado lazima zichunguzwe
  Image caption: Joaquim Chissano anasema sababu za vurugu za silaha huko Cabo Delgado lazima zichunguzwe

  Rais wa zamani wa Msumbiji Joaquim Chissano ametoa wito kwa serikali kutathmini uwezekano wa kujadiliana na makundi yenye silaha yanayohudumu katika eneo la Cabo Delgado linalokumbwa na mzozo.

  Anasema kuna “aina flani ya ugaidi” ambao umekomeshwa kupitia majadiliano.

  “Huenda pengine kiongozi wa kundi hilo naonesha ishara ya kutaka kutupatia nafasi ya majadiliano ambayo yatasaidia kumaliza” ghasia za silaha,alikiambia kituo cha Radio Mozambique kinachomilikiwa na serikali, katika mahojiano siku ya Jumatano.

  Rais huyo wa zamani wa Msumbiji alisema sababu za vurugu za silaha huko Cabo Delgado lazima zichunguzwe kama njia ya kutatua mzozo wa kijeshi na kijamii katika jimbo hilo.

  Bwana Chissano alikuwa rais wa Msumbiji kati ya 1986 na 2005. Aliongoza mazungumzo ya mafanikio na waasi wa zamani wa upinzani wa Msumbiji (Renamo), ambayo yalimaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe vya miaka 16 mwaka 1992.

  Rais wa sasa, Filipe Nyusi, ameelezea nia yake ya kujadiliana na vikundi vyenye silaha lakini amelalamika kuwa waasi hawajaonesha "ishara" ya kukaribisha mazungumzo hayo.

  Mkoa wa Cabo Delgado umetumbia kwenye ghasia tangu mwaka 2017, baadhi ya mashambulio yakidaiwa kufanywa na kundi la Islamic State.

  Mashambulio hayo kufikia sasa yamesababisha vifo vya zaidi ya watu 3,000 na wengine zaidi ya 800,000 kufurushwa makwao.

  Soma zaidi:

 3. Kampuni ya mafuta ya Msumbiji yakana kumwaga mafuta baharini

  Angalau lita 10,000 za mafuta zimemwagika
  Image caption: Angalau lita 10,000 za mafuta zimemwagika

  Kampuni ya kusambaza mafuta inayomilikiwa na serikali ya Msumbiji, Petromoc, imekanusha kuhusika na umwagaji wa mafuta ulitokea mwishoni mwa wiki katika bandari ya Pemba, karibu na pwani ya mkoa wa Cabo Delgado.

  Mwenyekiti wa bodi ya kampuni hiyo Hélder Chambisse amesema kuna maelezo finyu kuhusu chanzo cha mafuta hayo yaliyomwagika bahari.

  Alisema laiti kampuni hiyo ilihusika mamlaka katika eneo hilo ingeliwaarifu.

  Bw. Chambisse amesema uchunguzi unaendelea kufahamu kilichosababisha umwagikaji huo.

  Inakadiriwa kwamba umwagikaji huo umesababisha hasara ya karibu lita 10,000 za mafuta.

  Kisa hicho kimevutia umati mkubwa wa watu wakiwemo wanawake na watoto, ambao wanahatarisha maisha yao kuchota mafuta kwenye mitungi.

  Polisi wamepelekwa eneo hilo kudhibiti watu.

 4. Wanajeshi wa Rwanda wawaua wanamgambo wa kjihadi Msumbiji

  Wanajeshi kutoka nchitofauti za Afrika wanapelekwa Msumbij
  Image caption: Wanajeshi kutoka nchitofauti za Afrika wanapelekwa Msumbiji

  Vikosi vya Rwanda vilivyotumwa kusaidia kukabiliana na waasi vimewauwa wanamgambo wa kijihadi wasiopungua 30, maafisa wa usalama nchini Msumbiji wanasema.

  Maafisa hao wanasema wanajeshi walikuwa wakiifanya oparesheni ya usalama katika msitu wa karibu na mji wa bandari wa Palma walipokutana na wanamgambo hao.

  Karibu wanajeshi 1,000 wa Rwanda walipelekwa nchini Msumbiji mapema mwezi huu.

  Jumuia ya maendeleo ya mataifa ya kusini mwa Afrika (SADC) imepeleka wanajeshi wake nchini humo na vikosi vya Ureno vinasaidia kutoa mafunzo kwa wanajeshi wa Msumbiji.

  Karibu watu 800,000 wamefurushwa makwao kutokana na ghasia hizo zilizodumu miaka minne.

  Maelfu ya watu wameuawa na wengine wengi kukatwa vichwa.

  Soma zaidi:

 5. Uporaji Afrika Kusini: Lori za Msumbiji zachomwa moto

  mm

  Lori zinazomilikiwa na raia wa Msumbiji zimeporwa na kuchomwa moto na waandamanaji katika nchi jirani ya Afrika Kusini, chama cha wasafirishaji mizigo Msumbiji kinasema.

  Shirikisho la Chama cha Usafiri Barabarani (Fematro) linasema hakuna majeruhiwa au vifo vilivyoripotiwa miongoni mwa madereva.

  Kisa hicho kilitokea mjini Durban, mkoa wa KwaZulu-Natal, ana kwengineko mkoani Gauteng, alisema Constantino Jotamo, mkurugenzi wa Fematro director.

  "Tunatafuta maelezo zaidi kuhusu kile kilichotokea," alisema

  Madereva wanahofia hali huenda ikaendelea kuwa mbaya zaidi katika siku zijazo.

  "Siku chache zilizopita zimekuwa ngumu sana,” anasema Rui Muianga, dereva wa lori katika barbara ya Maputo-Johannesburg.

  Siku ya Jumanne, ni magari matatu pekee ya usafiri wa umma ziliondoka Msumbiji hadi Afrika Kusini

 6. Mashambulizi mapya ya wanamgambo yaripotiwa Msumbiji

  The insurgency has created a humanitarian crisis with many displaced from their homes

  Wanamgambo wa kijihadi wamehusika tena katika mashambulio mapya karibu mji wa Palma kaskazini mwa Msumbiji, vyanzo vya habari vya jeshi vimeliambia shirika la habari la AFP.

  Shambulio hilo linakuja wakati ambapo nchi za kusini mwa Afrika zimeishinisha kupelekwa kwa kikosi maalum kusaidia Msumbijikukabiliana na wanamgambo hao.

  "Wanamgambo hao walijaribu kushambulia ngome za vikosi vya serikali mjini in Patacua, karibu na eneo la Afungi LNG lakini walirudishwa nyuma baada ya kupatikana kwa msaada kutoka angani," shirika la habari la AFP lilinukuu vyanzo vya habari vikisema.

  Mkoa wa kaskazini Cabo Delgado kwa muda mrefu umekuwa ukikabiliwa na changamoto kadhaa lakini uvamizi kutoka kwa wanamgambo wa kijihadi ulianza mwaka 2017.

  Mzozo huo umevuti ajamii ya kimataifa baada ya wanamgambo kuteka mji wa Palma mwezi April, kuua raia wa kigeni na kukwamisha mradi wa gesi asilia wa thamani ya dola bilioni 20 za Kimarekani.

  Mashambuilo ya wanamgambo yamesababisha mzozo mkubwa wakibinadamu, huku watu waliofurushwa makwaowakiishi katika kambi za wakimbizi karibu na mikoa inayozunguka Cabo Delgado.

 7. Ripoti ya ukahaba katika gereza la Msumbiji kuchunguzwa

  Mwanamke

  Waziri wa sheria wa Msumbiji anatarajiwa kuanzisha uchunguzi kuhusu ripoti kuwa maafisa wa magereza katika jela ya wanawake wamekuwa wakiwalazimisha wafungwa kufanya ukahaba.

  Shirika la kupambana na ufisadi na uadilifu wa umma limefichua kuwa kwa miaka kadhaa sasa, wafungwa wa gereza la Ndlavela lililoko mji mkuu wa nchi hiyo Maputo wamekuwa wakipelekwa katika madanguro yaliopo karibu na gereza hilo kufanyishwa ukahaba.

  Waandishi wa habari wanaofanya taarifa za upelelezi walizungumza na baadhi ya wafungwa wa zamani na walioko sasa gerezani humo ambao wamesema walilazimishwa kufanya ngono na watu nje ya jela hiyo mara kadhaa kwa wiki.

  Inadaiwa kuwa maaskari wa jela hiyo walikuwa wakilipwa kati ya dola hamsini na mia tano na kila mteja.

  Wafungwa hao wanasema walipokataa kutumika kingono, walipigwa au kuadhibiwa kwa kufanyishwa kazi ngumu gerezani.

 8. Tanzania yawarejesha nyumbani wakimbizi wanaotoroka ghasia Msumbiji

  Thousands have been forced to flee their homes
  Image caption: Maelfu ya watu wamelazimika kutoroka makwao

  Mamlaka nchini Msumbiji zimesema kuwa zaidi ya raia 9,600 wa Msumbiji wanaokimbia vurugu kaskazini mwa Jimbo la Cabo Delgado "wamerudishwa kwa nguvu" kutoka Tanzania tangu Januari 2021, Diario de Noticias gazeti binafsi nchini humo limeripoti.

  Kulingana na Shirika la Wakimbizi la Umoja wa Mataifa karibu watu 900 "walisukumwa kwa lazima" kuvuka mpaka kati ya tarehe 7 na 9 Juni.

  Ripoti hiyo inakuja saa chache baada ya manusura walionukuliwa na tovuti inayomilikiwa na watu binafsi O Pais, kufichua kwamba mji wa Palma kaskazini mwa Msumbiji, ulibaki ukikaliwa na wanamgambo, ambao wanachama wao wanaendelea "kuchoma nyumba, kuua na kuteka nyara watu".

  Mashambulio makubwa ya hivi karibuni ya kundi hilo dhidi ya mji wa Palma mnamo 24 Machi, yaliwahamisha zaidi ya watu 70,000, na kuongeza idadi ya watu waliohamishwa kutokana na ghasia kaskazini mwa Msumbiji hadi karibu 800,000.

  Mnamo mwezi Aprli Waziri wa Mambo ya Ndani wa Tanzania George Simbachewene alisema kuwa Ripoti ya Umoja wa mataifa juu ya Tanzania kurudisha wakimbizi wa Msumbuji haina uhalisia wowote.

  Katika mahojiano na BBC Simbachawene alisisitiza kuwa Tanzania inalinda mipaka yake na kujilinda dhidi ya magaidi ambao wakati mwingine wanaweza kujichanganya na wakimbizi na kisha kuingia nchini.

  Maelezo zaidi: