Cameroon

 1. Samuel Eto atangaza kugombea urais wa shirikisho la soka Cameroon.

  Samuel Eto'o
  Image caption: Samuel Eto'o alifunga magoli 56 katika michuano 118 kama mchezaji wa Cameroon

  Nyota wa mpira wa soka nchini Cameroon Samuel Eto atangaza kugombea urais wa shirikisho la mpira wa miguu nchini Cameroon.

  Tangazo hilo limetolewa Jumanne katika ukurasa wake rasmi wa Facebook.

  "Nimeamua kuchukua uamuzi huu kwasababu ya kuipenda Cameroon na kupenda soka yetu", alielezea Samuel Eto katika taarifa yake.

  Aliandika pia, "ni wakati wa kujenga upya mpira wetu".

  Baada ya uvumi kadhaa, Eto ameamua kuwa mgombea wakati kuna utata juu ya marufuku ya uraia mara mbili nchini Cameroon.

  Samuel Eto alikuwa raia wa Uhispania wakati alikuwa akichezea Uhispania.

  Miongoni mwa masharti yanayotakiwa kuwa mgombea wa urais wa shirikisho la mpira wa miguu la Cameroon, ni marufuku ya kuwa na utaifa wa kigeni.

  Samuel Eto ni kigogo wa tatu wa zamani kugombea urais wa shirikisho la mpira wa miguu nchini Cameroon.

  Hata hivyo, bado haijulikani ikiwa ugombea wake utathibitishwa.

  Uchaguzi umepangwa kufanyika Desemba 11.

  Pia unaweza kusoma:

  Eto’o apewa kazi ya ukufunzi Uturuki

 2. Kikosi cha Cameroon mwaka 1990 kilikuwa cha kwanza kufika hatua ya robo-fainali katika michuano ya kombe la dunia

  Kikosi cha Cameroon kilichoshiriki kombe la Dunia 1990 kuzawadiwa nyumba walizoahidiwa miaka 30 iliyopita. Hatua hii inafikiwa wakati wachezaji watatu , Louis Paul Mfede, Benjamin Massing na Stephen Tataw wakiwa wameaga dunia.

  Soma Zaidi
  next