Eritrea

 1. Wanajeshi wa Eritrea wataondoka hivi karibuni - mjumbe wa UN Ethiopia

  Tigray has been devastated by a humanitarian crisis since fighting began in 2020

  Wanajeshi wa Eritrea ambao wamekuwa wakipigana katika jimbo la Tigray kaskazini mwa Ethiopia wataondoka hivi ''karibuni'' Balozi wa Ethiopia katika umoja wa Mataifa amesema.

  Taye Atske Sellasie Made amesema ''kinachoendelea kwa sasa ni kushughulikia masuala kadhaa muhimu” kabla hawajaondoka, shirika la habari la Reuters liliripoti.

  Mjumbe huyo alisema serikali ya Ethiopia imeonesha utashi "na Waeritrea pia wako wazi", shirika la habari la AP limemnukuu kusema.

  Alizungumza baada ya mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ambapo mkuu wa maswala ya binadamu wa Umoja wa Mataifa Mark Lowcock alisema “si ajabu tukashuhudia tena” baa la njaa la mwaka 1984 ghasia isipokomeshwa na wanajeshi wa Eritrea kuondoka.

  Wiki iliyopita, mkuu wa misaada wa Umoja wa Mataifa(UN), alisema kuna njaa kaskazini mwa Ethiopia baada ya kutolewa kwa uchambuzi ulioungwa mkono na UN kuhusu hali hiyo.

  Serikali ya Ethiopia imekanusha kwamba kuna njaa nchini humo.

  Tigray imekuwa ikikabiliwa na mzozo wa kibinadamu tangu mapigano yalipoanza mnamo Novemba 2020 kati ya vikosi vya serikali na waasi.

  Maelfu ya watu wanasadikiwa kuuawa na wengine milioni 1.7 kuhama makazi yao.

  Mzozo Tigray uliodumu kwa miezi saba umewafanya wote waliohusika, pamoja na wanajeshi wa Eritrea, kutuhumiwa kwa ukiukaji mkubwa wa haki kama vile ubakaji na mauaji ya kiholela.

  Soma zaidi:

  Mzozo wa Tigray: Jukumu la Eritrea katika mzozo wa Ethiopia

 2. Marekani yaiwekea vikwazo Ethiopia juu ya mzozo wa Tigray

  Maelfu ya watu wameuawa na wengine kadhaa kuachwa bila makao tangu mzozo ulipozuka miezi sita iliyopita.
  Image caption: Maelfu ya watu wameuawa na wengine kadhaa kuachwa bila makao tangu mzozo ulipozuka miezi sita iliyopita.

  Marekani imeweka vikwazo kadhaa vya kiuchumi na usaidizi wa kiusalama dhidi ya Ethiopia kufuatia mzozo wa eneo la Tigray.

  Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani, Antony Blinken, pia ametangaza marufuku ya usafiri dhidi ya maafisa wa Ethiopia na Eritrea pamoja na wengine ambao wanatuhumiwa kufanya ukatili.

  Bw. Blinken amesisitiza kuwa hatua ya kimataifa inahitajika ili kusaidia katika utatuzi wa mzozo huo na kuongeza wale waliopewa dhamana hawajachukua hatua madhubuti kukomesha ghasia.

  Maelfu ya watu wameuawa na wengine kadhaa kuachwa bila makao tangu mzozo ulipozuka miezi sita iliyopita.

  Pande zote mbili zimelaumiwa kwa ukiukaji wa haki za binadamu.

  Mapema siku ya Jumapili serikali ya Ethiopia ilipuuzilia mbali madai kwamba raia katika Jimbo lililokumbwa na vita la Tigray, walilengwa kwa silaha za kemikali kutoka kwa majeshi ya Ethiopia au Eritrea.

  Gazeti la Telegraph la Uingereza limeripoti kuwa watu kadhaa walichomeka vibaya kutokana na utumizi ya phosphorous nyeupe. Kemikali ambayo inaweza kutumika kihalalli vitani lakini ikitumiwa dhidi ya raia inasadikiwa kuwa uhalifu wa kivita.

  Gazeti hilo limesema miongoni mwa waathiriwa ni mtoto wa kike wa miaka 13 ambaye alichomeka baada ya nyumba yao kushambuliwa mwezi uliopita .

  Wizara ya Mambo ya nje ya Ethiopia imeelezea madai kwamba silaha za kemikali zilitumiwa dhidi ya watu wa Tigray kuwa mabaya na ya kutowajibika.

  Maelezo zaidi:

 3. Na Mohammed AbdulRahman

  Mchambuzi

  Rais Mohammed Abdullahi Farmajo wa Somalia

  Umezuka wasiwasi katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu baada ya mapigano makali ya risasi Jumapili na Jumatatu ya wiki hii, Kati ya majeshi yanayomuunga mkono Rais Mohamed Abdullahi Mohamed maarufu kwa jina la "Farmaajo", na makundi ya wanamgambo yanayowaunga mkono wapinzani wake

  Soma Zaidi
  next
 4. Eritrea yawachilia Wakristo 36 waliofungwa kwa imani yao

  Isaias Afwerki
  Image caption: Eritrea imekuwa ikitawaliwa na Isaias Afwerki tangu ilipopata uhuru kutoka kwa Ethiopia

  Maafisa nchini Eritrea wamewaachilia kwa dhamana wafungwa 36 ambao wamekuwa mahabusu kwasababu ya imani yao.

  Vyanzo vya habari hii vimeiambia BBC kuwa 14 kati ya wafungwa hao wamekuwa mahabusu kwa miaka minne iliyopita katika kisiwa cha Dahilik. Wengine 20 waliokamatwa mwishoni mwa mwezi uliopita wameachiliwa kwa dhamana.

  Wafungwa wote wanatoka katika madhehebu ya Kiinjilisti na Kipentekosti.

  Mwaka wa 2002 Eritrea ilianzisha sheria ambayo inazuia makanisa yote isipokua makanisa ya Orthodox, Katoliki na Kilutheli.

  Waislamu wa madhehebu ya Sunni wanatambuliwa rasmi.

  Serikali ya Eritrea imekuwa ikiwaachilia huru watu waliofungwa kwasababu za kidini.

  Mwezi Septemba mwaka 2020, serikali ya Eritrea liwaachilia mahabusu zaidi ya 20 ambao walikuwa wamefungwa kwa miaka mingi . Mwezi Disemba, maafisa pia waliwaachilia wafuasi 28 wa kikundi cha Mashahidi wa Jehovah baada ya kutumikia kifungo cha jela kwa muda mrefu.

  Wakristo wengi, bado wamebakia magerezani na wengine wamekuwa wakikamatwa mara kwa mara, kulingana na wanaharakati wa uhuru wa dini.

  Serikali ya Eritrea inawashutumu Wakristo wa madhebebu ya Kipentekoste na kiinjilisti kwa kutumiwa na serikali za kigeni.

  Eritrea, ambalo ni taifa lenye usiri, na la kijeshi kwa hali ya juu, imekuwa ikitawaliwa na Isaias Afwerki tangu ilipopata uhuru wake kutoka kwa Ethiopia mwaka 1993, bila uchaguzi au bunge na muswada wa katiba uliopo haujawahi kutekezwa.

  Soma zaidi:

  Eritrea: Mambo matano ambayo raia wanataka yatekelezwe kwa dharura