Wanyama

 1. paka

  Tulidhani sisi ndiyo aina pekee ya viumbe wanaofurahia mwingiliano wa kimwili, lakini kama Jason G Goldman alivyogundua, mabadiliko kadhaa ya kushangaza katika maumbile vimebadilisha maoni yetu.

  Soma Zaidi
  next
 2. Watu watatu wakamatwa Tanzania wakidaiwa kuuza mishikaki ya nyama ya mbwa

  mBWA

  Gazeti la Mwananchi nchini Tanzania limeripoti kuhusu kukamatwa kwa vijana watatu wanaodaiwa kuuza mishikaki ya mbwa katika kituo cha mabasi yaendayo mikoani eneo la Msamvu, Morogoro.

  Waliokamatwa kutokana na tuhuma hizo walikutwa wakichuna ngozi ya mbwa na kudai kuwa ni wauzaji mishikaki ni Hamza Rajabu (20), Omary Mohamed wote wakazi wa Msamvu na Mussa Juma (30) mkazi wa Mtawala.

  Vijana hao wamekamatwa wakiwa wanachuna ngozi ya mbwa tarehe 26 Aprili, 2021 katika daraja kuu la barabara iendayo Iringa eneo la relini.

  Kwa mujibu wa gazeti hilo wakazi wa eneo hilo wamesikitishwa na kulaani kitendo hicho na kutaka mamlaka kuchukua hatua kali dhidi yao.

  “Hawa watu wanafahamika kwa uuzaji wa mishikaki haswa majira ya usiku, ndio wamekuwa wakiuza mara nyingi, unawakuta kituo cha mafuta na stendi ya Dodoma. Watu tunakula na wanatuuzia mishikaki bila hata kujua kama ni ya mbwa ama la,” alisema Alexanda.

  “Tumesikia mmoja wa hao vijana ni wakala mkubwa wa wauza nyama za mishikaki hasa ya ile ya mia mia, kinachotakiwa ni kuepuka nyama za kununua mitaani, sio kila nyama unayoletewa unanunua, unatakiwa kuchukua nyama sehemu sahihi ukijua hii ni nyama ya mnyama fulani,” alisema dereva wa bodaboda eneo la Msamvu , Abdallah Pawa.

  Mfanyakazi wa stendi ya Msamvu, Samson Jonas alisema: “Idadi ya watu wanaoingia na kutoka hapa Msamvu ni wengi, huyu jamaa ni muuzaji na atafanya wale wafanyabiashara wa mishikaki kukosa wateja, kwani si wote wanaouza nyama ya mbwa, wapo wanaouza mishikaki ya ng’ombe, mbuzi au kuku.

 3. Video content

  Video caption: Mkoa wa katavi Tanzania waanzisha bucha maalumu ya kuuza nyama ya wanyamapori

  Mkoa wa Katavi kusini Magharibi mwa Tanzania , umeanzisha bucha maalumu ya kuuza nyama pori, biashara ambayo ni adimu Afrika Mashariki

 4. Video content

  Video caption: Fahamu jinsi ndege kwa jina tai walivyo katika hatari ya kuangamia Afrika

  Kati ya tai 11 wanaopatikana barani Afrika , saba wapo katika hatari ya kuangamia . Nchini Kenya spishi moja – ya tai wenye ndevu – imesalia na tai watano kulingana na wahifadhi w

 5. A hippo seen near Hacienda Napoles in 2016

  Viboko hao walilpelekwa Colombia kinyume na sheria mnamo mwaka 1980, na nguli wa biashara haramu za dawa za kulevya Pablo Escobar, wanyama hao wameongezeka na kuathiri mazingira ,kwa mujibu wa wanasayansi . Utafiti mpya unashauri kuwa nii vyema kuwaua ili kuzuia athari kubwa zaidi.

  Soma Zaidi
  next
 6. Video content

  Video caption: Tazama jinsi mjusi huyu alivyonusurika kifo kutoka kwa nyoka wenye njaa

  Mjusi mkubwa anayeishi baharini nusra awe chakula cha nyoka walio na njaa kisiwani Galapagos huko Fernandina.

 7. Video content

  Video caption: Tazama vita vya sokwe vilivyodumu miaka 4 Tanzania

  Tafiti mbalimbali zilizofanywa juu ya Wanyama aina ya Sokwe, matokeo yake mengi ikiwemo tabia za nyani hufananishwa na binadamu. Kama ilivyo kwa binadamu Sokwe pia huwa na migogo