Ubaguzi wa Rangi

 1. Wanawake watano kutoka DRC waishtaki Ubelgiji kwa kuwatenganisha na wazazi wao kwa lazima

  mm

  Wanawake watano wenye asili ya Kongo na Ubelgiji, waliotengwa na familia zao wakati wa ukoloni wameishtaki serikali ya Ubelgiji kwa uhalifu dhidi ya ubinadamu.

  Wanawake hao wanasema walichukuliwa kutoka kwa mama zao weusi wakati wa kuzaliwa tu kwa msingi wa rangi ya ngozi yao.

  Wanawake hao watano walikuwa kati ya maelfu ya watoto waliochukuliwa kutoka kwa familia zao na kupelekwa kwenye vituo vya kulelea watoto vya kidini kwa kuwa lilikuwa ni agizo kwa wakati ule wa ukoloni.

  Wengi wao walikuwa hata hawawafahamu baba zao wazungu. Wale ambao wameenda mahakamani hawakupelekwa Ubelgiji wakati Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo ilipopata uhuru mnamo 1960.

  Ubelgiji inashtakiwa kwa uhalifu dhidi ya ubinadamu, kosa ambalo hakuna kikomo cha wakati.

 2. Video inayoonesha jinsi polisi wanavyokabiliana na mtu mweusi anayelalamika 'Nimepooza' yachunguzwa

  p

  Polisi nchini Marekani wanafanyia utafiti video inayomuonesha mwanaume mweusi akitolewa kwenye gari akiwa anapiga kelele,"Nimepooza".

  Video hiyo inaonesha polisi wakiwa wamesimama eneo la Clifford Owensby ,Dayton, Ohio, na kumwamrisha kutoka katika gari ili wakague kama amebeba dawa za kulevya. Tukio hilo lilitokea mwezi uliopita.

  Winsby, mwenye miaka 39,alikataa kushirikiana nao na kusema kuwa hawezi kutembea wakati polisi wakiendelea kusisitiza na kumvuta nywele na kumvuta mkono atoke nje wakati akiendelea kupiga kelele ya kuomba msaada.

  Polisi wa Dayton wanasema wanafanya utafiti wa tukio hilo lililotokea Septemba 30.

  Mamlaka imeripoti kuwa Owensby alisimamishwa na polisi kwasababu alishukiwa kuwa amebeba dawa za kulevya lakini badala yake walikuta bag lake lililokuwa ndani ya gari likiwa na $22,500 .

  Hakuna mashtaka ya usafirishaji wa dawa za kulevya yaliyofungulwa dhidi ya Owensby ambaye alikataa kufuata maelekezo ya polisi.

 3. Shirikisho la FA lakemea ubaguzi wa rangi dhidi ya Marcus Rashford, Jadon Sancho na Bukayo Saka

  marcus

  Shirikisho la soka nchini Uingereza limelaani ubaguzi wa rangi dhidi ya wachezaji wa England Marcus Rashford, Jadon Sancho na Bukayo Saka baada ya fainali ya siku ya jumapili ya kombe la Euro 2020 walioshindwa na Italia kupitia mikwaju ya penalti.

  Wachezaji wote watatu walikosa kufunga magoli yao ya penalti katika mchuano huo walioshindwa mabao 3-2 na walilengwa katika mitandao ya kijamii baada ya mchuano huo. Polisi wa eneo la Metropolitan wanachunguza ubaguzi huo na wamesema ‘Hautavumiliwa’ FA imesema ‘imeshangazwa’ na matusi hayo ya ubaguzi wa rangi. Wachezaji wa England wamekuwa wakipiga magoti katika michano ya Euro kuangazia vita vyao dhidi ya ubaguzi wa rangi katik timu yao .

  "Tutafanya kila tuwezalo kusaidia wachezaji walioathiriwa huku tukisisitiza adhabu kali zaidi kwa kila mtu anayehusika. "Tutaendelea kufanya kila tuwezalo kumaliza ubaguzi ndani ya michezo, lakini tunasihi serikali ichukue hatua za haraka na kuleta sheria inayofaa ili unyanyasaji huu uwe na adhabu za kudumu kimaisha kwa wahusika.

  "Makampuni ya mitandao ya kijamii yanahitaji kuchukua hatua na kuwajibika kwa kuwapiga marufuku wanyanyasaji kutoka kwa majukwaa yao, kukusanya ushahidi ambao unaweza kusababisha kushtakiwa na kusaidia kufanya majukwaa yao kutotumiwa kwa dhuluma hizi’ Rashford aliangazia matukio ya kibaguzi aliyopokea kwenye mitandao ya kijamii mnamo Mei baada ya kupoteza fainali ya Ligi ya Uropa na Manchester United.

  Mwaka jana Sancho alikuwa miongoni mwa wachezaji nyota waliolalamika dhidi ya ubaguzi wa rangi kufuatia mauaji ya George Floyd na afisa wa polisi huko Minneapolis. Kampuni za mitandao ya kijamii zimekosolewa kwa kukosekana kwa hatua juu ya unyanyasaji wa kibaguzi kwenye majukwaa yao, na mnamo Aprili Instagram ilitangaza zana ya kuwezesha watumiaji kuchuja moja kwa moja jumbe za matusi kutoka kwa wale ambao hawawafuati.

  Kufuatia matukio kadhaa vya unyanyasaji mitandaoni, vilabu kadhaa, wachezaji, wanariadha na mashirika ya michezo walishiriki katika siku nne za kususia mitandao ya kijamii mnamo Aprili kuhamasisha kampuni kuchukua misimamo mikali dhidi ya unyanyasaji wa kibaguzi na kijinsia.