Shirika la Fedha Duniani (IMF)

 1. IMF yashindwa kutoa makadirio ya pato la ndani la Ethiopia

  M

  Shirika la Fedha Duniani(IMF) limesema kuwa haliwezi kukisia kukua kwa kiwango cha Pato ndani la Ethiopia kwa kipindi cha mwaka 2022-2026 kufuatia kile wanachosema kuwa ni "kiwango cha juu cha kutokuwa na uhakika".

  Hali inakuja kufuatia mzozo uliochukua miezi kumi na moja katika eneo la kaskazini la Tigray.

  IMF imetoa makadirio ya uchumi ya dunia kwa kukadiria kukua kwa pato la ndani kwa nchi kuwa 2% kwa mwaka 2021, ambayo iko chini kwa 6% ya mwaka 2020.

  Kwa kulinganisha, na nchi jirani ya Eritrea- ambayo pia inahusika katika mzozo huo - itaona ukuaji wa 4.8% kwa 2022-2026.

  Kenya- ambayo ina uchumi mkubwa Afrika Mashariki- kwa upande mwingine, utaongezeka kwa 6% katika kipindi hicho hicho.

  Katika muongo mmoja uliopita, Ethiopia ilikuwa miongoni mwa nchi ambazo uchumi wake unakuwa kwa kasi zaidi, kwa kuongezeka hata mara mbili ya takwimu ya kiwango kilichopita.

  Hata hivyo uchumi wake umeathirika kutokana na ukame, mvutano ya kikabila wakati huohuo wataalam pia wameonya juu ya kulipwa kwa deni lake la kigeni ambalo lilifadhili miradi mikubwa ya miundombinu.

  Nchi zingine ambazo IMF haikutoa makadirio ni Afghanistan, Libya na Syria- na nchi zote zilizokumbwa na mizozo.

  Ripoti ya IMF ilisema uchumi wa duniani unakadiriwa kukua asilimia 5.9 mnamo 2021 na asilimia 4.9 mnamo 2022, asilimia 0.1 chini kwa 2021 kuliko makadirio ya Julai.

  Mlipuko wa janga la corona pia umeathiri uchumi haswa wa nchi zinazoendelea.

 2. Aliyekamatwa kwa kutengeneza bango la picha ya Rais Kenyatta kulalamikia mikopo ya IMF aachiwa huru kwa dhamana

  Mwanaharakati Edwin Kiama aliyeshikiliwa kwa kutengeza bango lenye picha ya Rais Uhuru Kenyatta nchini Kenya ili kulalamikia hatua ya serikali kuuchukua mkopo mwingine wa shilingi dola bilioni 255 au dola bilioni 2.34 ameachiwa huru kwa dhamana wakati uchunguzi ukiendelea.

  Picha hiyo ilishirikishwa mtandaoni na Wakenya wengi wakilalamikia mkopo wa IMF kutochukuliwa nchini humo.

  View more on twitter

  Mutemi Kiama ameachiwa huru Alhamisi kwa dhamana ya dola 4,600 (£3,300) na kutakiwa kuripoti kila siku kwa afisa wa uchunguzi.

  Mwanaharakati huyo aliwekwa kuzuizini kwa muda wa siku mbili wakati akihojiwa kwa uchunguzi .

  Wakenya mtandaoni wamekuwa wakilalamikia fedha za mkopo wa dola bilioni 2.4 zilizotolewa na IMF kwa taifa la Kenya kukabiliana na Covid-19 na kudai kuwa hiyo ni rushwa.

  Ingawa IMF ilitetea uamuzi wake wa kutoa mkopo licha ya malalamiko ya umma.

  Ilisema kuwa Kenya imejidhatiti kutumia vyema fedha hizo kwa walengwa na imejipanga kuunga mkono jitihada za taifa hilo katika kulinda rasilimali za wananchi.