DRC

 1. Vikosi vya DR Congo vyakabiliana na wanajeshi wa Rwanda

  Jeshi la Rwanda halijajibu madai ya tukio hilo
  Image caption: Jeshi la Rwanda halijajibu madai ya tukio hilo

  Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo inasema kuwa vikosi vyake vimekabiliana na wenzao wa Rwanda karibu na mpaka wa mashariki siku ya Jumatatu.

  Msemaji wa jeshi katika Mkoa wa Kivu Kaskazini alisema vikosi vya Rwanda vilivuka mpaka na kuingia Congo katika hatua ambayo ilisababisha makabiliano.

  “Kitengo cha wanajeshi wa Rwanda kiliingia kilomita tano ndani ya Congo…Hauwezi kuelezea jinsi wanajeshi waliojihami walivuka mpaka na kuanza kupiga risasi," Brigedia Jeneral Sylvain Ekenge taliambia BBC Idhaa ya Maziwa Makuu.

  Majeshi ya Rwanda hayajatoa tamko lolote kuhusu madai hayo au kujibu ombi la BBC.

  Ramani

  Video zinazoshirikishwa mitandaoni zinawaonesha wenyeji waliokuwa na hofu wakikimbia huku vikosi hivyo viwili vikikabiliana kwa rasasi. Wanajeshi wa Rwanda baadaye walirudi nyuma na kwenda nyumbani.

  “Kwa bahati nzuri hakuna mtu aliyefariki katika tukio hilo”, Jenerali Ekenge alisema.

  Viongozi na wakazi wa eneo hilo walirejea majumbani mwao baada ya hali ya utulivu kudumishwa.

  Mvutano wa mipaka kati ya majirani hao wawili wa Afrika Mashariki ni jambo la kawaida kwa sababu ya biashara haramu, ukosefu wa mipaka wazi na mashambulio ya waasi.

  Tshisekedi na Kagame watofautiana kuhusu 'ukatili DRC'

  Kwanini hali ya usalama imeendelea kuwa tete nchini DRC?

 2. DRC: Mwandishi wa kibinafsi wa AFP bado anazuiliwa

  Kwa zaidi ya saa 24 sasa, mwandishi wa kibinafsi wa AFP nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Jam Pierre Sosthène Kambidi, bado anasemekana kuzuiliwa katika gerza la kijeshi,tangu siku ya Jumatatu.

  Mwandishi huyo mpekuzi pia anachangia mada katika tuvuti ya Actualité.cd, chombo cha habari mtandaoni DRC.

  Chombo cha habari anachofanyia kazi, kiliandika kikinukuu chanzo kutoka mahakama ya kijeshi kwamba Pièrre Sosthene Kambidi anahojiwa kwa kuwa mtu wa kwanza kuwa na video inayoashiria kuua kwa wataalamu wawili wa Umoja wa Mataifa ambao walitekwa na wanaume waliojihami mnamo March 12, 2017, kati kati ya DRC.

  Raia wa Marekani Michael Sharp na Zaida Catalan, wa Uswidi walikuwa sehemu ya kundi la wataalamu wa Umoja wa Mataifa nchini DR- Congo. Walikuwa wakichunguza mazo katika eneo la Kasaï.

  Zaidi ya vikao 100 vya mahakama vimefanywa tangu kesi hiyo ilipoanza kusikizwa Juni 15, 2017 dhidi ya watu 30 wanaotuhumiwa kwa mauaji ya wataalamu hao wa Umoja wa Mataifa.

  Kwanini hali ya usalama imeendelea kuwa tete nchini DRC?

  Mzozo wa DRC: Rais Felix Tshisekedi awateua wanajeshi kuwa magavana wa Ituri na Kivu Kaskazini

 3. Watu 12 wafariki DR Congo kutokana na mgodi uliovuja sumu Angola

  Mto uligeuka na kuwa mwekundu mwezi uliopita
  Image caption: Mto uligeuka na kuwa mwekundu mwezi uliopita

  Karibu watu 4,500 wameugua kusini mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kufuatia kuvuja kwa sumu kutoka kwa mgodi wa almasi katika nchi jirani ya Angola, waziri wa mazingira anasema.

  Eve Bazaiba alisema watu 12 walikuwa wamefariki dunia.

  Alisema kuwa DR Congo itauliza fidia ya uharibifu uliosababishwa lakini haikutaja kiasi.

  Hata hivyo, hadi kufikia hivi sasa hakuna aliyesema chchote kujibu hayo hasa kutoka kwa kampuni ya madini.

  Mwezi uliopita kulikuwa na uvujaji wa kutoka eneo la uhifadhi wa bidhaa za vyuma vizito uliosababisha mto kuwa na rangi nyekundu, samaki, viboko na wanyama wengine wakafa.

 4. Muungano wa upinzani waitisha maandamano DR Congo

  Martin Fayulu

  Vyama vya upinzani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo vimeitisha maandamano ya umma mwezi ujao kushinikiza kusawazishwa kwa sheria za uchaguzi.

  Upinzani umepinga sheria inayosimamia Tume huru ya Kitaifa ya Uchaguzi (Ceni) na kuonya dhidi ya majaribio yoyote ya kuchelewesha kura ya mwaka wa 2023.

  Rais Felix Tshisekedi anatuhumiwa kuzuia mchakato wa uchaguzi wakati wakuu wa madhehebu ya kidini wanahangaika kuafikia makubaliano juu ya mtu mwenye haiba gani anayepaswa kuongoza Ceni.

  Viongozi wawili wakuu wa Muungano wa upinzani maarufu Lamuka, Martin Fayulu na Adolphe Muzitois wameitisha maandamano ya Septemba 15 kote nchi.

 5. Vikosi vya Marekani kupambana na wanamgambo wa DRC

  Manajeshi wa Marekani

  Rais wa Jamuhuri ya kidemokrasi ya Congo, Felix Tshisekedi, amesema kikosi maalum cha Marekani kitapelekwa hivi karibuni nchini humo kusaidia kupigana na wanamgambo wa Kiislamu.

  Amesema watatakiwa kuwepo kwa wiki chache, kusaidia jeshi la DRC katika kampeni yake dhidi ya wapiganaji wa Allied Defence Forces (ADF).

  Watawashauri walinzi wa wanyamapori katika mbuga za wanyama za Virunga na Garamba, ambazo ni maficho ya makundi ya wanamgambo.

  Marekani ililiorodhesha kundi la ADF kama kikundi cha ugaidi chenye uhusiano na Islamic State.

  Wataalamu wa Umoja wa Mataifa wameelezea wasiwasi wao kuhusu uhusiano wa kundi hilo na Islamic State.

 6. Video content

  Video caption: Watoto 2000 wanakutanishwa na familia zao baada ya kukimbia mlipuko wa volcano DRC

  Watoto 2000 waliopoteana na familia zao wakati wa mlipuko wa volcano DRC waungana tena na familia