Israel

 1. Mapacha waliounganika kichwani watenganishwa katika upasuaji wa kipekee huko Israeli

  twin

  Watoto pacha wenye umri wa mwaka mmoja ambao walizaliwa wakiwa wameunganika nyuma ya vichwa vyao wameweza kuonana kwa mara ya kwanza baada ya kufanyiwa upasuaji nadra wa kuwatenganisha huko Israeli.

  Operesheni hiyo ya masaa 12 katika Kituo cha Matibabu cha Soroka katika mji wa Beersheba wiki iliyopita ilichukua miezi kadhaa ya maandalizi, na kujumuisha vipandikizi vya kichwa kwa wote wawili.

  Wataalam kadhaa kutoka Israeli na nje ya nchi walihusika.

  Wasichana hao ambao hawajatajwa majina, wanasemekana kupata nafuu "Wanapumua na wanakula peke yao," Eldad Silberstein, mkuu wa idara ya upasuaji katika kituo cha matibau cha Soroka, aliiambia Idhaa ya Israeli ya Channel 12.

  is

  Ni mara ya kwanza operesheni kama hiyo, ambayo imefanywa mara 20 tu ulimwenguni, kufanywa nchini Israeli.

  Miezi kabla ya upasuaji, mifuko ya silicone yenye iliingizwa vichwani mwao na kupanuliwa mara kwa mara ili kunyoosha ngozi. Ngozi mpya ilitumika kuziba vichwa vyao baada ya mafuvu kujengwa upya.

  Maandalizi pia ni pamoja na uundaji wa mfano halisi wa mapacha kupitia teknolojia ya 3D, alisema Mickey Gideon, daktari mkuu wa upasuaji wa Soroka. "Kwa furaha yetu, kila kitu kilikwenda kama tulivyotarajia," akaongeza.Wasichana hao, ambao walizaliwa mnamo Agosti 2020, wanatarajiwa kuishi maisha ya kawaida kabisa.

  Soma zaidi:

  Mapacha waliounganika: 'Tulijua kuwa tuko tofauti na watoto wengine'

  Sababu za kifo cha Maria na Consolata

 2. Walinzi wa Uingereza wakilinda meli kutoshambuliwa

  Malumbano ya hasira yamekuwa yakiendelea, huku mabalozi wakiendelea kuitwa na Wizara za mambo ya nje na vitisho vya ulipizaji kisasi vimetolewa wazi baada ya shambulio la droni dhidi ya meli ya mafuta lililosababisha mauaji wiki iliyopita

  Soma Zaidi
  next