Donald Trump

 1. Trump kuzindua mtandao wa kijamii wa TRUTH Social

  ormer US President Donald Trump said the new platform would "stand up to the tyranny of big tech"

  Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump ametangaza mipango ya kuzindua mtandao mpya wa kijamii, uitwao TRUTH Social.

  Amesema jukwaa hilo "litakabiliana na jeuri ya kampuni kubwa za teknolojia ", akizishutumu kwa kunyamazisha sauti za wapinzani huko Marekani.

  Kampuni ya Trump Media & Technology Group (TMTG), ambayo yeye ni mwenyekiti wake, pia inakusudia kuzindua huduma ya usajili wa mahitaji ya video.

  Bw. Trump alipigwa maarufuku katika mitandao ya kijamii au kufungiwa na mitandao kama ya Twitter na Facebook baada ya kundi la wafuasi wake kuvamia Bunge la Marekani Januari mwaka huu.

  Yeye na washauri wake tangu wakati huo walidokeza kuwa wanapanga kuunda mtandao hasimu wa kijamii.

  Toleo la mapema la biashara yake ya hivi karibuni, TRUTH Social, itakuwa wazi kwa wageni waalikwa mwezi ujao, na kutakuwa na "uzinduzi wa kitaifa" ndani ya miezi mitatu ya kwanza ya 2022, kulingana na taarifa ya TMTG.

  "Tunaishi katika ulimwengu ambao Taliban ina uwepo mkubwa kwenye Twitter, lakini Rais wako mpendwa wa Marekani amenyamazishwa," aliandika Bw Trump.

  Mapema mwaka huu, alizindua Kutoka kwa Dawati la Donald J Trump, ambayo mara nyingi ilikuwa ikiitwa blogu.

  "Kila mtu ananiuliza kwa nini mtu asisimame kupinga makampuni makubwa ya teknolojia? Sawa, tutafanya hivyo hivi karibuni!" aliongeza.

 2. Trump amkosoa Biden jinsi alivyoshughulikia suala la Afghanistan

  Trump
  Image caption: Donald Trump

  Trump amkosoa Biden jinsi alivyoshughulikia suala la Afghanistan katika mahojiano na kituo cha habari cha Fox News.

  Rais huyo wa zamani wa Marekani pia alikosoa kujiondoa kwa Joe Biden kutoka Afghanistan, na vile alivyoshughulikia suala la wanaovuka mpaka wa Mexico ambayo idadi yake hivi karibuni imepita ile iliyorekodiwa kwa kipindi cha miongo miwili.

  "Angalia kile alichokifanya Biden katika mpaka wa kusini... [hali ilivyo nchini Afghanistan] ni kama mpaka wa kusini lakini imeshughulikiwa vibaya zaidi.

  Hakuna mtu aliyeshughulikia suala la mpaka wa kusini vibaya zaidi kuliko yeye, Afghanistan vivyo hivyo", amesema.

  Bwana Trump pia alidai kwamba angeshughulikia uondoaji wa majeshi kwa njia tofauti.

  "Nilipunguza [jeshi la Marekani nchini Afghanistan] kutoka karibu 20,000 hadi wanajeshi 2,500 - na [sasa wanaondoa] tena wanajeshi kabla hatujatoa raia wetu na wakalimani na watu wengine ... waliotusaidia.

  "Sasa basi, tulichokuwa tunatakiwa kufanya ni kuchukua wanajeshi wetu mwisho - watu walikuwa ni wawe wa [kwanza] kuondoka", amesema.

 3. Trump aunga mkono hatua ya Nigeria kuifungia Twitter

  Bw. Trump alifungiwa na Twitter na Facebook mwezi Januari
  Image caption: Bw. Trump alifungiwa na Twitter na Facebook mwezi Januari

  Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump amepingeza hatu ya Nigeria kuipiga marufuku Twitter - na kutoa wito nchi zingine zifuate mkondo huo.

  "Pongezi kwa nchi ya Nigeria, kwa kuifungia Twitter kwasababu ya kumpiga marufuki Rais wao," alisema katika taarifa.

  Rais huyo wa zamani ametoa wito kwa nchi zingine kufuata mkondo na kuzifungia Facebook na Twitter " kwa kudhibiti uhuru wa kujieleza".

  Bw. Trump alipigwa marufuku na katika mitandao ya kijamii ya Twitter na Facebook mwezi Januari kwa tuhuma za kuchapisha ujumbe wa kuchochea uvamizi wa bunge la Marekani. Watu watano walifariki kutokana na kisa hicho.

  Twitter

  Katika taarifa yake siku ya Jumatatu, alijita kwanini hakuzifungia Facebook na Twitter wakati wa Urais wake.

  "Wao ni nani kuamua kizuri na kibaya ikiwa wao wenyewe ni wabaya? Nadhani ningeliwapiga marufuku nilipokuwa Rais. Lakini [Mwanzilishi wa Facebook Mark] Zuckerberg aliendelea kunipigia simu na kuja Ikulu ya White House kwa chakula cha jioni akiniambia jinsi nilivyokua mzuri," alisema.

  Wiki iliyopita Nigeria ilifunga akaunti za Twitter nchini humo kwa madai kwamba "shughuli za mtandao huo zinahujumu uwepo wa Nigeria kama taifa lililoundwa shirikisho".

  Hatua hiyo ilichukuliwa siku kadhaa baada ya ujumbe wa Rais Muhammadu Buhari kuondolewa kwa kukiuka kanuni za mtandao wa huo wa kijamii.

  Ilizua ghadhabu miongoni mwa Wanaigeria na mataifa ya magharibi ambayo yalisema hatua hiyo inaminya uhuru wa kidemokrasi.

  Pande zote mbili zimesema zinajadiliana kuhusu namna ya kusuluhishi

  Soma zaidi: