Ufaransa

 1. Yves Bucyana

  BBC Swahili, Kigali

  Itangizwa mu Rwanda ry'ishuri ryigisha umupira w'amaguru ry'ikipe ya Paris Saint-Germain yo mu Bufaransa, aha ni ku kibuga cy'i Huye mu majyepfo, ku itariki ya 27/11/2021

  Mabingwa wa Ufaransa, timu ya Paris Saint Germain imezindua rasmi kituo cha kufundishia soka kwa vijana nchini Rwanda, ikiwa ni sehemu ya makubaliano ya miaka 3 ya kibiashara na kuinua sekta ya utalii nchini Rwanda.

  Soma Zaidi
  next
 2. Ufaransa yawashauri raia wake kuondoka Ethiopia - AFP

  Raia wa Ethiopia

  Ufaransa imekuwa nchi ya hivi punde zaidi kuwashauri raia wake kuondoka Ethiopia huku waasi wa Tigray wakisema wanasonga mbele karibu na mji mkuu Addis Ababa, shirika la habari la AFP linaripoti.

  "Raia wote wa Ufaransa wanahimizwa rasmi kuondoka nchini bila kuchelewa," ubalozi wa Ufaransa mjini Addis Ababa ulisema katika barua pepe iliyotumwa kwa raia wa Ufaransa, shirika hilo linaripoti.

  Marekani na Uingereza ni kati ya nchi ambazo zimetoa ushauri kama huo katika wiki za hivi karibuni huku pia zikiwaondoa wafanyikazi wasio wa lazima.

  Afisa wa ubalozi wa Ufaransa alisema kunaweza kuwa na kuondoka kwa "hiari" kwa wafanyikazi wa ubalozi, haswa wale walio na familia, ripoti ya AFP.

  Vita vya Ethiopia: Kwanini kujua kinachoendelea Tigray ni muhimu?

  Mgogoro wa Ethiopia wa Tigray: Jinsi TPLF ilivyolizidi maarifa jeshi la Ethiopia

 3. Macron awaomba msamaha mashujaa wa vita wa Algeria

  Bwana Macron aliwaambia maveterani wa vita katika Jumba la Elysee huko Paris
  Image caption: Bwana Macron aliwaambia maveterani wa vita katika Jumba la Elysee huko Paris

  Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amewaomba msamaha Harkis -r Waalgeria waliopigania uhuru wa Algeria dhidi ya Ufaransa.

  Bwana Macron alizomewa aliposema Ufaransa ilizembea katika majukumu yake kwa mashujaa hao.

  Aliahidi ukumbusho na sheria juu ya fidia mwishoni mwa mwaka.

  Tume itaundwa kusikiza madai kutoka kwa wapiganaji walionusurika na watoto wao, ambao waliolelewa kwenye uzio wa sing'eng'e katika kambi za Ufaransa.

  Maelfu ya watu walipelekwa Ufaransa baada ya nchi hiyo kushindwa mwaka 1962, lakini wengine wengi wengi zaidi waliachwa nyuma na kuteswa kwa kuwa washirika.

  Marais waliopita waliomba msamaha, lakini viongozi Harki walisema mfuko wa ugumu wa dola milioni 50 (£36.5m) uliotangazwa miaka mitatu iliyopita haikidhi mahitaji.

  Kwa nini Rwanda inasubiri kuombwa radhi na rais wa Ufaransa?

 4. Korea Kaskazini:Aukus inaweza kuchochea 'nchi kukimbilia kujihami na zana za kinyuklia

  Kim Jong-un
  Image caption: Picha ya Kim Jong-un kutoka maktaba

  "Korea Kaskazini imekosoa mkataba mpya wa usalama kati ya Marekani, Uingereza na Australia, ikisema unaweza kusababisha "nchi kukimbilia kujihami na zana za kinyuklia."

  Afisa wa wizara ya mambo ya nje alisema makubaliano ya Aukus "yatasumbua usawa wa kimkakati katika eneo la Asia-Pasifik."

  Mkataba huo utajumuisha Marekani na Uingereza zikiipa Australia teknolojia ya kujenga nyambizi zinazotumia nyuklia.

  Inatazamwa sana kama juhudi ya kukabiliana na ushawishi wa China katika Bahari ya China Kusini inayozozaniwa.

  Mkataba wa Aukus ulitangazwa wiki iliyopita na pia utajumuisha makombora ya meli, akili ya bandia na teknolojia zingine.

  "Hivi ni vitendo visivyofaa na vya hatari ambavyo vitasumbua usawa wa kimkakati katika eneo la Asia-Pasifiki na kusababisha kila nchi kukimbilia kuwa na silaha za nyuklia," amesema afisa wa wizara ya mambo ya nje ya DPRK akirejelea makubaliano ya usalama.

  Wiki iliyopita, Korea Kaskazini ilifanya majaribio mawili makubwa ya silaha - lile la kombora la masafa marefu na kombora la balistiki.

  China pia imekosoa makubaliano hayo na msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Beijing Zhao Lijian amesema muungano huo unahatarisha "kuharibu kabisa amani ya eneo ... na kuimarisha juhudi za kujihami kwa silaha za nyuklia.

  Pyongyang ilisema ni "kawaida kabisa kwa nchi jirani [kama] China kulaani vitendo hivi kama kutowajibika kwa kuharibu amani na utulivu wa eneo hilo."

  Matarajio ya mkataba huo ni kuona Marekani ikishirikisha wengine teknolojia yake ya nyambizi kwa mara ya kwanza katika miaka 60, hapo awali ikiwa ilishirikisha Uingereza mara moja tu.

  Ni nchi gani zilizo na nyambizi?

  Nchi zilizo na nyambizi
  Image caption: Nchi zilizo na nyambizi

  Inamaanisha Australia itaweza kujenga nyambizi zenye nguvu za nyuklia ambazo ni haraka mno na ngumu kuzigundua kuliko meli za kawaida.

  Zinaweza kukaa ndani ya maji kwa miezi kadhaa na kudungua makombora ya umbali mrefu - ingawa Australia inasema haina nia ya kuweka silaha za nyuklia ndani yake.

  China haikutajwa moja kwa moja wakati wa tangazo la mpangilio wa usalama.

  Hata hivyo, viongozi wa nchi hizo tatu walitaja mara kwa mara masuala ya usalama wa kikanda ambayo "yameongezeka sana".

  Korea Kaskazini pia ilirejelea taarifa ya hapo awali iliyotolewa na Ufaransa, ambayo ilitaja makubaliano hayo kuwa "usaliti," na kusema kwamba mkataba huo umesababisha "mgogoro mkubwa" kati ya washirika.

  Ufaransa imekuwa ikikosoa mkataba wa Aukus kwasababu ilifikisha ukomo wa makubaliano yenye thamani ya $ 37bn (£ 27bn) yaliyosainiwa na Australia mnamo mwaka 2016 kwa Ufaransa kujenga nyambizi 12 za kawaida.

  Ufaransa inasema iliarifiwa juu ya makubaliano hayo saa chache kabla ya tangazo rasmi kwa umma kutolewa.

 5. Chuo cha kupambana na ugaidi chafunguliwa Ivory Coast

  Wanajeshi

  Chuo cha kimataifa cha kupambana na ugaidi kimefunguliwa karibu na mji wa Abidjan huko Ivory Coast.

  Chuo hicho kinachofahamika kama AILCT, kilifadhiliwa na Ufaransa na Muungano wa Ulaya ,EU, na nchini zingine kinalenga kusaidia eneo hilo kukabiliana na wanamgambo wa kijihadi.

  Hafla ya ufunguzi wake iliongozwa na Waziri Mkuu wa Ivory Coast, Waziri wa Ulinzi wa nchi hiyo na Waziri wa Mambo ya nje wa Ufaransa.

  Chuo hicho ambacho kimejengwa eneo lenye minazi mingi karibu kilo mita 80 kutoka mjini Abidjan, kitatumika kutoa mafunzo ya kijeshi.

  Wanajeshi

  Tayari dola milioni 27 sawa na (euro milioni 20) zimewekezwa katika mradi huo lakini fedha zaidi zinahitajika kuukamilisha ndani ya miaka miwili ijayo.

  Malengo matatu muhimu ni:

  • Kufundisha vikosi maalum vya majeshi katika mkoa huo.
  • Kuwapa mafunzo dhidi ya ugaidi maafisa, kama mahakimu, maafisa wa forodha na wahasibu.AILCT inataka kuunda mitandao ya wataalamu wanaojuana na kufanya kazi pamoja katika mipaka.
  • Kuunda kituo cha kimkakati cha kusoma.
  Tayari dola milioni 27 sawa na (euro milioni 20) zimewekezwa katika mradi huo
  Image caption: Tayari dola milioni 27 sawa na (euro milioni 20) zimewekezwa katika mradi huo

  Uzinduzi wake unakuja siku chache baada ya Ufaransa kutangaza kwamba inakamilisha Operesheni ya Barkhane katika eneo la Sahel, ambalo linakabiliwa ukame kusini mwa Jangwa la Sahara.

  Eneo hilo linajumuisha Mali, Chad, Niger, Burkina Faso na Mauritania.