Ugaidi

 1. Wanajeshi wa Rwanda wawaua wanamgambo wa kjihadi Msumbiji

  Wanajeshi kutoka nchitofauti za Afrika wanapelekwa Msumbij
  Image caption: Wanajeshi kutoka nchitofauti za Afrika wanapelekwa Msumbiji

  Vikosi vya Rwanda vilivyotumwa kusaidia kukabiliana na waasi vimewauwa wanamgambo wa kijihadi wasiopungua 30, maafisa wa usalama nchini Msumbiji wanasema.

  Maafisa hao wanasema wanajeshi walikuwa wakiifanya oparesheni ya usalama katika msitu wa karibu na mji wa bandari wa Palma walipokutana na wanamgambo hao.

  Karibu wanajeshi 1,000 wa Rwanda walipelekwa nchini Msumbiji mapema mwezi huu.

  Jumuia ya maendeleo ya mataifa ya kusini mwa Afrika (SADC) imepeleka wanajeshi wake nchini humo na vikosi vya Ureno vinasaidia kutoa mafunzo kwa wanajeshi wa Msumbiji.

  Karibu watu 800,000 wamefurushwa makwao kutokana na ghasia hizo zilizodumu miaka minne.

  Maelfu ya watu wameuawa na wengine wengi kukatwa vichwa.

  Soma zaidi:

 2. Habib with his laptop

  Taliban wameingia kwa fujo Afghanistan na sasa wanadhibiti karibu nusu ya wilaya za nchi hiyo. Baada ya vikosi vya kimataifa vikiongozwa na Marekani vikiondoka, baadhi ya raia wa Afghanistan kwa kuhofia maisha yao wanafanya mpango wa kutoroka. Tumezungumza na wale ambao wanang'ang'ana kuondoka.

  Soma Zaidi
  next
 3. Mlipuko wa Somalia waua zaidi ya wanajeshi 10

  Wanawake wanalia

  Zaidi ya wanajeshi 10 wameuawa baada ya mlipuaji wa kujitoa mhanga kujilipua katika kambi moja ya kijeshi iliyopo mji mkuu wa Somalia, Mogadishu, ripoti zinasema.

  Mwanahabari aliyekua katika eneo la tukio amesema mlipuaji huyo alijidai kuwa mwanajeshi, na kuingia katika kambi ya jeshi ya Wadajir na kuanza kulipua vilipuzi alivyokuwa amejifunga kiunoni, wakati wa mafunzo ya asubuhi.

  Watu wengine 10 pia wamejeruhiwa.

 4. Chuo cha kupambana na ugaidi chafunguliwa Ivory Coast

  Wanajeshi

  Chuo cha kimataifa cha kupambana na ugaidi kimefunguliwa karibu na mji wa Abidjan huko Ivory Coast.

  Chuo hicho kinachofahamika kama AILCT, kilifadhiliwa na Ufaransa na Muungano wa Ulaya ,EU, na nchini zingine kinalenga kusaidia eneo hilo kukabiliana na wanamgambo wa kijihadi.

  Hafla ya ufunguzi wake iliongozwa na Waziri Mkuu wa Ivory Coast, Waziri wa Ulinzi wa nchi hiyo na Waziri wa Mambo ya nje wa Ufaransa.

  Chuo hicho ambacho kimejengwa eneo lenye minazi mingi karibu kilo mita 80 kutoka mjini Abidjan, kitatumika kutoa mafunzo ya kijeshi.

  Wanajeshi

  Tayari dola milioni 27 sawa na (euro milioni 20) zimewekezwa katika mradi huo lakini fedha zaidi zinahitajika kuukamilisha ndani ya miaka miwili ijayo.

  Malengo matatu muhimu ni:

  • Kufundisha vikosi maalum vya majeshi katika mkoa huo.
  • Kuwapa mafunzo dhidi ya ugaidi maafisa, kama mahakimu, maafisa wa forodha na wahasibu.AILCT inataka kuunda mitandao ya wataalamu wanaojuana na kufanya kazi pamoja katika mipaka.
  • Kuunda kituo cha kimkakati cha kusoma.
  Tayari dola milioni 27 sawa na (euro milioni 20) zimewekezwa katika mradi huo
  Image caption: Tayari dola milioni 27 sawa na (euro milioni 20) zimewekezwa katika mradi huo

  Uzinduzi wake unakuja siku chache baada ya Ufaransa kutangaza kwamba inakamilisha Operesheni ya Barkhane katika eneo la Sahel, ambalo linakabiliwa ukame kusini mwa Jangwa la Sahara.

  Eneo hilo linajumuisha Mali, Chad, Niger, Burkina Faso na Mauritania.

 5. Jeshi la Msumbiji 'latibua shambulio jipya Palma'

  Mkoa wa kaskazini mwa Msumbiji wa Cabo Delgado umekumbwa na ukosefu wa utulivu kwa muda mrefu
  Image caption: Mkoa wa kaskazini mwa Msumbiji wa Cabo Delgado umekumbwa na ukosefu wa utulivu kwa muda mrefu

  Majeshi ya Msumbiji yamezima jaribio la mashambulizi mapyakutoka kwa wanamgambo wa Kiislamu katika mji wa kaskazini wa Palma, kwa mujibu wa Rais Filipe Nyusi.

  Palma iko karibu na mradi mkubwa wa gesi unaoendeshwa na kapuni kubwa ya kawi ya Total ya Ufaransa.

  Mwezi Machi, mamia ya wanamgambo walio na mafungamano na kundi la Islamic State (IS) walivamia mji huo katika shambulio lililosababisha vifo vya makumi ya watu.

  Rais alisema tukio la wikendi lilihusisha jaribio la wanamgambo wakijaribu kuvamia kijiji cha Lumbi, Wilaya ya Palma. Aliongeza kuwa wanamgambo hao waliwaua wenzao watano waliojaribu kujiondoa.

  Bw. Nyusi alitoa tamko hilo katika mkutano wa chama tawala cha Frelimo uliofanyika Matola, Mkoa wa Maputo.

  Alisema serikali yake iki tayari kuunga mkono msaada wa kigeni kukabiliana na wanamgambo kaskazini mwa nchi hiyo "hakuna mtu anayepaswa kujiona ana kinga au anaweza kupambana na ugaidi peke yake".

 6. Diana Mutisya ameungua majeraha ya maisha tangu shambulio hilo

  Mtumishi mmoja wa serikali nchini Kenya Diana Mutisya amekatishwa tamaa baada ya kubaini kuwa hata pokea fidia kama itakavyokuwa kwa raia wa Marekani waliojeruhiwa wakati wanamgambo wa al-Qaeda walipolipua kwa bomu ubalozi wa Marekani mjini Nairobi miaka 22 iliyopita.

  Soma Zaidi
  next