ICC

 1. Sudan yaidhinisha kwa kauli moja mswada wa kujiunga na mahakama ya ICC

  Sudan iliahidi haki kwa wahanga wa uhalifu uliofanywa Darfur wakati wa utawala wa Bashir
  Image caption: Sudan iliahidi haki kwa wahanga wa uhalifu uliofanywa Darfur wakati wa utawala wa Bashir

  Baraza la mawaziri la mpito la Sudan limepitisha kwa kauli moja muswada ambao utaiandalia njia ya kujiunga na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC), Waziri Mkuu Abdalla Hamdok ameandika katika ujumbe wa Twitter Jumanne.

  Rasimu hiyo imeidhinishwa kwa maandalizi ya mkutano wa pamoja kati ya Baraza Kuu la Uongozi na baraza la mawaziri ili kuipitisha kuwa sheria.

  "Haki na uwajibikaji ni uti wa mgongo wa Sudan mpya, ambayo imejitolea kwa sheria ambayo sote tunataka kuijenga," Bwana Hamdok alisema.

  Hatua hii imesongeza Sudan karibu na kuwakabidhi washukiwa wa ICC wanaotafutwa kwa uhalifu wa kivita na mauaji ya kimbari katika eneo la magharibi mwa Darfur, akiwemo Rais wa zamani Omar al-Bashir.

 2. Kiongozi wa zamani wa Ivory Coast kurejea nyumbani baada ya kuachiliwa na ICC

  Laurent Gbagbo

  Rais wa zamani wa Ivory Coast Laurent Gbagbo anatarajiwa kurejea nchini humu leo kwa mara ya kwanza tangu alipokamatwa na kufikishwa mbele ya Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Jinai (ICC), mnamo Novemba 2011 kutokana na jukumu lake katika ghasia za baada ya uchaguzi ambazo zilisababisha vifo vya maelfu ya watu. Tovuti ya Koaci imeripoti.

  Ndege ya Gbagbo kutoka Brussels inatarajiwa kutua mjini Abidjan saa 1545 gmt.

  Mamlaka za Ivory Coast zimeahidi kwamba atapokelewa "kwa heshima zote kutokana na hadhi ya ofisi aliyoshikilia nchini".

  Kurejea kwa Gbagbo kunatarajiwa kupiga jeki chama chake cha Ivorian Popular Front ambacho kinakabiliwa na mgawanyiko kwa miaka kadhaa sasa.

  Waathiriwa wa ghasia za baada ya uchaguzi wameapa kufanya maandamano atakapotejea.

  Ijapokuwa Gbagbo hatimaye aliondolewa mashtaka yote katika kesi dhidi yake ya ICC tarehe 31 mwezi Machi 2021, bado anakabiliwa na mashtaka nchini Ivory Coast kwa kuhusika na wizi katika Benki Kuu ya taifa hilo la Afrika Magharibi tawi la Abidjan (BCEAO).

  Alihukumiwa kifungo cha miaka 20 jela kwa kuhusika na "wizi wa BCEAO" mnamo Januari 2018.

  Rais Ouattara alimsamehe mtuhumiwa mwenzake katika kesi hiyo lakini hakuwajumuisha "watu waliofunguliwa mashtaka katika mahakama za kimataifa ".

 3. Wahanga wa uhalifu wa kivita wa Uganda 'wanahitaji kufanyiwa mengi zaidi'

  For some Ugandans, finding any sense of closure is still proving hard

  Wakili wa masuala ya haki nchini Uganda Sarah Kihika Kasande amesema hukumu ya Alhamisi dhidi ya Dominic Ongwen imetuma ujumbe kuwa wahusika wa uhalifu watawajibishwa.

  Bi Kasande pia ameiambia kituo cha televisheni cha NBS kwamba mengi zaidi yanahitajika kufanywa kuwasaidia wahanga wa uhalifu wa kivita kaskazini mwa Uganda.

  "Wahalifu waliosalia wanastahili kuwajibishwa kitaifa au kimataifa kwasababu Ongwen hakutekeleza uhalifu huo peke yake," alisema.

 4. Kwanini jaji mmoja alitofautiana na wenzake juu ya hukumu ya Ongwen

  Dominic Ongwen.

  Mmoja wa majaji wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa jinai ICC Jaji Bertram Schmitt ameelezea jinsi mahakama ilivyofikia uamuzi wa kumfunga kifungo cha miaka 25 r rebel kamanda wa waasi Dominic Ongwen.

  Amesema uamuzi huo haukuwa wa pamoja.

  Jaji Raul Cano Pangalangan alikuwa amependekeza kifungo cha miaka 30- jela, akisema mazingira ya utotoni ya Bw. Ongwen haistahili kugubika mateso waliopitia waathiriwa.

  Jaji kiongozi baadaye alisema hukumu yakifungo cha miaka 25 ilifikiwa na majaji wengi.

 5. ICC yamhukumu kiongozi wa zamani wa LRA Dominic Ongwen kifungo cha miaka 25

  Dominic Ongwen

  Mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa jinai ICC imemhukumu kifungo cha miaka 25 kiongozi wa zamani wa waasi wa Lord's Resistance Army,LRA Dominic Ongwen.

  Dominic Ongwen, anayefahamika kama White Ant, alipatikana na zaidi ya makosa 60 ikiwa ni pamoja na uhalifu dhidi ya binadamu na uhalifu wa kivita.

  Waendesha mashtaka wanasema kuwa Bw. Ongwen amepewa adhabu ndogo kwasababu alikuwa ametekwa na LRA akiwa mtoto mdogo.

  Kundi hilo la waasi liliundwa zaidi ya miaka 30 iliyopita ikiendesha shughuli zake nchini Uganda na mataifa jirani.

  Dominic Ogwen alizaliwa mwaka 1975

  Dominic Ogwen ni nani?

  Dominic Ogwen alizaliwa mwaka 1975 katika kijiji cha Choorum wilaya ya Amuru kaskazini mwa Uganda.

  Alitekwenyara na kundi la waasi wa Josephy Kony akiwa mvulana mdogo wakati akielekea shule ya msingi Abili Koro, kulingana na maelezo yake alidai alitekwanyara mwaka 1988 akiwa na umri wa miaka 14.

  Lakini ripoti sahihi zinasemekana alitekwanyara akiwa na umri wa miaka 9 au 10.

  Kwani alibebwa katika safari yao hadi kwenye kambi ya LRA, alikuwa hawezi kutembea.

  Waasi wa LRA

  Mama yake Ogwen alipofahamishwa habari za kutekanywara kwa mtoto wake aliamuwa kuwafata wafuasi hao, na badaye watu walimkuta mama huyo amefariki pamoja na mumewe.

  Baada ya muda akiwa na umri wa miaka 18, Ogwen alipewa cheo cha Brigadier wa kundi la waasi wa LRA na kuongoza kikosi cha Sinia.

  Ogwen alishirika katika matukio mbalimbali ya uhalifu wa kivita mwezi wa Mei mwaka 2004 walishambulia kambi ya ndani ya Lukodi wilayani Gulu kaskazini mwa Uganda.

  Pia alishambulia kambi nyingine za ndani ikiwemo ya Pajule, Odeke na Abok na kushiriki mauaji mbalimbali ya wanchi wasiokuwa na hatia , ubakaji na unyanyasaji wa kigono.

 6. ICC kutoa uamuzi juu ya kuachiliwa kwa Gbagbo wa Ivory Coast

  Bw.Gbagbo

  Mahakama ya Kimataifa ya Kesi za Jinai ICC leo inatarajiwa kuamua ikiwa itadumisha hatua ya kumuondolea mashtaka Rais wa zamani wa Ivory Coast Laurent Gbagbo.

  Bw.Gbagbo na kiongzi wake wa zamani wa Charles Ble Goude walistakiwa kwa kujihusisha na ghasia baada ya uchaguzi katika nchi hiyo ya Afrika ya Magharibi zaidi ya mwongo mmoja uliopita.

  Ghasia zilizuka baada ya uchaguzi wa mwaka 2010 wakai tBw Gbagbo – ambaye alikuwa madarakani kwa muongo mmoja – kukubali kushindwa .

  Waliondolewa kesi ya uhalifu dhidi ya binadamu mwaka 2019.

  Upande wa mashtaka ulikata rufaa dhidiya uamuzi wa kumuondolea makossa Laurent Gbagbo, ukihojijinsi uamuzi wa kwanza ulivyofikiwa na kusisitiza kwamba maelfu ya nyaraka na mashahidi 96 waliotoa ushahidi wao wakati wa kesi, walidhibitisha kuwa kwamba uhalifu ulitekelezwa

  Gbagbo mwenye umri wa miaka 75 amekuwa akiishi mjini Brussels lakini ana matumaini ya kurudi nyumbani ikiwa rufaa ilitowasilishwa na waendesha mashtaka itakataliwa.

  Hukumu hiyo itafuatiliwa kwa karibu Ivory Coast, ambako rais huyo wa zamani anasalia kuwa na ushawishi mkuwa, katika nchi hiyo ambayo bado inajitahidi kupata utulivu wa kisiasa.

  Mwaka jana kulitokea makabiliano makali nchini humo baada ya hasimu wa kisiasa wa muda mrefu wa Bw. Gbagbo, Alassane Ouattara kutangaza kwamba ana mpango wa kugombea urais kwa muhula wa tatu .

 7. ICC kuamua rufaa ya uhalifu wa kivita dhidi ya Bosco Ntaganda

  Bosco Ntaganda was the first person to be convicted by ICC of sexual slavery
  Image caption: Bosco Ntaganda alikuwa mtu wa kwanza kuhukumiwa na ICC kwa utumwa wa kingono

  Mahakama ya Kimataifa ya Kesi za Jinai (ICC) leo inatarajiwa kuamua rufaa iliyowasilishwa mbele yake na kiongozi wa waasi wa Jamhuri ya Kidemorasia ya Congo, Bosco Ntaganda, kupinga hukumu ya uhalifu wa kivita dhidi yake.

  Kamanda huyo wa zamani, aliyepewa jina la utani la "The Terminator", alihukumiwa kifungo cha miaka 30 jela mwaka 2019 baada ya kupatikana na hatia ya makosa 18 ikiwemo mauaji, ubakaji na kutumia watoto kama wanajeshi.

  Alikuwa mtu wa kwanza kushtakiwa na mahakama hiyo kwa tuhuma ya utumwa wa kingono.

  Mashtaka hayo yalihusisha uhalifu uliotekelezwa katika eneo la Ituri lenye utajiri wa madini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo mwaka 2002 na 2003.

  Waendesha mashtaka wanaomba majaji kutoa adhabu kali zaidi.