Rwanda

 1. Vikosi vya DR Congo vyakabiliana na wanajeshi wa Rwanda

  Jeshi la Rwanda halijajibu madai ya tukio hilo
  Image caption: Jeshi la Rwanda halijajibu madai ya tukio hilo

  Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo inasema kuwa vikosi vyake vimekabiliana na wenzao wa Rwanda karibu na mpaka wa mashariki siku ya Jumatatu.

  Msemaji wa jeshi katika Mkoa wa Kivu Kaskazini alisema vikosi vya Rwanda vilivuka mpaka na kuingia Congo katika hatua ambayo ilisababisha makabiliano.

  “Kitengo cha wanajeshi wa Rwanda kiliingia kilomita tano ndani ya Congo…Hauwezi kuelezea jinsi wanajeshi waliojihami walivuka mpaka na kuanza kupiga risasi," Brigedia Jeneral Sylvain Ekenge taliambia BBC Idhaa ya Maziwa Makuu.

  Majeshi ya Rwanda hayajatoa tamko lolote kuhusu madai hayo au kujibu ombi la BBC.

  Ramani

  Video zinazoshirikishwa mitandaoni zinawaonesha wenyeji waliokuwa na hofu wakikimbia huku vikosi hivyo viwili vikikabiliana kwa rasasi. Wanajeshi wa Rwanda baadaye walirudi nyuma na kwenda nyumbani.

  “Kwa bahati nzuri hakuna mtu aliyefariki katika tukio hilo”, Jenerali Ekenge alisema.

  Viongozi na wakazi wa eneo hilo walirejea majumbani mwao baada ya hali ya utulivu kudumishwa.

  Mvutano wa mipaka kati ya majirani hao wawili wa Afrika Mashariki ni jambo la kawaida kwa sababu ya biashara haramu, ukosefu wa mipaka wazi na mashambulio ya waasi.

  Tshisekedi na Kagame watofautiana kuhusu 'ukatili DRC'

  Kwanini hali ya usalama imeendelea kuwa tete nchini DRC?

 2. Rais wa Rwanda amsamehe waziri mkuu wa zamani kwa kugushi hundi

  r

  Rais wa Rwanda Paul Kagame amemsamehe waziri mkuu wa zamani Pierre Damien Habumuremyi ambaye alikuwa akitumikia kifungo cha miaka mitatu kwa kosa la kughushi hundi .

  “Kwa mujibu wa mamlaka aliyopewa”, ilisoma taarifa kutoka mkutano wa mawaziri wa kufikia azimio hilo ambao ulifanyika Jumatano, Rais Kagame alitoa msamaha kwa bwana Pierre Damien Habumuremyi.”

  Mtoto wake Appollo Mucyo, ambaye alikuwa na kampeni katika mitandao ya kijamii ya kutaka baba yake aachiwe huru aliandika kwenye Instagram: “Moyo wangu umejawa na furaha isiyo na kifani , sina maneno sahihi ya kueleza jinsi nilivyofurahi.

  “Ninamshukuru Mungu kwa yote, upendo nilionao kwa nchi yangu …bado uko vilevile.Ninashukuru…”

  Bwana Habumuremyi,mwenye umri wa miaka 60, alikuwa waziri mkuu wa tisa kuanzia mwaka 2011 mpaka 2014,kabla ya hapo alikuwa waziri wa elimu.

  Mwaka jana mwezi Novemba, alihukumiwa kifungo cha miaka mitatu kwa kosa la kughushi hundi ambayo aliitoa katika chuo kikuu cha Kigali- Christian University of Rwanda, ambacho tangu wakati huo kilikuwa kimefungwa.

  Alitakiwa kulipa $879,811 kama fidia.

  Chombo cha habari cha taifa kiliripoti Alhamisi kuwa bado anahitajika kulipa fedha hizo na akifanikiwa hilo ndio akaunti zake za benki zitafunguliwa na kuachiwa mali zake zilizotaifishwa.

  Wakati wa kusikilizwa kwa kesi hiyo bwana Habumuremyi alisema alitoa hundi kama dhamana kwasababu wapokeaji wote walikuwa wamepokea fedha zao.

  Mpaka alipokamatwa Julai 2020, alikuwa kiongozi wa kansela ya mashujaa , amri za taifa na mapambo ya heshima.

 3. Video content

  Video caption: Mauaji ya Kimbari Rwanda: Jinsi mafunzo ya sanaa yanavyowaponya wajane wa mauaji hayo

  Wajane wa mauaji ya kimbari ya Rwanda wamekuwa wakipokea mafunzo ya sanaa ya michezo kama njia ya kupona kutokana na majeraha waliyo nayo kwa miaka mingi kufuatia kupoteza wapendwa

 4. Wanaharakati: Ufaransa lisiwe eneo la hija la wahusika wa mauaji ya kimbari, Rwanda

  Theoneste Bagosora
  Image caption: Theoneste Bagosora alikuwa akitumikia kifungo cha miaka 35, kwa kosa la kuhusika katika mauaji ya kimbari

  Wanaharakati wa Rwanda wameitaka Ufaransa kutoruhusu ardhi yao kuzikwa wahusika wakuu wa mauaji wa kimbari ya mwaka 1994.

  Walisema hawataki kaburi la Theoneste Bagosora kugeuka kuwa eneo la hija kwa wale waliounga mkono mauaji ya watusi 800,000 na baadhi ya wahutu.

  "Tayari Ufaransa inawapa hifadhi washukiwa wengi wa mauaji ya kimbari na basi kusiwe sehemu ya kuhiji", kundi la wanaharakati, Collectif des Parties Civiles pour le Rwanda (CPCR), ilitoa taarifa .

  Baadhi ya wana familia wa bwana Bagosora wanaishi Ufaransa.

  Bagosora, amefariki Jumamosi ,nchini Mali akiwa na miaka 80 ambapo alikuwa anatumikia kifungo cha miaka 25-gerezani kwa makosa ya vita.

  Alikuwa ni afisa wa juu wa wizara ya usalama ya Rwanda wakati wa mauaji ya kimbari.

  Haata hivyo hijajulikana bado ni wapi Bagosora atazikwa.

 5. Paul Rosesabagina

  Paul Rusesabagina aliangaziwa kama mtu aliyetumia ushawishi wake - na rushwa- kuwashawishi maafisa wa kijeshi kuwapa njia salama ya kuwatorosha karibu watu1,200 ambao walitafuta maficho katika Hôtel des Mille Collines, ambayo alikuwa meneja wake wakati wa mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 dhidi ya Watutsi.

  Soma Zaidi
  next
 6. Hukumu dhidi ya Rusesabagina kutolewa leo Rwanda

  Rusesabagina

  Mahakama mjini Kigali leo inataraji kutoa hukumu yake dhidi ya Paul Rusesabagina, mkosoaji mkuu wa serikali ya Rwanda.

  Yeye na washirika wenzake 20, watuhumiwa kwa ugaidi ambao unaunahusiana wa mashambulio yaliyofanywa na kundi la waasi la MRCD- FLN dhidi ya Rwanda miaka ya 2018 na 2019.

  Waendesha mashtaka waliomba hukumu ya kifungo cha maisha jela dhidi ya Rusesabagina aliyejitoa katika kesi hiyo mara tu ilipoanza kusikilizwa kwa madai kuwa hawezi kupata haki katika mahakama za Rwanda.

  Juhudi za Bwana Paul Rusesabagina ambaye ni mwanahotelia wa zamani zilisaidia kuwaokoa zaidi ya watu 1200 wakati wa mauaji ya kimbari nchini humo ziliangaziwa katika filamu ya Marekani, Baadaye alikuwa mkosoaji wa serikali ya Rais Paul Kagame.

  Aliishia kushtakiwa na kufungwa nchini Rwanda baada ya kudaiwa kutekwa mjini Dubai. Rwanda imekanusha kumteka.

  Binti yake Carine Karimba ameiambia BBC kwamba hawatarajii haki yoyote kutoka kwa mfumo wa haki wa Rwanda.

  "Tunajua kwamba baba yangu atapatikana na hatia... Hatuna matumaini yoyotekatika mfumo wa haki wa Rwanda...Matumaini yetu yako katika haki ya kimataifa, jamii ya kimataifa," alisema.

  "Baba yangu hakutendewa haki. Haki zote za kimsingi za babangu yangu...Tulijua kuwa hakutakuwa na kesi ya haki kwa baba yangu na sasa ulimwengu unajua pia, "aliongeza.

 7. Kifo cha msanii nyota wa Hip Hop Rwanda: Mamlaka ya magereza yatoa taarifa

  Msanii huyo alizuiliwa mnamo Aprili baada ya kufanya sherehe kwa kukiuka kanuni za Covid
  Image caption: Msanii huyo alizuiliwa mnamo Aprili baada ya kufanya sherehe kwa kukiuka kanuni za Covid

  Rapa maarufu wa Rwanda ambaye alikuwa chini ya ulinzi wa polisi tangu Aprili amekufa ghafla akiwa na umri wa miaka 33.

  Mamlaka zinasema Joshua Tuyishime, maarufu Jay Polly, alifariki baada ya kunywa mchanganyiko wa dawa iliyokuwa imetengezwa na wafungwa wengine wawili.

  Msanii huyo alikamatwa nyumbani kwake miezi minne iliyopita kwa kufanya sherehe kinyume na kanuni zilizowekwa kukabiliana na Covid 19.

  Huduma ya Magereza nchini Rwanda imesema rapa huyo alikuwa na matatizo ya kiafya na alilazwa hospitalini Jumatano jioni. Alikufa saa kadhaa baadaye. Mamlaka zinasema zinachunguza chanzo cha kifo chake.

  Mashabiki wake wamekuwa wakimuomboleza katika mitandao ya kijamii nchini humo.

  Msani mwingine wa Rwandan, Kizito Mihigo, alikutwa amekufa akiwa chini ya ulinzi wa polisi mapema mwaka jana.

  Msanii huyo wa muziki wa injili alikuwa amesifiwa kwa talanta yake kubwa kitaifa lakini baadaye alishtumiwa kwa usaliti.