Misri

 1. Mwanafunzi wa Nigeria atuhumiwa kumpiga mhadhiri hadi kukosa fahamu

  Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Ilorin nchini Nigeria amezuiliwa na polisi baada ya shutuma za kumpiga mhadhiri wa kike.

  Polisi wanasema mwanafunzi huyo alikuwa ameenda kumuona msimamizi kuhusu kazi yake ya mwaka wa mwisho wa mradi wakati kutoelewana kulipotokea.

  Inadaiwa alimvamia mhadhiri huyo ambaye alipata jeraha kichwani na kuzimia.

  Mhadhiri huyo amelazwa katika hospitali isiyojulikana huku mwanafunzi huyo akizuiliwa na polisi.

  Msemaji wa chuo hicho Kunle Akogun alithibitisha kisa hicho katika taarifa iliyowasilishwa kwa vyombo vya habari siku ya Jumapili.

  Alisema mhadhiri huyo anaendelea kupata nafuu.

 2. Misri kuwazuia wafanyikazi ambao hawajachanjwa kwenda kazini

  Egypt has administered about 30m Covid vaccine doses

  Misri itawazuia wafanyikazi wa umma ambao hawajachanjwa dhidi ya kuingia katika majengo ya serikali kutoka katikati ya mwezi ujao.

  Ilani ya baraza la mawaziri Jumapili ilisema wafanyikazi watalazimika kupewa chanjo au kufanyiwa vipimo vya Covid kila wiki ili waruhusiwe kuingia kwenye majengo ya serikali kutoka 15 Novemba.

  Baraza la mawaziri pia liliruhusu kufunguliwa kwa bafu katika misikiti kutoka Jumatano.

  Bafu zilifungwa mnamo Machi mwaka jana kama sehemu ya hatua za kuzuia kuenea kwa virusi vya Corona Serikali pia imetenga pauni bilioni Moja za Misri ($ 64m; £ 47m) kushughulikia janga hilo.

  Misri imetoa chanjo zaidi ya milioni 30 kwa raia wake dhidi ya idadi ya watu zaidi ya milioni 100, kulingana na data kutoka kwa wizara yake ya afya.

 3. Afungwa miaka mitatu kwa kuwapiga picha wanawake Misri

  Mahakama moja nchini Misri imemhukumu kifungo cha miaka mitatu jela mfanyakazi wa uwanja wa ndege wa Cairo kwa kuwapiga picha kisiri wasafiri wanawake.

  Mmoja wa wanawake hao aliwasilisha malalamishi baada ya kugundua mwanamume huyo amempiga picha sehemu nyeti.

  Uchunguzi wa simu yake ulibaini kuwa aliwafanyia karibu wanawake 20 kitendo sawa na hicho.