Uchaguzi wa Tanzania 2020

 1. Video content

  Video caption: Tanzania: ‘’Walidhani mimi ni afisa usalama kwa kuvalia suti'

  Dickson anauza kahawa akiwa amevalia suti wakati wote wa kazi yake, jambo ambalo anasema baadhi ya watu hudhani yeye ni afisa wa serikali na si muuza kahawa.

 2. Video content

  Video caption: ‘Kwanza kazi ifanyike ya 2025 aachiwe Mungu’ Rais Samia

  Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema kuwa Watanzania wamekubali tozo lakini jambo linalolalamikiwa ni kiasi kinachokatwa.

 3. Video content

  Video caption: Virusi vya corona: Zanzibar yapinga kuwapa watu chanjo kisiri

  Serikali Visiwani Zanzibar imekanusha taarifa kwamba wameanza kutoa chanjo dhidi ya virusi vya corona

 4. Video content

  Video caption: Samia Suluhu Hassan aapishwa kuwa Rais wa Tanzania

  Samia Suluhu Hassan aapishwa kuwa Rais wa Tanzania

 5. Habari za hivi pundeRais wa kwanza mwanamke kuapishwa leo Tanzania

  samia

  Makamu wa rais wa Tanzania Bi. Samia Suluhu Hassan ataapishwa leo Ikulu, Jijini Dar es Salaam majira ya saa nne asubuhi saa za Afrika Mashariki.

  Bi. Samia Suluhu Hassan 61,atakuwa ndio mwanamke wa kwanza kushika wadhifa huu nchini Tanzania na wa pili Afrika Mashariki.

  Slyvie Kiningi ndiye alikuwa rais wa pekee mwanamke aliyeshika nyadhifa ya urais Afrika Mashariki nchini Burundi.

  Bi.Samia anaapishwa kushika wadhifa huo kufuatia kifo cha rais Magufuli kilichotokea Jumatano, Machi 17, 2021.

  Samia atashikilia wadhifa huo kwa kipindi kilichosalia cha muhula wa urais mpaka 2025, kwa mujibu wa katiba ya Tanzania.

  View more on twitter

  Hii ni mara ya kwanza katika historia ya Tanzania kwa Rais kufariki akiwa madarakani.

  Kwa mujibu wa kifungu cha 37 (5) cha Katiba ya nchi hiyo iliyotungwa mwaka 1977, nafasi ya urais inapokuwa wazi kwa sababu yoyote ikiwemo kifo, viongozi watatu wameorodheshwa na ni Makamu wa Rais, na endapo hatakuwepo atachukua Spika wa Bunge na kama hayupo atachukua Jaji Mkuu.

  Kwa Watanzania wengi, jina la Samia Hassan Suluhu (61) lilipata umaarufu zaidi wakati alipoteuliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Bunge la Katiba lililoteuliwa mwaka 2014.

 6. Ezekiel Kamwaga

  Mchambuzi

  ccm

  CCM ni miongoni mwa vyama vichache vya ukombozi ambavyo bado vimesalia madarakani takribani miaka 50 baada ya nchi nyingi za Afrika kuwa huru.

  Soma Zaidi
  next
 7. Tanzania yasema haijapata taarifa rasmi ya vikwazo vya Marekani

  Waziri wa mambo ya Nje wa Marekani Mike Pompeo

  Wizara ya Mambo ya Nje ya Tanzania imesema haijapata taarifa rasmi ya maafisa kadhaa wa nchi hiyo kuwekewa vikwazo vya kuingia Marekani.

  Jumanne wiki hii, aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Mike Pompeo alitangaza kuwawekea vikwazo maafisa wa Tanzania ambao hawakutajwa majina kwa kile alichokiita “kuvuruga uchaguzi wa Oktoba 28.”

  Gazeti la Mwananchi la nchini Tanzania hii leo limemnukuu Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Tanzania Emmanuel Buhohela kuwa hawana taarifa rasmi kutoka Marekani juu ya suala hilo.

  “Hatujapata taarifa rasmi zaidi ya kuona katika mitandaoni na hatuwezi kufanyia kazi vitu vya mitandaoni. Wizara yetu ina utaratibu mzuri wa mawasiliano na Balozi na hatujaletewa taarifa rasmi,” Buhohela ameiambia Mwananchi.

  Gazeti hilo pia limemnukuu Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Tanzania (NEC), Jaji Semistocles Kaijage ambaye akisema kuwa maelezo ya taarifa hiyo hayapo wazi na haijaeleza “uchaguzi umeingiliwa kivipi.”

  Soma zaidi:

  Uchaguzi Tanzania 2020: Marekani yatangaza vikwazo vya kusafiri dhidi ya maafisa wa Tanzania